Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Ukweli lazima usemwe wana CCM wengi ndani ya chama wapo kinafiki,wengi wanamchukia jiwe moyoni hawawezi kuonyesha hadharani ebu imagine Mtendaji Mkuu wa chama alipishana kauli na jiwe na kutaka kujiuzulu-in membe voice sasa katika hali hii huyu mtendaji mkuu amekaa ili kutoleta aibu.

Makamu wa Jiwe-mama samia kulikuwa na rumours kuwa alitaka kujiuzuru-ni dhahiri akibaki ili kulinda heshima ya chama na serikali.

Sasa hao ni top management ndani ya serikali na chama kwa sasa wapo kimwili ila mioyo yao imisha jeuriwa,vipi common people ambao hawakidhi mahitaji yao ya kimaisha???

Magu hata ikitokea akishinda inabidi abadilishe msimamo wake na mtazamo wake kuhusu Taifa hili.
 
Umenena vyema sana mkuu! Lakini ngoja Malalamiko FC waje!!
 
Haya tuambie wewe waliojiandikisha ni wangapi kama unakataa takwimu za NEC?
 
Milioni 17 za ccm umezipata wapi (source)?
Kweli mkuu umeuliza swali zuri ,kwamba 2015 mpaka 2020 wameongezea wanachama ml 10 ? Alafu mtoa mada pamoja na takwim zake ila amesahau kwamba 2015 jpm alikua angalau na mvuto kwa wapiga Kura japo hakumzidi lowassa kwa mvuto ila hata Kura mil 8 sidhani Kama zilifika Sasa Kama hazikufika kipindi kile vipi Leo ambapao unaonesha wazi mvuto kwa jpm kwa wapiga Kura upo chini Sana ,
Wenda wengi wapenzi na wafuasi wa ccm hawataki habari Kama hii lakini ndo ukweli wenyewe.
Sawa Kila chama kina njia ya kufanya kampeni,na ccm wanafanya kampeni na wanamziki ,Sina shida na hilo ,shida hapa ni ccm kupata data kamili kwamba wanakubalika wao Kama chama au Basi tu watu wapo kwa kimuangali zuchu,hivyo ukitaka Hali halisi ya ccm wapige mkutano mmoja bala wasanii,kwa Sasa aina ya kampeni wanayofanya ni ngum kuelewa Kama watapata Kura m3 au zaidi ,so Kama Wana ubavu ili tuwapime vizur ebu pigeni mkutano mmoja katika wilaya moja ila wasisombe watu
 
it true for physical sciences but not so for political science.
 
Kwahiyo CHADEMA NA ACT tafadhali msiondoe agenda ya NGUVU YA UMMA mezani. Lissu atashinda si chini ya 70%. Mnadhani tume ya Daktari Mahera kwa vyovyote itamtangaza????? No!!!! Never!!! So what!!!!???
 
Haya tuambie wewe waliojiandikisha ni wangapi kama unakataa takwimu za NEC?

Sina idadi kamili maana sina means za kujua idadi kamili, lakini hakuna uwezekano wowote nusu ya watanzania wote kuwa wamejiandikisha kwenye daftari la wapiga kura. Sana sana wengi ni wale wenye vitambulisho vya 2015, na wachache mno wapya. Hardly hawafiki 25m.
 
Kama unapuuza nguvu ya Mama Samia, Makamu wa Rais, je, Majaliwa, Waziri Mkuu? Pamoja na kejeli zake Lissu hajathubutu kuwataja. Uadilifu wao na nguvu yao kisiasa, 2025, upinzani hauna pa kutokea.
 
Unafikiri utaletewa mikataba hapa JF?
Mikataba inabidi iwekwe wazi ili wananchi popote walipo waweze kui-access,ndo ilivyo hivo. Sasa unafikiri ikishakuwa released kwa public itashindikana kupatikana humu?
BTW hujaelewa content yangu hapo mwanzo ndo mana umedakia.
 
Bado natafakari njia ambayo Magufuli ataitumia kushinda uchaguzi huu sioni ni ipi.

Mbinu zote za NEC zinamulikwa 24/7 wako monitored.

Mbinu zote za baadhi ya police wanaotaka kusaliti umma ziko under control.

Mbinu zote za kunakili namba za vitambulisho hazotaruhusiwa kufanya kazi siku ya uchaguzi na mawakala wa upinzani watakaokuwa kila kituo na watakuwa monitored.

Wazee ndani ya system wamegoma kutumika kubariki uvunjifu wa Katiba na sheria.

Wazee ndani ya chama wamesusa kabisa hawataki lawama

Jeshi siku zote ni la Wananchi na kamwe haliwezi kuwasaliti watanzania.

Umoja wa mataifa wanataka uchaguzi huru na haki.

Marekani anaunguruma kila uchao anataka uchaguzi huru na haki

Umoja wa ulaya wanataka uchaguzi huru na haki.

Sasa najiuliza anachomokea wapi huyu mtu uchaguzi huu?

Sioni mwisho mwema wa CCM ya Magufuli Polepole na Bashiru.
 
Kazi kubwa aliyofanya kwa miaka minne na ushehe.
Ujenzi wa miundombinu ya barabara
SGR
ununuzi wa ndege
elimu bure
ujenzi wa vituo vya afya
kuwashughulikia mafisadi
ujenzi wa meli mpya
treni kuabza kazi baada ya miaka 30
Tembo kuongezeka
uboreshaji wa mapato
kupunguza vifo vya albino na vikongwe
ajali za mabasi kupungua
ununuzi wa ndege
TTCL kurejea
pato la madini kukua na udhibiti wa rasilimali
Kupambana na covid 19
kuondoa kero kwa wamachinga
kuondia kero ya bodi ya mikopo vyuo vikuu
elimu bure
n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…