Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Nimetafakari kwa kina kuhusu uchaguzi wa tarehe 28.10.2020 kwa maoni yangu ni bora JPM achaguliwe tena ili apate fursa ya kumalizia miradi iliyopo.

Iwapo kuna mapungufu yoyote naamini amesikia kilio cha wananchi atarekebisha kasoro hizo kwa vile uongozi ni pamoja na mafanikio na changamoto.
 
Siwezi kumuunga mkono mgombea anayewatisha wananchi!Mgombea anayeona kutekeleza maendeleo ni hisani yake utafikiri pesa anatoa mfukoni kwake!Hii ni dharau kubwa kwa wapiga kura!
 
Vipi kama hatutamchagua, utatufanya nini? HATUMTAKI. Mchague mwenyewe.
 
Wewe ukiacha wengine watamchagua. Muhimu kura zitimie na kujaa by 80%

Hata hao wengine nao wana akili timamu kama mimi, hivyo hawatajisumbua kuchagua dikteta. Watachagua mabadiliko bila shaka yoyote ile.

Ni kupitia tu Necccm na Policcm ndiyo hiyo 80% itapatikana. Ila siyo kwa kupitia sanduku halali la kura.
 
Kakwambia nani kuwa wakandarasi wanaishiwaga miradi?

SGR ikifika Rwanda, anahamia bomba la gesi Mtwara hadi Uganda, halafu maji toka Ziwa Victoria hadi Dodoma nakadhalika nakadhali nakadhalika
 
Magufuli sio 'contractor' wa miradi na wala sio 'consultant', na pesa ya kumalizia miradi ni kodi zetu! ... SEMA JINGINE!
😅
👊 ✌✌✌💥
 


Wakulima wa Tanzania wanasema Magufuli amewafanyia makubwa

Wanasema kura zote wanazipeleka kwa Rais Magufuli
 
Inamaama hao wakulima wameona manufaa ya reli tayari?Mbona hata haijakamilika?
[emoji16][emoji16],hao watakuwa wakulima wa Lumumba wa nyuma ya keyboard!
Kuna wengine walipongeza kwa kuletewa Reli ya kiwango cha Lami.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…