Eneo la kwa Mama John Mbeya liligeuka uwanja wa vita kwa muda jioni baada ya kampeni za CCM kumalizika. Mara baada ya msafara wa Magufuli na viongozi wengine wa CCM kuondoka, gari aina ya Land Cruiser lenye machata ya Sugu 2015 lilipita likisindikizwa na vijana waliokuwa wakishangilia.
Mara baada ya hapo kila bajaj au bodaboda iliyokuwa ikikatiza eneo hilo ikiwa na bendera ya CCM ilikuwa ikishambuliwa kwa mawe huku bendera nyingine zikiporwa. Kuna wakati hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya foleni kuzidi na magari kutotembea ambapo kundi la vijana liliifuata bajaj iliyokuwa imepakia watu waliovalia sare za CCM na kuanza kuwafanyia vurugu na mmojawapo alipojaribu kujibizana nao walimkokota kwenye mtaro na kuanza kumpiga. Baada ya muda umati wa watu ulijaa na mawe yalianza kurushwa huku wanawake na watoto waliokuwa wakirejea majumbani wakilizamika kuanza kukimbia kujiokoa na baadhi kuishia kuanguka mitaroni na bodaboda kukosa kosa kuwagonga watu.
Hii imenisikitisha sana, nadhani inabidi ifikie hatua viongozi wa vyama vyote wapige marufuku vurugu za aina hii kuwe na kuvumiliana kila mmoja afanye kampeni bila kubugudhiwa. Kama alivyosema Mbatia kuwa hawatamshambulia mtu au kumsema yeyote vibaya ni muhimu mbegu hii waipandikize kwa wanachama wa matawi yote. Na Magufuli kasema kuwa hatamsema mtu wao pia waihubiri hiyo kwa wanachama wao ili kampeni ziishe kwa amani.
sugu tatizo lake ni bangi mtu na wafuasi wake
Lakini bangi zake ni smart kule bungeni anawanyoosha akili zenu zinazofikiria kwa ile kitu ya kunyeeesugu tatizo lake ni bangi mtu na wafuasi wake
kama ccm wapigwe tuu kwani hakuna njia nyingine wapo ni wachokozi sana hawa magamba
ccm ni mabingwa wa kuteka watu na kungoa kucha
haya yamefanya na kinana ... yule bingwa wa kuua tembo wa tanzania
Hujengi unabomoa. Mungu akusamehe wewe na wote wanaofanana na wewe. Angekuwa ni mke wako amevamiwa na kupigwa ungelihusishaje na pembe za ndovu?
Kwenye taarifa ya habari saa mbili nimeshangaa kuona maandamano ya magufuri kuelekea uwanjani.polisi walipiga marufuku maandamano nchi nzima lakini leo sijaona polisi wakipiga mabomu haya maandamano yasio na kibali
![]()
sugu tatizo lake ni bangi mtu na wafuasi wake
Nimeshangaa nilipoona na kusikia mh.Magufuli alipokuwa akinadi sera huko mbeya alisema:
"Nimeamua kutembea kwa gari ili nione matatizo na changamoto za barabara japo wengine watakuja kwa ndege na helkopta hawawezi kujua changamoto za barabara"
Najiuliza hivi katika miaka 20 aliyohudumu kama waziri miaka 20 amehudumu kama waziri wa Ujenzi sasa leo anasema ndiyo anatembea kwa gari ili kujua changamoto za barabara ataweza kuzijua chanhamoto hizo kwa siku za kampeni wakati ameshindwa kwa miaka 20?
Bungeni alikuwa akitoa takwimu za barabara na kilomita nyingi,kumbe zilikuwa za uongo?alizitoa wapi hizo takwimu wakati hata changamoto hazijui?
Wananchi yeye amesema anashangaa wanafunzi kukaa chini? Anashangaa kuona kina mama wanajifungulia chini? Anashangaa kuona dawa hazionekani na hazipo hospitalini?
Je wananchi nyie hammshangai?
Hivi anashangaa hayo au anaishangaa ccm kuongoza miaka hamsini na nne bila hzo huduma?
Mshangaeni! Chukueni hatua.
Magufuli ageuka kuwa kampeni meneja wa lowasa.
Siku utakapofuatilia ya Lowassa nafikiri utanganyikiwa zaidi.Nimekua nikiifutilia ziara ya magufuli kuanzia jangwani wiki inayomalizika,vijiji kadhaa vya mikoa ya nyanda za juu kusini simbawanga,katavi na hii mbeya na watu wengi wamekua wakimfuata naona ccm Ni kama tayari imeshashinda urais