nuruyamnyonge
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 4,452
- 2,317
Nampa pole sana atapona tu. Mimi ni ukawa lakini kwenye afya tuko pamoja
Machata ni kitu gani ili tuielewe vizuri habari hii, maana nashindwa kuoanisha vurugu na gari la sugu!Eneo la kwa Mama John Mbeya liligeuka uwanja wa vita kwa muda jioni baada ya kampeni za CCM kumalizika. Mara baada ya msafara wa Magufuli na viongozi wengine wa CCM kuondoka, gari aina ya Land Cruiser lenye machata ya Sugu 2015 lilipita likisindikizwa na vijana waliokuwa wakishangilia.
Mara baada ya hapo kila bajaj au bodaboda iliyokuwa ikikatiza eneo hilo ikiwa na bendera ya CCM ilikuwa ikishambuliwa kwa mawe huku bendera nyingine zikiporwa. Kuna wakati hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya foleni kuzidi na magari kutotembea ambapo kundi la vijana liliifuata bajaj iliyokuwa imepakia watu waliovalia sare za CCM na kuanza kuwafanyia vurugu na mmojawapo alipojaribu kujibizana nao walimkokota kwenye mtaro na kuanza kumpiga. Baada ya muda umati wa watu ulijaa na mawe yalianza kurushwa huku wanawake na watoto waliokuwa wakirejea majumbani wakilizamika kuanza kukimbia kujiokoa na baadhi kuishia kuanguka mitaroni na bodaboda kukosa kosa kuwagonga watu.
Hii imenisikitisha sana, nadhani inabidi ifikie hatua viongozi wa vyama vyote wapige marufuku vurugu za aina hii kuwe na kuvumiliana kila mmoja afanye kampeni bila kubugudhiwa. Kama alivyosema Mbatia kuwa hawatamshambulia mtu au kumsema yeyote vibaya ni muhimu mbegu hii waipandikize kwa wanachama wa matawi yote. Na Magufuli kasema kuwa hatamsema mtu wao pia waihubiri hiyo kwa wanachama wao ili kampeni ziishe kwa amani.
kama ccm wapigwe tuu kwani hakuna njia nyingine wapo ni wachokozi sana hawa magamba
ni kweli anafaa kwa kukurupukamagufuli anafaaa sana lowasa kaa pemben
Nampa pole sana atapona tu. Mimi ni ukawa lakini kwenye afya tuko pamoja
Nampa pole sana atapona tu. Mimi ni ukawa lakini kwenye afya tuko pamoja
sugu tatizo lake ni bangi mtu na wafuasi wake
Nimeshangaa nilipoona na kusikia mh.Magufuli alipokuwa akinadi sera huko mbeya alisema:
"Nimeamua kutembea kwa gari ili nione matatizo na changamoto za barabara japo wengine watakuja kwa ndege na helkopta hawawezi kujua changamoto za barabara"
Najiuliza hivi katika miaka 20 aliyohudumu kama waziri miaka 20 amehudumu kama waziri wa Ujenzi sasa leo anasema ndiyo anatembea kwa gari ili kujua changamoto za barabara ataweza kuzijua chanhamoto hizo kwa siku za kampeni wakati ameshindwa kwa miaka 20?
Bungeni alikuwa akitoa takwimu za barabara na kilomita nyingi,kumbe zilikuwa za uongo?alizitoa wapi hizo takwimu wakati hata changamoto hazijui?
Wananchi yeye amesema anashangaa wanafunzi kukaa chini? Anashangaa kuona kina mama wanajifungulia chini? Anashangaa kuona dawa hazionekani na hazipo hospitalini?
Je wananchi nyie hammshangai?
Hivi anashangaa hayo au anaishangaa ccm kuongoza miaka hamsini na nne bila hzo huduma?
Mshangaeni! Chukueni hatua.
MAGUFULI AUMBUKA
Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ameishia na sauti ghafla hali iliyolazimu mkutano wa kampeni kufungwa pasipo mgombea kumaliza kunadi ilani ya chama.
Magufuli amepatwa na balaa hilo leo hii akiwa mkoani Mbeya hali iliyozua hofu na sintofahamu nyingi juu ya afya ya mgombea huyo wa CCM.
Magufuli ambaye alitakiwa kuongea na waendesha boda boda mara ya mkutano huo kuisha ameishia kuwapungia mkono boda boda hao na juu ya tatizo la afya mgogoro uliomkumba.
Hata hivyo habari zilizotufikia hivi punde zinasema Magufuli amelazwa katika hospitali ya mkoa kwa kile kinachosemekana mapigo yake ya moyo hayapo sawa sawa.
Ikumbukwe moyo wa magufuli unafanya kazi kwa kifaa cha kuchaji kinacho rekebisha mapigo ya moyo kiitwacho "Pacemaker" ambacho kipo mwilini mwake.
Hii ni mara ya pili kupatwa na tatizo la kiafya tangu aanze kampeni za urais. Mara ya kwanza moyo ulileta shida akiwa mkoani Katavi hali iliyopelekea kushindwa kuhutubia katika mkutano mmoja wa hadhara na hivyo kuishia kuwapungia mkono watu waliojitokeza kumsikiliza.
Tatizo hili la moyo linampa wakati mgumu Dk. Magufuli nyakati hizi za kampeni.
sijaona la ajabu pale na bado aliongea sana tu , acha tumubiri Rais Mamvi katika ubora wake wa kuzunguka Tanzania