Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

attachment.php
 
Ccm Tunduma ni sawa na leo hii uvae sare za ccm upite nazo Posta au Kariakoo.
Respect Wa Boda njoo huku uwape hali halisi ya Tunduma hawa wazee wa Fisi.

watu wote wako bize na mambo yao,,,asilimia 70 ya waliohudhuria hapo wamekwenda kuwaangalia wasanii tu

Siuna macho na masikio tunduma ngome yao ukawa angalia watu walijitokeza kusikiliza ilani ya mgombea mwenye sera za kuipeleka nchi mbele kwa amani na utulivu

Watu wa Tunduma na waaminia mikutano ya CCM watahudhuria na kipigo kwa CCM watatoa.
1440585904926.jpg1440585945109.jpg

Hakuna msanii hata mmoja alietumbuiza hapa, watu tumekuja kusikiliza sera ambayo ni haki ya kila mwananchi.

Kila chama kitasikilizwa maana ndio wakati wao kuuza sera.
 
Mgombea wa CCM azidi kung'ara kwa wananchi kila anapopita kujinadi,ni hv karibuni amezindua kampeni na chama chake kwa kishindo kikubwa kisichokua cha kawaida kutokana na kundi kubwa la watu waliojitokeza kumshuhudia mwana sayansi huyo akihutubia mkutano huo.Magufuli alijinadi na kuuonyesha umma wa wa Tanzania kua anaweza na ndio dawa ya matatizo ndani ya nchi yetu hii.Hata hvyo baada ya uzinduzi huo aliendelea kuzuru mikoa mingine kama Katavi,Rukwa na kwengineko kote huko alikopita ameonekana kung'ara isivyokawaida kutokana na wim,bi kubwa la watu nwanvyojitokeza kumshangilia nakuonyesha wanamatumaini makubwa kwa kiongozi huyu huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kusema hakika Lowasa hatumtaki aende akachunge ng'ombe kwao Monduli.
 
Ukitaka kujua tofauti kati ya Lowassa na Magufuli; 1. Kila anacho fanya Lowassa tz nzima wanataka wakijue, mfano katembea na Daladala na kwenda Sokoni tz nzima imejua na kwa wakati huo huo Magufuli yupo Katavi anatoa ahadi hewa na hakuna chombo cha habari wala mtu anaye jali wala kujadili nini Magufuli anafanya au amesema. Na sasa serikali kwa kutumia vyombo vyake vina pambana na Lowassa kama kuzuia maandamano ya kuelekea kwenye mikutano, kuzuia asifanyie kampeni uwanja wa Taifa, Halmashauri kuhujumu uzinduzi wake kwa kuzuia uwanja wa jangwani, Polisi kuanza kuzuia Lowassa asiende Sokoni au kupanda Daladala!
 
Chama cha Mapinduzi kisimwache Magufuli peke yake, hasa wakati huu wa kampeni. Jaribuni kumtengenezea mambo ambayo anapaswa kuyaongea mbele ya wapiga kura.
Jana nimeshangaa badala ya kumwaga sera huko katavi analalamika kuwa hajapanda chopa ili aweze kuwa karibu na wananchi, aone shida zao. Na akawatahadharisha kuwa kuna wengine watakuja na chopa, msiwasikilize, ni wajuu mno hawawezi kujichanganya na ninyi maskini.
Hapo nikaona mzee mzima hajajipanga, analialia tu
 
Yan anaongea km hajielewi kabisa...!
Yan badala ya kuzungumzia mambo yake anakomaa na vijembe vya kijinga
 
CCM ni chama kinachokufa ,sasa kipo kwenye sakatulmauti ,katika mikutano yao yote wanayofanya watatoa maneno mazito ambayo yatahitaji kuchambuliwa kwa kina na pia kunukuliwa na kuwekwa kwenye kumbukumbu;

Tunatarajia mengi sana kutoka kwa Mgombea Makufuli akinadi sera zilizonadiwa na wagombea waliopita ,kwa ufupi ni yaleyale waliyopita na wale walioahidi kutoa mabilioni ila hawa wamekuja na mamilioni ,umeona ni yale kwa yale,

Ukishawasikiliza maneno yao yawe mbolea ya utekelezaji wa kuiondoa CCM madarakani na si vinginevyo.
 
Magufuli kumsikiliza inabidi uwe mpole mana anaongea utumbo tupu
 
Back
Top Bottom