Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Wanaukumbi..

Kutokana na imani waliyonayo watanzania na kumbukumbu za kazi alizofanya Lowassa ni Kazi nzito kumnadi Magufuli na uccm wake.

Ndio maana wamepigwa upofu wakabandika mabango wa ugumu huo ktk matangazo kuwa HAPO WANA KAZI.
 
Tumeshachoka na ahadi hewa, badala ya kutueleza mmefanya nn mpaka sasa munatuandalia matamasha ya music na katutukana.El hata asipofika sehemu niliyopo kura yangu ni rasmi kwake.
 
Acheni kutufanya cc wajinga huyo makomeo hana lolote ataendelea kutumiwa kama lemmote, hakuna cha kujenga tanzania mpya wala nini imefika wakati wa Kufanya Mabadiliko. Tumechoka kudanganywa.
 
Nadhani mngetueleza kwanza kwa nn nchi hii ni masikini ilhali tuna rasilimali kibao?? Hatuhitaji sera wakati huu maana mnazo nyingi bado hamjakamilisha utekelezaji wake
 
Hivi huyu Magufuli naye kwenye mahesabu ya kupewa urai naye yupo?.

Mtu ambaye ana jidai kuwa ni mtu muadilifu lakini ana washawishi wapiga kura wawachague wabunge wa CCM waovu kwa kuwa siyo malaika ili wamsaidie kufanya kazi katika serekali yake.

Magufuli huyuhuyu ambaye amesema kuwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi na watoa rushwa,wakati mafisadi na watoa rushwa wameshonana ndani ya chama chake na wengine ndio hao anaowanadi ili wapate ubunge na wakipata ubunge wamsadie katika serekali yake huku akijua kuwa hata nafasi zenyewa walizipata kwa njia za rushwa kipindi cha mchakato wa kura za maoni.

Magufuli huyuhuyu ambaye ameanza kudanganya umma kuwa mafisadi wote wamemkimbia kwa kuhama chama baada ya kuona kuwa amepitishwa kuwa mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi kwa kuwa wanaogopa asije akawachukulia hatua za kisheria.

Kwa hiyo ina maana kuwa wewe kama ni fisadi ukishamkimbia Magufuli CCM haupaswi kuchukuliwa hatua za kisheria,na kama wewe ni fisadi ukiendelea kubaki ndani ya CCM bila kumkimbia Magufuli unatakiwa upigiwe kura kwa kuwa siyo malaika.

Wakati wananchi tumeshagundua ujanja wake kuwa ana taka kuaminisha umma kuwa mafisadi wa CCM wameondoka wakati wananchi tunajua kuwa mafisadi wapo wa kumwaga ndani ya CCM.

Wakiwepo wazee wa vijisenti,kiasi cha mboga na wazee kadha wa kadha wa ESCROW na baadhi yao ndio hao anaotushawishi tuwachagua wamsadie kazi kwa kuwa siyo malaika.

Labda kama ni Magufuli mwingine hata kura yangu atapata.
 
Maadhimisho ya Miaka 54 ya ahadi hewa Tanzania

Maadhimisho ya miaka 54 ya kuendelea kuwa nchi masikini Tanzania
 
KWANINI CCM INA MKAKATI WA KUJENGA UCHUMI WA VIWANDA 2015-2020

Azwamu ya nne chini ya Mh. Prof. Kikwete imeweka mazingira rafiki na mazuri kwa kuanzishwa na kujengwa kwa viwanda hapa nchini.

Kujengwa na kuimarishwa kwa barabara za lami zinazounganisha mikoa na nchi za mipakani

Kujengwa na kuimarishwa kwa viwanja vya Ndege katika maeneo ya Mwanza, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Mtwara,.Tabora, Dodoma na Zanzibar.

Kukamilika wa bomba la gesi toka Mtwara kuja Dar kunatoa uhakika wa uwepo wa nishati ya uhakika na kwa gharama nafuu zaidi.

