Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Tutarajie kunyoroshwa barabara.
 
Hayo ameyasema mwenyewe wakati akiwasisitizia wakazi wa Singida kuwa ahadi zake ni za kweli tupu maana zikiwa za uongo atakosa nafasi ya kuwa waziri wa malaika huko mbinguni nafasi amabayo anaitamani sana
 
Wakati kampeni hazijaanza alikuwa mwenyewe kujiimarisha, cha kushangaza jinsi siku zinavyoenda amezidi kuporomoka na watu kumwona hana jipya kwenye kampeni zake.

Sera anazoongea hazina mashiko amebaki na sera za kukejeli na vijembe ambavyo wananchi wanaona hana kipya.

Amekaa miaka yote 5 kapunguza ajira halafu leo anakuja tena kusema ataleta ajira mil 8,mara mimi sitoki nje ya nchi ni mzalendo,ajira elfu 8 kashindwa ataweza mil 8 kama siyo kutuletea comedy, vile vile kutokwenda nje ya nchi haionyeshi kwamba we ni mzalendo ni hofu yake tu.

Kusema Lissu siyo mzalendo kisa amekaa nje ya nchi haina mashiko ni kuropoka tu maana hakuna asiye jua alienda kwa matibabu.

Magufuli anaenda kuwa Rais wa awamu moja dalili zote zinaonyesha ,wafanyakazi wamemchoka ,wastaafu wamemchoka ,vijana wamemchoka, wazee wamemchoka na kila mtu anamwona vyote anavyoongea ni usanii tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…