Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Ukisoma comments katika tweet hii hapa utagundua kuwa Watanzania wana Ufahamu sana kuliko dhana aliyo nayo Mgombea wa CCM kichwani mwake kuwa Wapiga kura hawajui chochote kuhusu pumba na mchele katika kauli zake... akiongea pumba tu wanampa za Uso na kumrudisha huko alikotoka; wenye akili ndani ya CCM kama Wapo nadhani wanaona aibu sana kuwa na Mgombea kama huyu

Soma comments:
“Ndugu zangu Watanzania msichague Watu wa majaribio katika uongozi, uongozi sio wa kujaribu madhara yake makubwa, zipo Nchi zilijaribu uongozi madhara yake mnayaona, mpaka leo zinapigana, usalama hakuna, kabila moja wanapigana, amani haipo” -JPM akiwa Geita
#MillardAyoUPDATES https://t.co/VkTiTLmp31
 
Kama mnavyokumbuka kipindi Rais Magufuli anafanya kampeni mwaka 2015 aliomba akasema anaomba miaka mitano tuu anyooshe nchi, saa hivi anataka tena mitano ya nini wakati ameshatunyoosha au anataka kutuvunja vunja?

Akae tuu pembeni jamani apishe na wengine kwanza alishasema alisukumiwa huko.
 
Mi naona riziki anatoa Mungu, Magufuli has nothing to do with it, hivi kabla ya Magu ulikula bata Sana mzee eti!?
 
Wana CCM sehemu nyingine tunajisikia wanyonge.

Nguvu kubwa ya mgombea Urais imeelekezwa Kanda ya Ziwa peke yake.
Naona sasa hivi Mh Rais anatembelea wilaya hadi wilaya huko Kanda ya Ziwa.
Siyo bure kuwa maendeleo mengi katika kipindi hiki cha miaka 5 iliyopita yameelekezwa huko huko Kanda ya Ziwa.
Je , watanzana tunataka kumpigia kura mh Rais wa Kanda ya Ziwa au Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Mtu mwenye akili atang'amua kuwa kwa mahesabu yaiyopigwa ni kwamba mgombea wa CCM akipata kura za kutosha Kanda ya Ziwa wengine hata wasipompigia kura ni poa tu.
Hii ni kuua Utanzania.

Hatuchagui Rais wa Kanda ya Ziwa , tunataka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wapambe wa Rais wamwambie vile vile kuwa Rais akitembelea wilaya zote za Tanzania itakuwa vizuri zaidi ili wamweleze watakacho kwa miaka mitano ya mbeleni
 
Hata Tundu Lisu alianzia huko.....kanda ya ziwa ina kura zaidi ya milioni 10!
 
Hata Tundu Lisu alianzia huko.....kanda ya ziwa ina kura zaidi ya milioni 10!
Lissu kaanzia Dar kaenda arusha akaenda mwanza akaenda shy tabora dom mbeya mtwara then zenji hakukaa kanda ya ziwa kama huyu bwana na ukizingatia nguvu inayotumika huku kanda ya ziwa ni kubwa saaana na ndiko hakubariki kiivyo pia ndo maana anatumia kuchafua mji kwa mabango kusomba mpk watoto wetu kuwaletea burudani badala ya sera naona wanaandaa kuiba kura nyingi za urais huku lake zone
 
CHADEMA mnahangaika, mnataka rais afanye kampeni nchi nzima kwa wakati mmoja, kwani uko mkoa gani nikupe ratiba. Tume imepanga ratiba wagombea wasikutane eneo moja kwa wakati mmoja.
Magufuli atafika mikoa yote.
 
Ccm wametawanyika nchi nzima
Magu anashambulia
Kikwete anashambulia
Pinda
Makamu wa rais
Majaliwa
Na wengine wengi

Chadema wanatembea fungu moja wote badala watawanyike
 
Ccm wametawanyika nchi nzima
Magu anashambulia
Kikwete anashambulia
Pinda
Makamu wa rais
Majaliwa
Na wengine wengi

Chadema wanatembea fungu moja wote badala watawanyike
Nguvu yao ipo wakitembea pamoja,

Watapata aibu Sana Kama wakijaribu kugawana maeneo.

CCM timu yake ina watu wenye Ushawishi mkubwa hivyo wakigawana bado Kila mahali watu watapatikana wa kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…