Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Na wewe unataka kusujudiwa akati unamiliki kisimu cha kichina bando la kukopa tala........minywele michafu ....kuoga sio lazima .......haya sasa kakojoe ulale hapa
Mimi ni civilized na matured pia sikuruka stage ya makuzi hivo sitegemei kusujudiwa na kuabudiwa ili nikamilike
 
Tuombe tu haki itendeke na wala tusiwe mawakala wa kusemea watanzania wengine. Kuna wengi sana wapo kimya ila miyoni mwao wanaye mgombea wanaeamini ni mkombozi wa nchi na wananchi!
 
Tangu aingie madarakani 2015, Rais Magufuli amehakikisha vyombo vyote vya habari, ikiwemo TV, Magazeti, na mitandao mingine ya kijamii wanatangaza habari zake peke yake. Pale alipopata nafasi ya kuapisha viongozi wapya alitumia nafasi hiyo kufanya kampeni alikwa live kwenye TV (TBC, Channel 10 na ITV. Haikuishia hapo, kila alipokuwa akielekea nyumbani kwake Chato, alihakikisha anasimama kila mahali na kufanya kampeni kwa kuelezea mambo aliyoyafanya.

Wakati Rais Magufuli akifanya hayo yote, alihakikisha wapinzani hawafumbui mdomo, alihakikisha vyombo vyote vya habari haviwapi air time wapinzani, isipokuwa vi TV vya online ndivyo viliruhusiwa kuchukua habari za wapinzani.

Swali la kujiuliza, kama kwa miaka mitano amekuwa akijinadi yeye peke yake, kampeni za uchaguzi 2020 kuna haja gani ya yeye kupoteza muda wake?
 
Mabibi na mabwana live tokea Dodoma.

Mgombea huyu asipokuwa na majibu thabiti na ya wazi kuhusiana na:

1. Uhuru wetu
2. Usalama wetu
3. Demokrasia yetu
4. Haki zetu
5. Ustawi wetu

Zaidi sana "katiba yetu."

Kwa hakika atakuwa anatwanga maji kwenye kinu.

Kwamba asiwe na neno lolote kuhusiana na wasiojulikana? Wala enguaengua ya wagombea tunayoiona? Wala nafasi sawa kwa vyama siasa katika kampeni? Wala katika kutumia vyombo vya umma kwenye kampeni kwa mujibu wa katiba?

Tusije kulaumiana come Oct. 28.

Macho na masikio Dodoma.

Safari hii tunataka majibu.

Hapendwi mtu hapa!
 
Anachohakisha magufuli
Nchi inakuwa na
1. Viwanda
2. Madaraja.
3. Mabarabara
4. Ndege za kutosha hata kama mbovu
5. Majengo ya hospital yasiyo na wahudumu
6. Ujenzi wa mji wa chato ili uwe mkoa
7. Ujenzi wa uwanja wa mpira wa kimataifa jijini Chato
8. Kukamata kamata wale wote wanaompinga
9. Kupindisha pindisha katiba ili kukidhi matakwa yake.
10. Kuhakikisha upinzani unakufa kwa gharama yoyote.
11. Kuhakikisha kauli ya rais inakuwa katiba ya nchi.
12. Kuifanya Tanganyika iwe kama Ulaya kwenye ndoto
13. Na mengine mengi mazuri
 
Habari yenu wanabodi,

Kama mada isemavyo, ili upate uhalali wa kuhukumu mhalifu lazima usikilize upande wa mshitakiwa na na anaetoa malalamiko..
Naomba niseme ktk uchaguzi huu CCM ndiye mlalamikiwa, ndiye mshitakiwa, anashitakiwa na vyama vingine anashitakiwa na wananchi wengine.

