Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Hapana mkuu siyo kila mtu. Ni kwa mtindo wa wengi wape. Maamuzi yakipata sapoti ya wengi yanakuwa halali.
Hao wengi utaziona kura watakazompa Magufuli Oktoba 28 mwaka huu.

Hao wengi wapo huko mikoani na ndio wanaofaidika na kila kinachofanyika awamu hii.

Hao wengi ni zaidi ya hawa wasomi wa Twitter wenye ufundi mkubwa wa kukosoa kila kinachofanyika.
 
punguza hasira sio mimi niliyeamrisha watu wasombwe wakamwone lissu ?

Hiyo bajeti ya kusomba watu ipo kwenye gharama za kampeni Chadema
 
Kusema kampeni za CCM ni ngumu ni vichekesho. Rais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%

Rafiki zetu wa CHADEMA mtaula wa chuya huu mwaka hampati hata mbunge.

Ingekuwa rahisi hivyo asingelialia huko mikoani na kusema mbona marais wengine wamepewa miaka 10 kumi kwani yeye ametukosea nini!! Hii ni ishara tosha kishatambua hatakiwi na 28Oct anaweza akafungishwa virago.
 
Hiyo ni kauli ya kisiasa kuongezea kura zifikie 99%,October 28 mtashaanga
Ingekuwa rahisi hivyo asingelialia huko mikoani na kusema mbona marais wengine wamepewa miaka 10 kumi kwani yeye ametukosea nini!! Hii ni ishara tosha kishatambua hatakiwi na 28Oct anaweza akafungishwa virago.
 
View attachment 1567029 punguza hasira sio mimi niliyeamrisha watu wasombwe wakamwone lissu ?

Hiyo bajeti ya kusomba watu ipo kwenye gharama za kampeni Chadema
Dah!!! brother!!!napata shda Sana kung'amua uelewa wako,inawezekana wewe chaguzi za vyama vingi tz ndio mala yako yakwanza kushiriki.....ili lakubeba watu kwenye maroli Kama ng'ombe CCM halijaanza leo....kwaiyo ustumie Nguvu kubwa kuamnsha watu....mwaka2000 kwastaili ilsha wahi tokea ajar kubwa pale Nyakato national Jj Mwanza....;Tafuta point za msingi ila sio kujchosha na Kitenco chako kwenye mikutano yawapinzan ata viongoz wako huwa wanaona haibu kujbu ili nahc ndio maana wanawatumia walemavu wafikra Kama nyny.maroli niutalatbu waCCM toka mwaka1995 ili kuuhadaa ulmwengu kuwa wanakubalka lakn niuongo.usichokijua pia huwa kunafungu lakuwalpa hao kwaajl yachakula kwasiku watakayo kua fiestan,mwaka huu ndio dau lilipungua kdogo nlienda kufanya tafti zangu singida sku amefka jiwe,nkaambiwa walilipwa elfu5 kla mtu....tofaut namiaka mingne tulkuaga tunapewa elfu10 adi 15....;Tafuta sababu nyngne ila hii itakuabsha
 
 
Sasa hiyo 90% unaipima na kuipataje ikiwa mgombea wa CCM hana mvuto, mpaka malori yatumike, shule zifungwe na wanafunzi wahudhurie?
Mkuu tumaini lao lotee ni tume tu ichakachue sana kama ilivyofanya kwa EL vinginevyo huyo mtu wao ambae wanasema kafanya mengi madege,reli bwawa la umeme Rufiji yote hayajamsaidia kipindi cha mvutano wa suala la korosho bungeni alifikia hatua ya kumuuliza katibu mkuu Bashiri namba ya wabunge wa ccm huko kusini akidai anaweza kuwafukuza wote,leo hii amini usiamini anamwomba Kikwete na mkewe wamsaidie kampeni mikoa ya kusini,shida yake kubwa alijiaminisha katika vitu na si maisha ya watu.
 
Hiyo ni kauli ya kisiasa kuongezea kura zifikie 99%,October 28 mtashaanga
😂😂😂😂🤣🤣🤣Kauli ya kisiasa.....unafel mkuu.....mwenzio kasoma upepo ndio maana anaomba huruma ya watanzania......ndio maana adi mama nyerere akalazmishwa kwenda kumuombea kura hali nitete usidanganywe namaneno yamtandaoni au watu mnaowasomba kwenda kushuhudia wasanii.ingia mitaan ndio utapata jibu....me npo nazunguka kufanya tafti anapopta magufuri na Ccm...nimefka Nilianzia Dodoma,singida,Arusha,babati,Mara,Mwanza,na Maswa Simiyu...kifup hali ntete kwawatu ndan kabsa usidanganywe namaneno yawatu wenye access ya mtandao.Bla janjajanja safar hii mtu anaweza weka history yakua Rais wamiaka5 tu
 
Kwenye biashara hapo bana hii nchi iache utani,,
Biashara zinakufa watu wanarudi kwenye umasikini. Biashara ndizo zinalea idadi kubwa ya watu kuliko hizo ajira za serikali.
Rais yeyote atakayepita afanye jitihada za makusudi kuiinua sekta ya biashara.
Ni huruma sana kuona vijana wachapa kazi wanafunga maduka na kurudi vijiweni.
 
Ndio nakuambia hiyo ni sayansi ya siasa anaongezea ushindi kufikia 98%
 
Wanafunzi ndio wapiga kura wa kesho, tatizo CHADEMA mmjezana wengi wenye fikara zisizo ona mbali
Je hiyo kesho watakuwa na uhakika wa maisha? Je watakuwa na uhakika wa ajita? Je mikopo ya elimu ya juu itakuwa rafiki kwao? Je huduma za kijamii zitakuwa zenye manufaa nao?
 
Ndugu,hao wote uliowataja hawana mvuto kabisa,kwakuwa hawana jipya.
Wapiga kuja wanajipima wao wenyewe kwa miaka hii mitano hali ikoje?Hao ulio wataja zaidi Treni/ndege/madaraja/zahanati hawana jipya!
Mtaani hali mbaya,wanyonge mlo moja taabu.
 
Katika hali inayoashiri mikikimiki ya Campaign, Mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi amepumzika kufanya kampeni.

Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa kampeni za Mwaka huu zimekuwa siyo nyepesi kama zilivyodhaniwa.

Magufuli ambaye mwaka 2015 alizunguuka kwa barabara nchi nzima, inaonekana dhahiri kuwa safari hii hawezi kuifikia rekodi ya mwaka huo. Safari hii inaonekana ameweka nguvu zaidi katika mikoa ya ukanda wa ziwa huku Wapiga kampeni wengine wakienda kanda nyingine.

Hata hivyo wapiga kampeni wake yaani Mama Samia na Kassim Majaliwa hawana mvuto mkubwa wa kisiasa wa kuweza kuchangia kura za maana kwa Magufuli.

Wakati huohuo mgombea wa Chadema Tundu Lissu ambaye ana faida ya kujinadi mapema makhsusi kwa ajili ya uchaguzi huu kwa kisingizio cha "kutafuta wadhamini" ameendelea kuchanja mbuga kwenye ngazi ya jimbo kwa jimbo baada ya kumaliza kupiga show kwenye ngazi ya kanda kwa kanda.

Sambamba na ngazi ya Jimbo kwa jimbo, Chadema watafanya mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanamng'oa Magufuli madarakani.

Bado haijajulikana kama kupumzika huku kwa mgombea wa CCM ni routine ya kawaida tu au uchovu au afya, tunangoja chama cha mapinduzi kitujuze zaidi.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…