Kuimarishwa kwa bandari za Dsm, Zanzibar, Tanga na Mtwara

Kuanza kwa ujenzi wa reli mpya yenye ubora wa kimataifa yaani standard gauge toka Dar, Tanga,Arusha, Kigali na Uganda

Kuanza kwa ujenzi wa reli mpya ya kusini

Uchumi wa viwanda unataka nishati ya uhakika na nafuu, miundombinu bora, malighafi na utulivu wa kutosha. Kwa sasa vyote tunavyo.
Zaidi ni kupata kiongozi atakayesimamia na kuimarisha maendeleo kwa kasi zaidi.

TANZANIA KWA SASA TUNAHITAJI KIONGOZI MWADILIFU,ASIYE NA MAKUU,MWENYE KUTAKA MAENDELEO KWA KASI ZAIDI NA ANAEJUA SHIDA ZA WANAINCHI WAKE:

JOHN POMBE MAGUFULI kwa sasa anazo sifa zote stahiki za kuwa kiongozi wa Tanzania.
HAPA NI KAZI TU.

Acheni unafiki hamuwezi kuwaita na kuwadhalilisha watu wapumbavu, malofa, vibaka, wanywa viroba, mama ntilie, madada poa halafu mfikirie kuwapatia ajira.
 
Wanaukumbi..

Kutokana na imani waliyonayo watanzania na kumbukumbu za kazi alizofanya Lowassa ni Kazi nzito kumnadi Magufuli na uccm wake.

Ndio maana wamepigwa upofu wakabandika mabango wa ugumu huo ktk matangazo kuwa HAPO WANA KAZI.


attachment.php
 
Kinachonifurahisha huyu gamba ameleta uzi na mamluki wake na mbwembwe kibao lakini makamanda wakiuliza maswali hawajibiwi zaidi ya wafa maji wakisema tu Mh Lowassa hawezi. Hapa wanadhihirisha kuwa hawana sera wako tu kama huyo msuKUMA wao pombe magunduli.
 
Nchi hii haihitaji watu wanaoongea jukwaani masaa kumi wala watoka povu midomoni,kinachohitijika ni kufanya kazi kwa vitendo,suala la afya ya mtu naamini wote wana matatizo yao ambayo wanayajua wenyewe na wake zao,binafsi nataka mabadiliko na kura yangu ni kwa LOWASSA,hata iweje.
Nchi kama Tz ina rundo la hotuba hasa za hayati Mwl.JK.Nyerere,binafsi sihitaji porojo za mtu kwa kuw matatizo ya watanania yanaeleweka,kilichobaki ni kuyatatua tu,kwa hiyo hata akipatikana rais bubu,na akaonesha nia na dhamira ya kutatua kero kwangu mimi ni sawa tu.



Bila kutumia usafiri wa anga hawezi kuicheza ngoma ya kusafiri na gari katika maeneo mengi hapa Tanzania.

Bila kutanguliza wapambe kwenye mikutano yake, hawezi kusimama bila kukaa kwa saa moja achilia mbali wananchi kukielewa kile anachokiongea.

Kwa sasa kila anapofungua mdomo, wananchi wanajiuliza maswali mengi kuhusu uwezo wake wa kujieleza achilia mbali afya yake.

Wakiwa wanasubiri kuanza kampeni, Magufuli kwa sasa yuko huku,



 
Last edited by a moderator:
NI KAZI NGUMU SANA KUMNADI MAGUFULI, MTU ALIYEPO KWENYE SYSTEM YA CCM ILIYOTUONGOZA KWA MIAKA ZAIDI YA 50,NA BADO WANATOA AHADI ZA UONGO NA WANAIBA FEDHA NA MALI ZA UMMA (NA USHAHIDI UPO ILA CCM WANALINDANA)....Wananchi Tumeichoka CCM.
 
Back
Top Bottom