Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Kweli Polepole na Bashiru ndiyo mwisho wenu wa kufikiria umeishia hapo. Yani karne hii ya technologia na utandawazi na mwenyekiti wenu mkamshauri ivyo na bila kusita akakubali....
Wamelewa madaraka. Miaka 60 madarakani siyo mchezo. Uzee umewanyemelea. "Thinking capacity is in erosion".
 
Kama kuna mwenye video clip ya hii, irusheni tafadhali.
 
Ushamba mzigo
 
Hayo ni mawazo yako
 
Kugawa pesa kutoa Amri za kuleta maendeleo kwa pesa ambazo ni zao hao hao wananchi ni vituko vilivyosalia Tanzania pekee hakuna Taifa wana mambo ya hivyo.
 
Huyu anahisi kwa vile sehemu nyingi elimu haijawakomboa watanzania hata majukumu madogo madogo ya mbunge hatujui!

Kazi kubwa ya mbunge ni kutunga sheria na kusimamia serikali anayoongoza.

Kama mbunge ndo amwombe yeye basi tumempeleka ng'ombe bungeni sio mtu
 
Ila wabunge wetu nao wanashangaza sana,

Wakati anaomba kura anatoa ahadi kama vile yeye ndiye anakwenda kuzitekeleza kwa fedha zake za mfukoni,

Halafu akiona kashindwa kutimiza ahadi zake atawaambia wananchi kuwa kuzitimiza hizo ahadi alizozitoa sio jukumu lake Bali ni la Serikali.

Na kwamba eti yeye hakusanyi Kodi hivyo wasimsumbue.

Unabakia kujiuliza kama alijua yote hayo hizo ahadi alizitoa ili iweje.
 
Hiyo ndio maana makusanyo yote yanaelekezwa mfuko mkuu wa makusanyo.Ili wawe wapole.
 
Matokeo ya baadhi ya wenye mamlaka kukubalu kuporwa na mtu mmoja.Kwa kusema ndiooo hata kwa Yale yenye kudhulumu haki.
 
Hiyo ndio maana makusanyo yote yanaelekezwa mfuko mkuu wa makusanyo.Ili wawe wapole.

..TL ameahidi kuzirudishia halmashauri mamlaka yake.

..kwasababu hali ilivyo sasa hivi tuna wabunge na madiwani ambao wamepokwa majukumu yao.
 
Huyo ni magu katika ushenzi na udhalilishaji wake.
 
Ahadi huwaahidi vizuri lakini kwa upande wa ccm hujitahidi kuwatekelezea kiasi fulani hata kwa 60% lakini zile ahadi za wabunge wa upinzani hubuni mbinu za kuwakwamisha kwa kutumia halimashauri wakurugenzi ili mbunge wa upinzani aonekane hafai kabsa, huu ujinga umekuwa sana kwenye awamu hii ya tano zaidi huko nyuma kwa kikwete mkapa hawakuwa na shida hawakuwaingilia wakurugenzi kuwaamuru kuzuia maendeleo kwa makusudi kama sasa.
 
..TL ameahidi kuzirudishia halmashauri mamlaka yake.

..kwasababu hali ilivyo sasa hivi tuna wabunge na madiwani ambao wamepokwa majukumu yao.
Awamu ya tano huwatumia RC, DC, makatibu tawala wakurugenzi kukwamisha maendeleo kwenye majimbo yaliyo chini ya wapinzani ili wananchi wawaone wapinzani hawafai hawaleti maendeleo.
 
Mkuu mbona kuna miradi mingi tu imejengwa ndani ya majimbo ya wabunge toka upinzani.

Hiyo no janja janja tu katika mkakati wa kukwepa uwajibikaji ,

Kuna ahadi nyingine zipo ndani ya uwezo wao na hawatekelezi hata hizo pia unataka kusema ni hujuma??
 
Mkuu ndiyo yale ya kupeleka ndege kumchukua Omondi wakati kuna wagonjwa wamekwama mikoani hawawezi kufika Muhimbili. Ndiyo yale ya kupeleka ndege Antananarivo kuchukua miti shamba
Dhana hii inajengwa na ubutu wa Bunge. Kwamba, Bunge limekuwa mhuri tu
Lakini pia ni dhana ya viongozi wa Afrika, utawala bora kwao ni msamiati.
Kinachochagiza haya yote i wananchi kutoelewa haki zao ikiwemo haki ya kodi zao.
 
Hahaaaa. Maghobe...huyo Mbunge kaonyesha dharau si kidogo. Sisi tupambane na hali zetu tu. Tule maghobe tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…