Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

CCM imefanyiwa ukatili sana na watanzania yaani miaka mitano yote usingejua kama kuna upinzani. Wananchi wamepiga U-turn hadi Magufuli haamini

Nipo Kijijini huku, aisee wananchi wa kawaida tu wameichukia ccm na magufuli mpaka basi!! Hawaoni umuhimu wowote ule wa kununua bombardier!

Kitendo cha mgombea wao kuondoa mzunguko wa fedha mtaani, kuwadhulumu wafanyakazi stahiki zao, na ugumu wa maisha kwa ujumla! Vimempunguzia sana credit, maana hata wale "wanyonge" aliojinasibu kuwapigania, nao hawamuungi mkono kwa lolote.

Nina imani kungekuwa na uchaguzi huru na wa haki mwaka huu wa 2020, hakika Magufuli angepata kura chini ya 30%!!

Kimsingi Mzee hakubaliki kwa sababu ya kiburi chake, dharau zake, majivuno yake, hulka yake ya kujilimbikizia utukufu na sifa, tabia yake ya ukatili, ubaguzi kwa wapinzani wake, na kuwakumbatia wanafiki, nk.
 
Alienda na usukuma wake ikulu. Hayo ndio matokeo yake
 
Lissu ana haki ya kupumzika maana alipiga kazi nzito
Sasa huyu vikampeni vinne ulimi nje!

Bora aachane na biashara za urais akapumzike zake Chato aache wrnye nguvu wapige kazi ya kurejesha haki nchini
Hahaaaaaa............. 😁 😛
 
Lissu amerudi na mabilion aliyopewa na Wazungu ili kuja kuharibu amani ya Nchi yetu

Hapo kuwachangisha ni kuwapiga chenga asishtukiwe kwa kutakatisha pesa chafu

Mfa maji haachi kutapatapa. Ngoja Lissu aendelee kuwanyoosha maana hakuna namna. Huyo ndiye kiboko ya Magufuli. Na kwa ule ujinga wenu ulioshindwa wa mwaka 2017, hakika awamu hii atawanyoosha kweli kweli!!

Mtamfanya nini? Kumpiga risasi tena hamuwezi, kumfunga kwa hila hamuwezi!! Unadhani ni kwa nini!! Wale marafiki zenu Mabeberu wanawaangalia kwa 24 hours.
 
Na kauli za Polepole kuwa Chadema haina hospitali haiwezi kutoa bima ya afya kwa watu wote ni kauli chakavu sana. Kwani hospitali ni za CCM?
Polepole Hana akili nasijui aliipataje hiyo nafasi , yaani hakuna hata siku moja aliyo pata kuongea Jambo la maana.
 
Wadau bwana 😂 eti amekata moto,, mwacheni avute pumzi aje kuchafua kusini na kaskazini kisha amalize pwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…