Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

faiza foxy hii habari uje uthibitishe maana hawa ukawa wamezidi sasa
 
Last edited by a moderator:
WASIKUUMIZE KICHWA HAYA NDIO MAJIBU

Swali: Alikuwa wapi siku zote asipande daladala?
Jibu: Alikuwa CCM

Swali: Kwa nini siku zote asinywe chai kwa mama ntilie?
Jibu: Njaa haikumwuma.

Swali: Tutampaje urais mtu anaumwa?
Jibu: Kama watu hawatakiwi kuugua hospitali zimejengwa kwa kazi gani?

Swali: Mtu mwenyewe si amekuja kwa sababu anataka tu urais?
Jibu: Ulitaka aje anapotaka urefarii wa Simba na Yanga?

Swali: Kwa nini amegonjea akatwe ndo aje?
Jibu: Wewe huwa ukikosa kazi mahali huwa unajifungia chumbani na mpenzi wako ama unatafuta kazi kwingine?

Swali: Kwa hiyo nawe utakwenda Jangwani?
Jibu: Nisipoenda mimi mawe yatakwenda.

LOWASAAAAAAAAAAAA!
 
Wanafuata pesa. Sio ukombozi. Hatuwahitaji!

Mkuu, mkombozi wako ni wewe mwenyewe. Unakuta kidume kina familia lakini kiko miguu juu kinasubiri mwanaume mwingine aje akikomboe. Mtu anacheza pool saa sita mchana au yuko JF siku nzima ana comment kila post, naye anasubiri mwanaume mwingine toka Ukawa au Ccm aje amkomboe. Utopia...
 

ccm katika ubora wa kuchakachua mmechapisha card za cdm alaf mnatuma makada wenu wakazisalimishe hahahhah imekula kwenu
 
Kwani karudi lini Tanzania alivyo ondaka kwani Tanganyika ilikuwaje mbona amekuwa hodari wa kushangaa ni bora awaache wanaojua kwanini watoto shuleni wanakaa chini,wakina mama wanaojifungulia sakafuni hakuna viwanda na mazagazaga yote shida kila idara wanayojua atatizo wapo tuwaoe nafasi wafanye kazi wnaoshagaa tuachane nao
 
Mkuu huns jipya thread zako za kutengeneza na kutudanganya humpati mtu
 
Sugu kiboko yake inatia timu kesho hatumwi m2 dukani, jembe linakubalika kila kona sasa zamu ya monduli weweeee......ukawa mtakufa kwa presha
 
Eneo la kwa Mama John Mbeya liligeuka uwanja wa vita kwa muda jioni baada ya kampeni za CCM kumalizika. Mara baada ya msafara wa Magufuli na viongozi wengine wa CCM kuondoka, gari aina ya Land Cruiser lenye machata ya Sugu 2015 lilipita likisindikizwa na vijana waliokuwa wakishangilia.

Mara baada ya hapo kila bajaj au bodaboda iliyokuwa ikikatiza eneo hilo ikiwa na bendera ya CCM ilikuwa ikishambuliwa kwa mawe huku bendera nyingine zikiporwa. Kuna wakati hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya foleni kuzidi na magari kutotembea ambapo kundi la vijana liliifuata bajaj iliyokuwa imepakia watu waliovalia sare za CCM na kuanza kuwafanyia vurugu na mmojawapo alipojaribu kujibizana nao walimkokota kwenye mtaro na kuanza kumpiga. Baada ya muda umati wa watu ulijaa na mawe yalianza kurushwa huku wanawake na watoto waliokuwa wakirejea majumbani wakilizamika kuanza kukimbia kujiokoa na baadhi kuishia kuanguka mitaroni na bodaboda kukosa kosa kuwagonga watu.


Hii imenisikitisha sana, nadhani inabidi ifikie hatua viongozi wa vyama vyote wapige marufuku vurugu za aina hii kuwe na kuvumiliana kila mmoja afanye kampeni bila kubugudhiwa. Kama alivyosema Mbatia kuwa hawatamshambulia mtu au kumsema yeyote vibaya ni muhimu mbegu hii waipandikize kwa wanachama wa matawi yote. Na Magufuli kasema kuwa hatamsema mtu wao pia waihubiri hiyo kwa wanachama wao ili kampeni ziishe kwa amani.
 
Kwenye taarifa ya habari saa mbili nimeshangaa kuona maandamano ya magufuri kuelekea uwanjani.polisi walipiga marufuku maandamano nchi nzima lakini leo sijaona polisi wakipiga mabomu haya maandamano yasio na kibali
 
Hayakuwa maandamano...bali watu walikuwa wanatembea kuelekea mkutanoni....
 
ccm ni mabingwa wa kuteka watu na kungoa kucha

haya yamefanya na kinana ... yule bingwa wa kuua tembo wa tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…