Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

11887906_796415783809748_1990254608746852463_n.png
 
Pinda-Kampeni.JPG

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akihutubia wananchi wa Rukwa wakati akimnadi mgombea wa CCM, Dk John Magufuli​

26 Agosti 2015

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, jana alikuwa mstari wa mbele kunogesha kampeni za mgombea wa urais wa CCM, Dk John Magufuli, akisisitiza ni chaguo sahihi kwa Watanzania na kwamba hata upatikanaji wake ulikuwa sahihi kwa asilimia 100 na kwamba, yeye aliyekuwa mjumbe wa vikao hivyo ni shuhuda wa hilo.

Kutokana na ukweli huo, amesema hana kinyongo, ndiyo maana yuko mstari wa mbele kumnadi aweze kuwa Rais wa Tano wa Tanzania baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Akizungumza na wananchi katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini hapa, Pinda alisema kuna baadhi wamesusa na hivyo haya yeye alipokosekana katika uzinduzi wa kampeni za Urais za CCM jijini Dar es Salaam, kuna waliompigia simu na kuhoji kwa nini hakuwepo.

"Mimi ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Kamati ya Maadili, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Nimeona nisiache kuja huku, maana Waswahili hawaachi kusema, unaona hata Waziri Mku kamsusia mwenzake, maana alikuwa naye katika kinyang'anyiro.

"Mimi ni muumini wa chama changu, kilichofanyika mpaka tukampata Magufuli nataka niwaambie ni halali asilimia 100," alisema. Alifafanua kuwa walichokuwa wakitafuta CCM ni kumpata mtu ambaye kwa wale waliokuwa katika kamati na vikao hivyo, wamekubaliana kuwa anaweza kuwavusha bila matatizo.

"Mimi nilikuwepo na nilikuja mkanidhamini na niliwaambia tulikuwa 42, ikaja 38 nikasema atabaki mmoja. Tumeletewa Magufuli, si mwingine si Pinda. Chama hapo kama ni kupiga, basi kimelenga shabaha. "Huyu baba ni mwadilifu na mchapakazi sana, ana huruma sana lakini kwa mambo yenye uongo, wakwepa kodi, wezi ni mkali sana…

Nilitaka kuja kuwathibitishia kuwa mimi nimeungana naye kwa asilimia mia," alisema. "Juzi mtu mmoja alinipigia akasema mbona katika uzinduzi hukuwepo, nikamjibu kwa hiyo?" nikahoji. Akaongeza: "Tumepewa heshima ameanzia huku Katavi na Rukwa, namngoja huku.

Sisi barabara tumepata, mkoa wa Katavi tumepata wilaya na kata za kutosha, sasa zawadi ni kumpa kura". Wapanda daladala Alisema anashangaa imekuwaje watu waanze kupanda daladala sasa kwenda Chanika na kwingineko Dar es Salaam na kuhoji; "Siku zote alikuwa wapi.

Anangoja moto umewaka ndio anapanda?" Magufuli Akizungumza katika mkutano huo, Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli alianza kwa kusalimia kwa karibu lugha kumi na kusema ataunda serikali ya mawaziri wachache, lakini kazi atakazowapa anahisi baadhi watakimbia.

Aliahidi kuhakikisha wafanyabiashara wadogo hawabugudhiwi, wakiwemo bodaboda na mamalishe na kuhakikisha wafanyabiashara wakubwa wanalipa kodi ili ihudumie wananchi.

Alisema atahakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji, barabara, umeme na nyingine na atawabana wanaotumia fedha za umma vibaya, ambao ana hakika hawatampigia kura.

Aliwataka Wanasumbawanga, kumpigia kura kwa wingi kwa kuwa wachache waliokuwa wakijinufaisha kwa fedha za umma na rushwa, ana hakika hawatampigia kura. Alitoa mfano wa Mfuko wa Barabara ambao ameusimamia tangu ulipokuwa ukikusanya Sh bilioni 70 mpaka sasa unaingiza zaidi ya Sh bilioni 890, kuwa waliotumia vibaya fedha hizo wamekiona, hivyo anajua hawatampigia kura, lakini akawataka wanaohitaji barabara, wampigie kwa wingi.

