Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Kusema kampeni za CCM ni ngumu ni vichekesho. Rais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%

Rafiki zetu wa CHADEMA mtaula wa chuya huu mwaka hampati hata mbunge.
Binti ulipotelea wapi,au mpini ulikukolea ukapasahau hapa?
 
Mambo mengine ni ya ajabu sana. Ukiangalia kwenye ratiba ya kampeni kwa mgombea wa ccm, imeonesha siku atakapo pumzika. Pia niwaambie cdm. Jembe litaendelea kuikanyaga nchi nzima kwa gari.
 
Hana woga, muulize Prof. Kabudi kutwa kucha kueleza balozi UK na US uchaguzi utakuwa huru na haki. Ingia control room utajua kunachoendelea hapa Tanzania.
 
Kumbuka uchaguzi ni mwezi ujao tena mwishoni na safari hii kampeni inafanywa na viongozi wakubwa wote katika mikoa tofauti tofauti.
Hakuna kiongozi yeyote wa ccm mstaafu na hata wa sasa mwenye ushawishi kwa wananchi , watu wametekwa na kuuawa hakuna aliyenyanyua mdomo kupinga , leo hii watasema nini mbele ya wananchi wanaopoteza ndugu zao kila uchao kwa kutekwa
 
Mambo mengine ni ya ajabu sana. Ukiangalia kwenye ratiba ya kampeni kwa mgombea wa ccm, imeonesha siku atakapo pumzika. Pia niwaambie cdm. Jembe litaendelea kuikanyaga nchi nzima kwa gari.
CCM wanafanya kampeni za kisayansi😁😁😁 kampeni zenye matokeo chanya.... na sio kampeni za kulalamika kuonewa kutwa na kutishana
 
Hahaha kampeni miaka mitano bado hueleweki, inakatisha tamaa sana.

2015 mpaka leo 2020 kampeni na hueleweki sio kupumzika angeacha kabisa.
 
Kuna ubaya gani mtu kupumzika? Ukijadili suala hili bila mwegemeo wa kisiasa utaona hakuna tatizo mtu kuamua kupumzika. Safari ya Dodoma mpaka musoma, Mwanza Geita wakati huo anaongea kula mahali Kuna shida gani hapo mtu akipumzika. Badala ya kujadili issue ya mtu kupumzika, ambayo ni kawaida,tungepiga kelele humu mitandoni jinsi ambavyo mawakala la tume ya uchaguzi( wakurugenzi) walivyoharibu uchaguzi huu kwa kuengua wagombea. Inaumiza kuona uchaguzi unageuka kuwa uteuzi. Inawezekanaje mnaenda kupiga kura kwenye kinachoitwa uchaguzi huku tayari almost theluthi ya madiwani ameshapita bila kupingwa? Kuna wabunge wameshapita pia. Hii mentality ya kuona Mambo mazuri katika wapési wa kifikra itatusaidia? Kujadili mtu kakata pumzi au napumzika kwangu Mimi ni dhana ya kukupa Mambo madogo kwa gharama ya Mambo muhimu. Let's change.
 
Kusema kampeni za CCM ni ngumu ni vichekesho. Rais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%

Rafiki zetu wa CHADEMA mtaula wa chuya huu mwaka hampati hata mbunge.
Mhh ulipotea
Karibu tena.,

Ulikula ban ama?.
 
Wanafunzi ndio wapiga kura wa kesho, tatizo CHADEMA mmjezana wengi wenye fikara zisizo ona mbali
Kaka sijui Dada, vipi kuhusu malipo yetu ya leo huko? Tunapata ugumu sana kutetea chama chetu huku tukiwa na njaa ujue.
 

Attachments

  • Lumumba Buku 7.jpg
    20.8 KB · Views: 1
Mwacheni Mh Rais apumzike jamani kwanza amehakikishiwa na wapambe nuksi kwamba mwaka huu anashinda kwa asilimia 99.9.
 
Madukuduku ya watu wanajibiwa na rais kwa muda wote anaokuwa ikulu.

Msafara unaposimama njiani rais huongea na watu na kuwauliza shida zao,anachokifahamu katika vikao vya aina hiyo ni zaidi ya mbwembwe za midahalo.

Kwenye mdahalo ndio sehemu sahihi ya kuulizwa na kujibu kwa utaratibu mzuri. Huko barabarani anakutana na watu waliopangwa kumuuliza, na wale wote ambao hawajapangwa wakimuuliza huwa anawajibu kwa kejeli na dharau kubwa. Huwa tunaona anachokifanya wala hatuhadithiwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…