RAISI MAGUFULI AMALIZA HOJA ZA WAPINZANI
Na Mackdeo Shilinde
Ndugu Wana jukwaa la siasa wenzangu nawasalimu katika jina la Bwana wetu Yesu kristo wa Nazareth na mtume Muhammad (SAW)
Wana jukwaa wenzangu kwa Sasa ukiangalia hali ya kampeni zinazoendelea,wazi kabisa utaona kuishiwa kwa hoja kwa wapinzani.
Kuingia kwa hi ungwe ya mwisho kwa maana ya siku hizi 12 zilizo baki ,utagundua wapinzani wanachokifanya Ni kutembea na MAGUFULI,Maana yake Nini?
Wanachofanya wapinzani aswa huyu Lissu Ni kisubiria anacho zungumza MAGUFULI kwenye mikutano yake na yeye kutokea hapohapo, hi inaonesha wazi kuishiwa kwa hoja za kuzungumza bwana Tundu Lissu,lakini sio kuishiwa kwa hoja tu hi pia inatokana na CHADEMA kuwa na sera na ILANI mbovu.
Raisi alivyo kuwa dar alikuwa akizungumza Ni kwa namna gani atakwenda kutatua changamoto za wakazi wa jiji Hili.
Na kwa kuchanganyikiwa kwake mgombea wa CHADEMA na yeye huchukua hoja hizo na kwenda kuwalisha wananchi wa eneo lingine. Mfano raisi alipokuwa Temeke amesema atajenga flyover za kutoshaa ili aende akapunguza adha ya foleni jijini.
Lakini Cha kushangaza TUNDU LISU akiwa mkoani Singida alisikika akiwaambia wananchi wa huko kuwa hawatakula flyover kwa sababu haziwasaidi,kufanya hivyo haiwasadi chadema kupata kura na badala yake wanaendelea kumpaisha raisi kipenzi Cha Watanzania.
Lisu alitakiwa kujua changamoto za watu wa singida na kuwambia Ni kwa namna gani akiingia madarakani atakwenda kutatua changamoto za wakazi wa huko SINGIDA.
Na ndio maana Raisi MAGUFULI kila mahala anapokuwa kwenye kampeni anazungumzia changamoto za eneo husika na ata siku moja uwezi kusikia raisi MAGUFULI akizungumzia kutatua changamoto za wakazi wa Dar kwenye kampeni mkoa mwingine.
Sasa huyu wa kwao kwa kuonesha wazi kuchanganyikiwa kwake akiwa singida ataongea changamoto za Dar, akiwa mwanza ataongea changamoto za kagera na akiwa Mara ataongea changamoto za shinyanga.
Sera na Ilani mbovu ya Chadema ndio inapelekea mpaka mgombea wao kushindwa Ni kitu gani Cha kuzungumza kwenye kampeni zinazo endelea.