Nimekuwa nikisikiliza sn mashitaka yanayotolewa dhidi ya CCM na leo nilikaa Karibu kabisa ili kusikia uteteze wa mshitakiwa...
Moja ya mashtaka anayopewa CCM ni:

1: Uhuru wa watu hakuna
2: Uhuru wa vyombo vya habari hakuna
3: Watu wanatekwa na kuuawa ila ccm haichukui hatu
4: Hali za maisha mtaani ni ngumu kuliko wakati mwingine wowote
5: Wakulima hawana bei nzuri za mazao
6: Watumishi hawana nyongeza za mishahara
7: Vituo vya afya mlivyojenga havitoi huduma nafuu ni zile zile
8: Kwanini CCM haitaki uchaguzi wa huru na haki, n.k

Kwa kweli nimemsikiliza mshitakiwa hajajibu shitaka hata moja. Mshitakiwa amejibu mashitaka ambayo hajashitakiwa nayo. Hakuna mwananchi anaehoji barabara, hakuna mwalimu anaetaka ndege, hakuna machinga anaetaka kuuza bidhaa mahala popote bila kupata wateja ...naomba wakili yeyote wa ccm aliyebaki humu JF(wanachama),mtusaidie kujibu vinginevyo tukubaliane yafuatayo:-

1: CCM itaendelea kutawala kwa kuwa sehemu kubwa ya wapiga kura hawana dira na wala hawana cha kudai (wazee, wanafunzi, maskini waliokata tamaa)

2: Ni rahisi kutawala kwa kuwa ya hao watu namba moja above maana kwenye nchi maskini ndiyo wengi

Mwisho nahitimisha upande wa MASHTAKA UNA HOJA KUBWA NA NZITO KULIKO UPANDE WA MSHITAKIWA. Kwa kuwa hakimu ni baba mdogo wa mshitakiwa na kwa kuwa mshitakiwa amesindikizwa na wapiga debe wengi mahakamani wachache wanaamini anayo haki.

MAENDELEO hayana vyama
 
Mwisho nahitimisha upande wa MASHTAKA UNA HOJA KUBWA NA NZITO KULIKO UPANDE WA MSHITAKIWA... Kwa kuwa hakimu ni baba mdogo wa mshitakiwa na kwa kuwa mshitakiwa amesindikizwa na wapiga debe wengi mahakamani wachache wanaamini anayo haki....
 
Acha CCM waendelee kutangaza sera zao, Lissu aendelee kuropoka, tuone je mwisho wa siku wananchi watasikiliza sera au uhuru wa kuropoka.
 
Ndio maana wamejaza wasanii siku nzima. Walofata burudani ya muziki ndio wamejaa wakwaachia hata usiku kucha.
 
Habari yenu wanabodi,

Kama mada isemavyo, ili upate uhalali wa kuhukumu mhalifu lazima usikilize upande wa mshitakiwa na na anaetoa malalamiko..
Naomba niseme ktk uchaguzi huu CCM ndiye mlalamikiwa, ndiye mshitakiwa, anashitakiwa na vyama vingine anashitakiwa na wananchi wengine....
Mashtaka peleka mahakamanj.

Hapa tunanadi sera zetu na siyo kuchunguza tuhuma ambapo unaweza kuviomba vyombo husika wachunguze.

Kama mlijipanga kuongelea hoja za kuokoteza mitaroni basi mmetopola.
 
Nitumie aya mbili tu kutoa ushauri kwa Mh Rais wa JAMHURI ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Nimevitazama vyama vyote tangu kutangaza nia hadi jana vilipoanza kampeni. Nimegundua hawana hoja wala ushawishi wa kuwashawishi Wananchi kuvichagua. Wengi wao wamejaa sanaa na kutafuta fursa za kupata fedha kutoka kwa wafadhiri na si kutafuta dola.

Baada ya kutambua haya, ninaomba nimshauri Rais wetu mpendwa MUDA huu autumie kuendelea na majukumu ya kulijenga taifa kwa kufanya kazi zake za Urais. Kwa namna wapinzani walivyo jipanga Hii kazi wakabidhi UVCCM NA UWT TU. Wewe usijichoshe bure hawa washughulikiwe na vijana na Wanawake tu. Kule Mbagala wamefeli, Kawe wameshafeli......
 
Nilipoona jina nikajua ndani hakuna content zaidi ya blah blah na porojo! Baada ya kusoma nimejiridhisha kuwa nilikuwa sahihi!

Toeni ajira kwa watu makini wawasaidie kuandika propaganda zilizoenda shule na sio upuuzi kama huu!
 
Kweli CCM ni chama bora kwa kuweza kuarticulate issues na mipango yao. Nimeona kipengele kinachozungumzia Magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Covid 19.
 
Ni Furaha iliyoje kuwa na Baba anayejali
FB_IMG_15989054356815143.jpg
FB_IMG_15989054283147940.jpg
 
Back
Top Bottom