Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Akiomba Dua na kumshukuru yeye atoaye.

Ni jambo jema na ishara ya unyenyekevu.

Safari inaendelea vizuri sana na ushindi ni dhahiri.

FB_IMG_15994389138957719.jpg
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu na ukweli lazima tuuseme hadharani, CCM ina hali mbaya na inazidi kuwa tete kila uchao.

Wamejaribu kutumia viongozi wa dini kusifu na kuabudu juhudi, ngoma imegoma. Alichokipata PM huko alikoenda wote tumeona na hata mikutano ya mama isiyokuwa na wasanii tunaona hali ilivyo tete.

Ukiangalia mikutano ya PM na mama isiyokuwa na wasanii na maroli utagundua namna CCM ilivyo na hali mbaya

Sasa Kikwete anaingia ulingoni kuokoa jahazi kama Hayati JK kipindi cha marehemu Mkapa. Vipi ataweza mziki huu? Asipopewa wasanii na maroli ataweza? Japo nguvu ya Kikwete siyo ya kubeza ukizingatia watanzania tulivyommiss na sifa alizomwagiwa na wapinzani kipindi hiki.
 
Kabla ya ujio wa T. Lissu, CCM walijua mh Magufuli alikwisha eleweka kwa watanzania maana kalibia kila siku vipindi vya TUNATEKELEZA vilieleza waliyoyafanya kupitia television ya Taifa TBC, Mawaziri na makatibu walieleza kwa kina Sana Nini wamefanya.

Cha kushangaza katika kipindi hichi Cha kampeni walewale mawaziri wastaafu hawawezi Tena kuyasimulia waliyoyatenda badala yake Magufuli anakutana na wananchi na wanampinga live mbele ya television ya Taifa TBC, mfano kule BUSEGA.

Hiyo ni sehemu moja tu, lakini pia kitendo Cha KM wa CCM kuwataka UVCCM kujibu hoja za upinzani inaashiria hali halisi kwamba upepo umebadilika. CCM hawakujua kuwa siasa Ni maisha ya watu, na watu asili yao ni Upinzani.

#28october2020
 
Back
Top Bottom