Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
CCM imefanyiwa ukatili sana na watanzania yaani miaka mitano yote usingejua kama kuna upinzani. Wananchi wamepiga U-turn hadi Magufuli haamini
Nipo Kijijini huku, aisee wananchi wa kawaida tu wameichukia ccm na magufuli mpaka basi!! Hawaoni umuhimu wowote ule wa kununua bombardier!
Kitendo cha mgombea wao kuondoa mzunguko wa fedha mtaani, kuwadhulumu wafanyakazi stahiki zao, na ugumu wa maisha kwa ujumla! Vimempunguzia sana credit, maana hata wale "wanyonge" aliojinasibu kuwapigania, nao hawamuungi mkono kwa lolote.
Nina imani kungekuwa na uchaguzi huru na wa haki mwaka huu wa 2020, hakika Magufuli angepata kura chini ya 30%!!
Kimsingi Mzee hakubaliki kwa sababu ya kiburi chake, dharau zake, majivuno yake, hulka yake ya kujilimbikizia utukufu na sifa, tabia yake ya ukatili, ubaguzi kwa wapinzani wake, na kuwakumbatia wanafiki, nk.