Katika hatua nyingine, alionya watu wanaouza dawa za Serikali katika maduka binafsi na kuongeza kuwa, watu hao moto unawajia kwa kuwa hataki wananchi waandikiwe dawa hospitali, kisha watumwe kwenda kununua dawa katika maduka binafsi.

Alihoji, hayo maduka yanakopata dawa ambako Serikali haiwezi na kuongeza kuwa anajua kuna mchezo mchafu wa kuuza dawa za umma hivyo wauzaji hao wasubirie moto wake.

Kuhusu atakapopata fedha za kutekeleza ahadi zake, alisema yeye amekuwa serikalini kwa miaka 20 hivyo anajua kuna wala rushwa na kuonya kuwa, wala rushwa hao watarajie kupambana na yeye.

Pia aliahidi kutoa mikopo kwa kila kijiji, ili kusaidia vijana, wanawake na wananchi wengine kwa ujumla, kuanzisha na kukuza biashara zao, huku akiwahakikishia kuwa hakutakuwa na manyanyaso kwao kwa kuwa anataka wajenge maisha yao.

Ahadi zingine ambazo mgombea huyo amekuwa akitoa kwa wananchi ni pamoja na kuanzisha ujenzi wa barabara, kumalizia zilizoanza kujengwa na kuendeleza zile zilizoko katika hatua za upembuzi yakinifu.

CHANZO:Habari Leo
 
Bac wakaja sumbawanga mjini wakasema diamond atakuwepo,,watu kuckia hvyo waliminka vbaya,mpaka anamalza kampen hakuna diamond wala msanii alikuwepo...
 
Hongera magufuli na mheshimiwa waziri mkuu pinda,na bado ccm mbele kwa mbele.
 
Wapinzani wamechuchumaa.

Na nawaambieni tena hii si mara yangu ya kwanza ni kwamba CCM hamuwawezi, fanyeni mtakavyofanya nyinyi mtabaki kuwa wasindikizaji.

Nyinyi wenyewe wapinzani mmeonyesha udhaifu na unyonge wa hali ya juu mmeshindwa kuwa na msimamo kumuweka mgombea wenu ambae mlianza nae enzi na enzi, ina maana nyinyi wenyewe hamjiamini?

Wapinzani kaeni kimya imekula kwenu, mmeshapigwa bao. Eti Dar mpaka Moro...

Tatu bila...

Tatu bila...

Tatu bilaaa...
 
Wapinzani wamechuchumaa.

Na nawaambieni tena hii si mara yangu ya kwanza ni kwamba CCM hamuwawezi, fanyeni mtakavyofanya nyinyi mtabaki kuwa wasindikizaji.

Nyinyi wenyewe wapinzani mmeonyesha udhaifu na unyonge wa hali ya juu mmeshindwa kuwa na msimamo kumuweka mgombea wenu ambae mlianza nae enzi na enzi, ina maana nyinyi wenyewe hamjiamini?

Wapinzani kaeni kimya imekula kwenu, mmeshapigwa bao. Eti Dar mpaka Moro...

Tatu bila...

Tatu bila...

Tatu bilaaa...
Sijui umeandika nini.


swissme
 
Duh!
Mama Samia naona kamuacha mwenza wa ukawa kwa mbali sana! Ukweli, mgombea mwenza wa ukawa peke yake hawezi kukusanya umati huu!
 
wanachama wa CCM ni wachache sana kwenye mkutano huo. sioni sare zao. nakumbuka siku ya ufunguzi pale jangwani sare zilikuwa nyingi lakini leo hazionekani tena DAR kila mtu anaogoba kuvaa kwani Wanajua MAGUFULI HASHINDI
 
Back
Top Bottom