Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Tukiwa waungwana kutumia kilugha chako kwenye kampeini ni ukabila maana unatafuta huruma ya kabila lako kwa kuzungumza lugha yao .
Kilugha kitumike wakati wa kusalimia tu maana kwenye mikutano hiyo siyo wote wanajua lugha ya mamaako.
Alitumia 2015 dhambi iko wapi kutumia 2020 kwa unataka kusema Tundu Lissu kuvaa kanzu na balagashia anatafuta huruma ya waislamu acheni upumbavu wa siasa za bei nafuu
 
CHADEMA mnajitutumua hapa JF lakini mkiwa wenyewe huko mnakiri kuwa mnashiriki tu ili kutimiza wajibu.
 
Naona Bashiru ametoa Order kuwa kila kada wa CCM mwenye akaunti Twitter anapaswa kumnadi Magu, la sivyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Mambo ni magumu huko field.
Raia wamekuwa wagumu.

1599514082197.png
 
Si mara moja wala mara mbili nimesikia hasa katika matukio ya uzinduzi viongozi waliopewa dhamana na JPM mwenyewe wakimuaminisha kuwa kazi ameshaimaliza hana haja ya kuzunguka 2020.

Sasa hivi wanapoyaona haya wana yapi tena ya kumuambia? Wana ujasiri wa kusema lolote tena? Au ndio wanamuambia tulia mzee haka ni kaupepo tu kanapita?
Maendeleo hayana chama
 
Yani wamelegea utafikiria samaki aliechina,ccm kinabebwa na nec,policeccm,tiss bila hivyo kinasahaulika milele...hii ndio hali ya leo mwanza wamejaza watoto tu mabasi ya zuberi, zakaria, macoaster ndio yalikua yanasomba tu watoto View attachment 1562261

1599514198331.png

1599514239164.png

kama unajiskia vibaya vumilia tu , huu mchezo hauhitaji hasira maaana ccm ipo mpaka mwaka 2100
 
Hapa haya mataga yameambiwa buku 7 zitatolewa baada ya mkutano ndiyo maana yanakomaa hapo ni saa 12 jioni na yalibebwa kwenye malori kuletwa hapo mkutanoni asubuhi saa kumi.

Mpinzani wa CCM ni ccm wenyewe! ili kue na upinzani mzito lazima mgombea upinzani atoke ccm , bila hapo tunaenda mpaka 2100, mtajipa moyo sana lakini ata akisema asiendelee na kampeni ana ushindi mzito kwahio mwache atekeleze wajib tu
 
Si mara moja wala mara mbili nimesikia hasa katika matukio ya uzinduzi viongozi waliopewa dhamana na JPM mwenyewe wakimuaminisha kuwa kazi ameshaimaliza hana haja ya kuzunguka 2020.

Sasa hivi wanapoyaona haya wana yapi tena ya kumuambia? Wana ujasiri wa kusema lolote tena? Au ndio wanamuambia tulia mzee haka ni kaupepo tu kanapita?
Ngoja waje wenyewe waseme
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mpinzani wa ccm ni ccm wenyewe! ili kue na upinzani mzito lazima mgombea upinzani atoke ccm , bila hapo tunaenda mpaka 2100, mtajipa moyo sana lakini ata akisema asiendelee na kampeni ana ushindi mzito kwahio mwache atekeleze wajib tu
Unapoteza muda bure Mkuu, hiyo serikali ya WATEKA NYARA imechokwa mno kwa sasa. Umati wa kwenye mikutano yake ni wanaofuata BURUDANI TU.
 
Wakati wa Lowasa mlisema hivi hivi??
 
Wakati wa Lowasa mlisema hivi hivi??

issue sio wakati wa lowasa ila ndo ukweli sasa! haiwezekani chama chochote kukitoa ccm madarakani kwa mda huu labda mbelen uko ambapo pole pole amesema ni 2100
 
Unapoteza muda bure Mkuu, hiyo serikali ya WATEKA NYARA imechokwa mno kwa sasa. Umati wa kwenye mikutano yake ni wanaofuata BURUDANI TU.

