Mgombea wa CCM kwa kiti Cha Urais ajapata kizuizi chochote Cha kutembea eneo lolote nchini lakini Hadi Sasa ametembelea chini ya Nusu ya Wilaya na Mikoa ya Tanzania Bara, je, kwa kipindi kilichobaki ataweza kutembea maeneo yaliyobaki?
Mwaka 2015 alifanya kampeni karibia kila kona ya nchi, kwa nini baada ya kuwa madarakani speed yakuwaomba wananchi Kura imepungua? Ikumbukwe kwa miaka mitano pia hakuweza kurudi kwa wananchi kuwashukuru kwa Kura walizompa, maeneo mengi aliyotembelea akiwa madarakani Ni Yale aliyokuwa na miradi ya uzinduzi. Timu ya kampeni itamsaidiaje awafikie Watanzania waliobaki wasije wakamnyima Kura kwa kumtafsiri Kama amewadharau?