Mkuu
kibaravumba , naunga mkono hoja, haswa ukizingatia ni kwa miaka mingi, Watanzania tumekuwa tukimlilia Mungu, atupe kiongozi wa aina fulani ili kuliokoa taifa letu Tanzania lililofanywa shamba la bibi kwa muda mrefu, kisha Mungu akajibu maombi, akatupatia kiongozi chaguo la Mungu, hivyo ndicho hicho hicho anachokwenda kutenda hiyo tarehe 28 October
P
P ktk ubora wako wa Sasa!
Hebu Soma hii then unipe maoni!
Juzi nilikuwa kijijini fulani Mikoa ya Pwsni..
Nikutana na mama mmoja Nesi vyeti feki aliyetumbuliwa ..Ameishi katka Kijiji alichofanyia kazi kwa miaka 30!
Nilielezwa kuwa kwa miaka yote 30 yeye pale amekuwa Ni Daktar Bingwa wa Moyo,magonjwa ya nje na ndani! Mtaalamu wa upasuaji,gyno, mtaalamu wa watoto,Mfamasia ,mkunga,mhudumu wa Afya ,mtaalamu wa Lishe na Afisa Ustawi wa Jamii....kiufupi yeye Ni Kama Mganga Mkuu wa Serikali ya Kijiji...si ajabu Waziri wa Afya!
Leo Bibi huyu ametumbuliwa kwa kosa la kukosa cheti Cha Form Four.Alinieleza kuwa alisoma kwa shida kwao Ukerewe ,lakini hkufnya vizuri mitihani akatafura cheti Cha mtu akaenda kusoma cheti Cha Nurse!
Bahati nzuri anatambua kuwa kutumia cheti Cha mtu Ni kosa!
Kwa Nini nimekuletea simulizi hii!
Ni like nilichokisikia kutoka kwa wanakijiji kumhusu Mama huyu!
Wao hawaelewi kuwa huyu Mtaalamu wao Ni feki...wanasema wanamuona Kama Mungu wao kwa Utumishi ulitukuka alio utoa pale kijijini kwa miaka 30!
Wanasema haijawahi kutokea...watumishi wenzake walikuwa wakiletwa pale wanaacha kazi !
Alikuwa anafanya kazi kuanzia saa 2 Hadi saa 11,Jumapili ana jumamosi alikuwa available!
Kijiji pale kina makumi ya watoto wanaitwa jina lake Kama hesshima yake kwa kazi ya ukunga!
Baada ya kubaini kuwa mama yule kafukuzwa kazi Wazee wa Kijiji walimwambie isiwe shida wewe umetumia maisha yako yote hapa ukituhudumia ,ulikuws huwezi kwenda shamba Wala biashara:
Kwa kifupi Wazee waluchangishana mabati kadhaa,vijana wajampa tofali ...mafundi wajasimsmisha nyumba ya Daktari mtukuks wa Kijiji!
Cha ajabu wamemjengea nyumba si mbali na Zahanati! ambayo Sasa haina Mtumishi!🤭🤭🤭 Baada ya watumishi 2 walioletwa kuacha kazi!
Wale wanakijiji wanamuona mtu aliyemtumbua kazi Daktari wao kuwa ni Hamnazo!!
Sasa kuwashawishi watu Hawa kuwa ...Kuna chaguo la Mungu......!