Kwani mmenyimwa na nyie kuweka wasanii? kwani ccm peke yake ndio wanaweka wasanii kwenye majukwaa? ACT mpaka NEY wa Mitego yupo, tafuteni sera ingine hii ishachacha

Magufuli ana followers 910K twitter, Tundu Lissu ana 100K, mpaka apo tumefunga mada
 
Si mara moja wala mara mbili nimesikia hasa katika matukio ya uzinduzi viongozi waliopewa dhamana na JPM mwenyewe wakimuaminisha kuwa kazi ameshaimaliza hana haja ya kuzunguka 2020.

Sasa hivi wanapoyaona haya wana yapi tena ya kumuambia? Wana ujasiri wa kusema lolote tena? Au ndio wanamuambia tulia mzee haka ni kaupepo tu kanapita?

Wewe umeona nini cha kukutisha?
 
Unapokuwa umefanikiwa uko level yajuu watu wabaya kwako ni wapambe rejea hotuba ya mwalimu Nyerere alipotaka kung'atuka wapambe walivomshauri kuwa nchi bado changa kumbe nchi wanayoisema wapambe ni familia zao. Katika marais wote waliopita Rais mwenye wapambe wabaya ni Magufuli inabidi awe makini nauhakika wanamshauri hata kujiongeza muda
 
Tukiwa waungwana kutumia kilugha chako kwenye kampeini ni ukabila maana unatafuta huruma ya kabila lako kwa kuzungumza lugha yao .
Kilugha kitumike wakati wa kusalimia tu maana kwenye mikutano hiyo siyo wote wanajua lugha ya mamaako.
Bahati nzuri, Magufuli anaongea Lugha zote. Na hakuna sheria yoyote inayozuia. Kikubwa mtu asiongee lugha zisizoeleweka, au za kuudhi mfano kama yule jamaa yenu mzee wa kutukana watumishi wa umma nakupayukapayuka ovyo
 
Jana nimeenda kuangalia jina langu kuhakikisha kuwa nampigia Lissu kura, niko kwenye listi na watoto wangu watatu nimeona majina yao.
 
Aisee CCM na JPM wao wana hali mbaya sana. Si bara si Zanzibar.

Kwa hali niliyoiona leo Zanzibar kwenye mkutano wa Lissu ni dhahiri CCM lazima wanyooshe mikono mwaka huu!

Sasa ni wazi!! Uchaguzi wa kihistoria Tanzania ni mwaka huu!
Endeleeni kujifariji, majibu kwenye sanduku la kura
 
Tukiachilia mbali kile KIWANDA CHA MATUSI. NA KIKI ZA MIUJIZA, nani mpinzani wa Jemadariii ,MAGUFULI??
hata hizi kampeni anazofanya Magufuli nikutimiza wajibu tuuuu. Hata akiamua kujitulia ikulu ushindi wa asilimia mia, ukopale pale.
Mmmh ningumu kushinda kwa asilimia 100 bado naona Kuna upinzani mkubwa
 
Si mara moja wala mara mbili nimesikia hasa katika matukio ya uzinduzi viongozi waliopewa dhamana na JPM mwenyewe wakimuaminisha kuwa kazi ameshaimaliza hana haja ya kuzunguka 2020.

Sasa hivi wanapoyaona haya wana yapi tena ya kumuambia? Wana ujasiri wa kusema lolote tena? Au ndio wanamuambia tulia mzee haka ni kaupepo tu kanapita?
La msingi siyo matukio ya majukwaani bali nini wasikiacho wanaohudhuria ili wachambue pumba na mchele.

Mtaji wa aliyeko madarakani ni yake aliyotenda na siyo atakayotenda. Km huyu alipewa ruzuku (kodi ya wapiga kura) kaifanyia nini na yule aliyekusanya kodi naye kaifanyia nini. Mpiga atapenda kusikia kutoka kwa wote wawili aamue yupi wa kumwamini.

Kinachotokea kwa sasa, hata humu JF ni mashindano ya matukio ya nyomi na ubingwa wa kukashifiana kwa wagombea. Lakini, kundi moja linaeleza jinsi pesa ya mlipa kodi ilivyotumika na jinsi likipewa madaraka tena nini kitafanyika kwa pesa yao. Kundi lingine libatoa ahadi bila kueleza ahadi hizo zitatekelezwaje.

Sasa wewe Mkuu Mtini, huoni kama kuna ambaye hastahili kufanya kampeni maana tayari aliyoyafanya ni mtaji tosha wa kura?
 
Back
Top Bottom