Hatimaye Mh John Pombe Magufuli apokelewa kwa shangwe na MAELFU ya wakazi wa Mbalizi, Mbeya.
Hata hivyo rais huyo mtarajiwa aliwahakikishia wakazi hao serikali yake itatoa kipaumbele katika kufufua viwanda, ikiwa ni kusaidia kutengeneza ajira nyingi kwa vijana. Aidha Mh Magufuli pia kasisitiza kuboresha miundo mbinu hususani ujenzi wa barabara za kisasa ambazo zitakuwa ni kitovu cha kuinua uchumi wa nchi hii na kuondoa umaskini.
Hata hivo katika mkutano huo zaidi ya wanchama 1000 wa CHADEMA wamerudisha kadi zao na kujiunga rasmi na CCM.
Wanachama hao wapya wameahidi kuachana na porojo, kubuluzwa, hatimaye kuchukua hatua mapema, wamempongeza sana Dr Magufuli kwa utendaji wake uliotukuka.
KAZI NI KAZI TU