Kabla ya ujio wa T. Lissu, CCM walijua mh Magufuli alikwisha eleweka kwa watanzania maana kalibia kila siku vipindi vya TUNATEKELEZA vilieleza waliyoyafanya kupitia television ya Taifa TBC, Mawaziri na makatibu walieleza kwa kina Sana Nini wamefanya.
Cha kushangaza katika kipindi hichi Cha kampeni walewale mawaziri wastaafu hawawezi Tena kuyasimulia waliyoyatenda badala yake Magufuli anakutana na wananchi na wanampinga live mbele ya television ya Taifa TBC, mfano kule BUSEGA.
Hiyo ni sehemu moja tu, lakini pia kitendo Cha KM wa CCM kuwataka UVCCM kujibu hoja za upinzani inaashiria hali halisi kwamba upepo umebadilika. CCM hawakujua kuwa siasa Ni maisha ya watu, na watu asili yao ni Upinzani.
#28october2020