Ccm bila kupakia watu kwenye matipa hakuna mkutano hata mama samia nae anasomba wanafunzi vibaya mno ninaomba kova atoe Povu i mean Tamko.
Porojo wakati huu si mahali pake. Ungeokoteza hata picha ya shule yoyote tu angalau kuhalalisha taarifa yako.Akiwa katika ziara ya kujinadi wilayani Rungwe Magufuli amesababisha wanafunzi watolewe madarasani ili wapelekwe uwanjani anapohutubia, jambo hilo limezua jazba kwa wazazi wakihoji uhalali wa kuwanyima haki yao ya kusoma huku walio darasa la saba wakijiandaa na mitihani ya kuhitimu. Japo wapo watu wazima wamesombelewa na malori kwenda mkutanoni. Suala la wanafunzi ndilo gumzo kwa wananchi wengi wanatafuta wanasheria kuhoji jambo hilo kwa sasa wanafunzi na waalimu wapo mitaani, hivyo tunahoji mgombea Urais ana mamlaka gani hadi afisa elimu awatoe wanafunzi madarasani.
Picha tafadhari hapo nyumbani kwetu wengine , tuone hao wadogo zetu kama kweli walipelekeshwa
Akiwa katika ziara ya kujinadi wilayani Rungwe Magufuli amesababisha wanafunzi watolewe madarasani ili wapelekwe uwanjani anapohutubia, jambo hilo limezua jazba kwa wazazi wakihoji uhalali wa kuwanyima haki yao ya kusoma huku walio darasa la saba wakijiandaa na mitihani ya kuhitimu. Japo wapo watu wazima wamesombelewa na malori kwenda mkutanoni. Suala la wanafunzi ndilo gumzo kwa wananchi wengi wanatafuta wanasheria kuhoji jambo hilo kwa sasa wanafunzi na waalimu wapo mitaani, hivyo tunahoji mgombea Urais ana mamlaka gani hadi afisa elimu awatoe wanafunzi madarasani.
Porojo wakati huu si mahali pake. Ungeokoteza hata picha ya shule yoyote tu angalau kuhalalisha taarifa yako.
acha unafiki
Ujinga at its highest Level anaona huu ni mwaka 47!Wana JF
Nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi leo kwenye mkutano amabao Magufuli alikuwa akihutubia huko Mabizi jijini Mbeya eti kwamba waTanzania tukikosea tukachagua upinzani tutajutia. Nanukuu:
Alisema nchi kama Libya, Tunisia, Iraq na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wananchi wake walilazimisha mabadiliko lakini leo wanajuta.
Msitoe hukumu ya jumla, zipo nchi zilifanya hivyo zinajuta. Libya ya (Hayati Muammar) Gadaffi ulikuwa ukioa unapewa nyumba, unatafutiwa mtaji, maji, elimu na umeme bure lakini wananchi walichoka raha, alisema.
Wakasema anaondoka lakini leo hii hakuna raha na wale vijana waliotaka ukombozi wa haraka ndiyo wa kwanza kuvuka Bahari ya Mediterranean kwenda Ulaya.
Aliwaomba Watanzania wamwamini na kumpigia kura kwa kuwa akiingia Ikulu hatakuwa na deni la kulipa kwa sababu hakupata nafasi ya kugombea urais kwa kuwalipa watu ili wamteue.
My take:
Zili porojo, vitisho na kutia hofu wananchi ya kwamba mambo yatakuwa mabaya tusipoichagua ccm yamepitwa na wakati ni bora ajikite kwenye sera. Sisi sio waDanganyika anymore, tukutane Oktoba.