Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Nashindwa kuelewa weredi wa wachangiaji wa hii post, hivi ni kweli kwamba nyote hamjapitia ratiba ya kampeni ya wagombea wa kiti cha urais?

Tarehe 9 anafanya kampeni Chato, baada ya hapo anapumzika siku tano, kisha ataendelea tarehe 15 huko Bukoba.
Kwa akiamua kuwaambia tume waweke ratiba za mapumziko anashindwa?.... Magufuli si ndiye anayeteua tume na kuiamrisha atakavyo?
 
Hao hata muda wa kujiandikisha hawana
Wakati mnawalazimasha vijana kutumia kadi za mpiga kura kuwa kitambulisho, kupatia dhamana polisi nk ndio mlipo wapa uwezo wa kuwachinja sasa.
Hizo kadi zimegeuka kisu cha kukata shingo ya jiwe 28/10
 
Katika hali inayoashiri mikikimiki ya Campaign, Mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi amepumzika kufanya kampeni.

Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa kampeni za Mwaka huu zimekuwa siyo nyepesi kama zilivyodhaniwa.

Magufuli ambaye mwaka 2015 alizunguuka kwa barabara nchi nzima, inaonekana dhahiri kuwa safari hii hawezi kuifikia rekodi ya mwaka huo. Safari hii inaonekana ameweka nguvu zaidi katika mikoa ya ukanda wa ziwa huku Wapiga kampeni wengine wakienda kanda nyingine.

Hata hivyo wapiga kampeni wake yaani Mama Samia na Kassim Majaliwa hawana mvuto mkubwa wa kisiasa wa kuweza kuchangia kura za maana kwa Magufuli.

Wakati huohuo mgombea wa Chadema Tundu Lissu ambaye ana faida ya kujinadi mapema makhsusi kwa ajili ya uchaguzi huu kwa kisingizio cha "kutafuta wadhamini" ameendelea kuchanja mbuga kwenye ngazi ya jimbo kwa jimbo baada ya kumaliza kupiga show kwenye ngazi ya kanda kwa kanda.

Sambamba na ngazi ya Jimbo kwa jimbo, Chadema watafanya mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanamng'oa Magufuli madarakani.

Bado haijajulikana kama kupumzika huku kwa mgombea wa CCM ni routine ya kawaida tu au uchovu au afya, tunangoja chama cha mapinduzi kitujuze zaidi.

View attachment 1567050
Kitu spana mkononi hiki kiburi cha bure tu
 
Kwa akiamua kuwaambia tume waweke ratiba za mapumziko anashindwa?.... Magufuli si ndiye anayeteua tume na kuiamrisha atakavyo?

Maana yangu sio kwamba mapumziko kapangiwa na tume, ninachopinga ni huku kusema kwamba ameamua kupumzika kwasababu ya kuchoka ama kampeni kumuelemea.

Kama una ratiba yako inasema jumamosi hauendi kazini, halafu ikatokea ijumaa ukapewa kazi nzito sana na Boss, kesho yake usipoenda kazini hatutasema haujaenda kwasababu ya kazi ya jana, bali ni kwasababu ratiba yako ilikutaka hivyo.

CCM walipanga ratiba yao hivyo kwamba akifika Chato atapumzika kwanza na familia yake, kutembelea mizimu ya kwao na kama ana imani za kiasili kwenda kwa waganga wake kwa wiki hiyo moja, ni kama ambavyo Mheshimiwa Lisu alipumzika siku mbili baada ya kutoka Zanzibari
 
Walienda kuhakiki taarfa ? Si mlijifanya mmegoma ? Kutokana na serkali za mitaa [emoji3][emoji3]
Kwani wale milioni 29 mliosema wamejiandikisha kumbe kuna wengine hawamo kwa vile hawajahakiki?
Hiyo maana yake NEC inao wapiga kura pengine milioni 40 katika RAIA milioni 52
 
Hahaha Mkuu tayari Ccm ina wapiga kura milion 19
Kampeni za Magufuli zimevuta wapi kura milion tano wasio kuwa na chama, jumla milion 24

Sasa hivi tunawatafuta milion tano waliobaki
Nilikuwa nakudharau kidogo ila sasa nakudharau sana!!
Kwa akili ya kawaida tu unawezaje kuja kusema fulani ana wapiga kura kadhaa wakati kura ni siri???
 
Hujui Ccm inawapiga kura milion 19? Hizo ni kura za Rais Magufuli

Mikutano ya Rais Magufuli imevuta wapiga kura milion tano jumla ni kura milion 24

Kwahiyo sasa hivi Rais Magufuli anatafuta kura milion tatu ili ashinde kwa 97%
Jibu swali, how comes unatoa takwimu za wapigakura wakati kura ni siri???
 
Na wewe nyumbu wa kinondoni ufipa, shwine wewe
Hahahaaa...... Tundu Lissu alishasema hakuna aliye salama akasema zaidi kua hata kinana na makamba hawako salama na hakuna aliyekanusha😄😄😄😄

Tundu Lissu kaendelea kutukumbusha zaidi aliposema kila mmoja ana September 7 yake😲😲
 
Tume huru ikija bado litatafutwa lingine la kulalamikia.

Kwa hiyo tume huru hapana ili walalamike kwa hili ambalo ni wazi mno kwa mtu yeyote kuona kuwa siyo siri bali ni ukweli ulio wazi Kwamba CCM ni dhulumati.

Umeeleweka mkuu.
 
Wakubwa! Hivi mmeangalia ratiba ya kampeni? Mpaka mnakuja ajenda, kila mgombea ana muda wa kupumzika hata TL alipumzika siku 2 tarehe 8&9 hii ni kutokana na muongozo wa ratiba ya NEC.
We huwajui misukule ya lissu? Kazi yao kuropoka ropoka ovyo kama wamerukwa na akili vile! Kila jambo la magu kwao ni hoja ya kuifungulia uzi! Mpaka oct 28 watakuwa na hali mbaya sana hawa
 
Rais JPM Leo Yuko Chato akikutana na mheshimiwa Museveni kusaini makubaliano ya ujenzi wa bomba.
Kuna kazi Za rais na kazi za mgombea, ukiona amepumzika kampeni ujue anafanya kazi Za rais wala usipanic.
Alipogombea mwaka 2015 alikua mgombea tu sio rais alikua na muda mwingi wa kufanya kampeni bila kuingiliwa na kazi Za rais.
Naona sheria zetu zibadilishwe ili rais akiwa ni mgombea akabidhi kwa mwingine majukumu ya rais awe na muda wa kutosha wa kampeni na kuondoa mgongano wa maslahi.
Kuna muda unashindwa kujua Kama nimgombea au ni rais.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Pumzi imekata! Lissu hafai aisee!! Alijua mwaka huu atateremka tu mlima kitonga! Kisa amenunua ndege na kujenga flyovers. Alichokutana nacho, hatokuja akisahau kamwe.

Hili ndilo somo sahihi la kudhani maendeleo ni VITU pekee!
Angalia TBC blaza shida mnashindanisha Rais na mtu ambae bado anatafuta kazi.....mwenzie leo ana majukumu ya kitaifa huyo mwengine aendelee kupuyanga tu atembeze CV ili apate kazi anayoisaka kwa hamu
 
Back
Top Bottom