Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Nimefurahi sana kitendo cha Rais Magufuli kuamua kumkaribisha mgeni wake Rais wa Burundi, bwana Evariste Ndayishimie mkoani Kigoma.

Na sisi leo tumeonja ladha ya kuwa makao makuu ya nchi kwa muda. Ungeweza kumkaribisha akaja Dodoma au Dar.

Leo kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimeona uwanja wa Ziwa Tanganyika ukiwekwa zuria jekundu.

Kama ulivyosema kama unaipenda Kigoma umedhihirisha maneno yako kwa vitendo.

Wiki hii imekuwa ya kihistoria sana mkoani Kigoma. Inasemekana mnaweza kuwa Kigoma wewe na mpinzani Tundu Lissu. Hii yote imenifurahisha.

Zitto nae najua atajiunga nanyi kwenye mapokezi hayo ya ugeni.

Asante sana Magufuli kwa Kigoma
 
Uwanja umejaa vumbi hatari
Tunafeli wapi kutunza viwanja ....
 
Sasa nani asiyetaka kwenda kumuona Alikiba tena bure kabisa!???
 
Kweli kaweka historia ya kubebewa wasikilizaji toka wilaya zote na mikoa ya jirani.
Tusubiri tuone Lissu atawezaje kuwaaminisha yeye hatumii somba somba bali mioyo ya watu ina mfuata..
 
Hii ni mbinu ya Magufuli kuchota fedha hazina za kampeni zake kwa kisingizio cha kuwa katika ziara ya kiserikali. Msafara wake wote utatumia fedha za serikali kwa mafuta ya magari na posho kwa wote alioambatana nao!
 
Hivi Magufuli hajui Kiswahili au anafanya makusudi. Anapouliza ni wangapi watanipa, huku mbele mtanipa? Na kule nyuma je?
 
Ule ni ujumbe kuwa wana Kigoma wanataka maendeleo na siasa za kijinga za kupinga kila jambo, kususia, kudanganya, kuchochea na nk.
Mkutano wa ufunguzi wa kampeni wa Zitto, ulitofautina kidogo na wa Jana wa Magufuli. Na hapo Zitto hakuwa na wasanii. Kwa kigoma magu ameangukia pua labda kwa wizi sawa hapo atapita Ila hawezi.
 
Angeenda bila fiesta hapo tungekuwa na cha Kujadili,watu wameenda kuona wasanii tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…