Tangu aingie madarakani 2015, Rais Magufuli amehakikisha vyombo vyote vya habari, ikiwemo TV, Magazeti, na mitandao mingine ya kijamii wanatangaza habari zake peke yake. Pale alipopata nafasi ya kuapisha viongozi wapya alitumia nafasi hiyo kufanya kampeni alikwa live kwenye TV (TBC, Channel 10 na ITV. Haikuishia hapo, kila alipokuwa akielekea nyumbani kwake Chato, alihakikisha anasimama kila mahali na kufanya kampeni kwa kuelezea mambo aliyoyafanya.
Wakati Rais Magufuli akifanya hayo yote, alihakikisha wapinzani hawafumbui mdomo, alihakikisha vyombo vyote vya habari haviwapi air time wapinzani, isipokuwa vi TV vya online ndivyo viliruhusiwa kuchukua habari za wapinzani.
Swali la kujiuliza, kama kwa miaka mitano amekuwa akijinadi yeye peke yake, kampeni za uchaguzi 2020 kuna haja gani ya yeye kupoteza muda wake?