Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Ingawa ni mgombea, bado pia ni Rais wa nchi kwa hiyo hawezi kutumia muda wote kwenye kampeini na kusahahau majukumu ya uraisi. Halafu kama angekuwa na woga, ndipo angekuwa anafanya kampeini usiku na mchana lakini kwa vile hana hofu basi anaweza kuchukua time-off ili kufanya mambo mengine.

October 28 ndiyo fainali.

Au inawezekana afya haimruhusu kuendelea na mikikimikiki ya kampeni. Tungoje CCM watujuze zaidi

Lakini kikubwa zaidi, wana CCM wengi hawana shauku ya kumpigania Magufuli kwenye kampeni za mwaka huu isipokuwa kwa unafiki na hofu tu ya kushughulikiwa.
 
Pamoja na kutegemea kuiba kura , ajue kabisa watu wameshamuwekea plan B na dunia nzima inafuatilia kila kinachoendelea Tanzania Mpaka uchaguzi ukamilike .
Screenshot_20200911-174752.png
 
Tatizo watu wanakuwa na maana zao za usikivu na unyenyekevu ambazo ni za kumtaka kiongozi aendeshe nchi kwa matakwa yao.

Tupo milioni 59 ikiwa rais atamsikilza kila mtu hip haitakuwa nchi bali itakuwa Bar.

Kampeni hazijadorora tena zimeboreshwa kwani mashambulizi yanatokea kila upande.

Mama Samia, Pinda, Kikwete, JPM na Majaliwa wanashambulia jukwaa katika mikoa tofauti huwezi kulinganisha na Lissu anayetembea mkoa mmoja hadi mwingine na akipitisha michango kwa wanaomsikiliza.

Mikutano mingi haimaanishi kuwa ni ubora. Watu wanapima ubora na sio wingi. Hayo kwenye soka tunasema chenga twawala.
 
Katika hali inayoashiri mikikimiki ya Campaign, Mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi amepumzika kufanya kampeni.

Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa kampeni za Mwaka huu zimekuwa siyo nyepesi kama zilivyodhaniwa.

Magufuli ambaye mwaka 2015 alizunguuka kwa barabara nchi nzima, inaonekana dhahiri kuwa safari hii hawezi kuifikia rekodi ya mwaka huo. Safari hii inaonekana ameweka nguvu zaidi katika mikoa ya ukanda wa ziwa huku Wapiga kampeni wengine wakienda kanda nyingine.

Hata hivyo wapiga kampeni wake yaani Mama Samia na Kassim Majaliwa hawana mvuto mkubwa wa kisiasa wa kuweza kuchangia kura za maana kwa Magufuli.

Wakati huohuo mgombea wa Chadema Tundu Lissu ambaye ana faida ya kujinadi mapema makhsusi kwa ajili ya uchaguzi huu kwa kisingizio cha "kutafuta wadhamini" ameendelea kuchanja mbuga kwenye ngazi ya jimbo kwa jimbo baada ya kumaliza kupiga show kwenye ngazi ya kanda kwa kanda.

Sambamba na ngazi ya Jimbo kwa jimbo, Chadema watafanya mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanamng'oa Magufuli madarakani.

Bado haijajulikana kama kupumzika huku kwa mgombea wa CCM ni routine ya kawaida tu au uchovu au afya, tunangoja chama cha mapinduzi kitujuze zaidi.

View attachment 1567050
mwinyi.jpg

TUNA JAMBO LETU ZANZIBAR KAA KWA KUTULIA
CCM NI CHAMA IMARA
YAJAYO NI NEEMA ZANZIBAR YA DR HUSSEIN MWINYI
 
Ndugu,hao wote uliowataja hawana mvuto kabisa,kwakuwa hawana jipya.
Wapiga kuja wanajipima wao wenyewe kwa miaka hii mitano hali ikoje?Hao ulio wataja zaidi Treni/ndege/madaraja/zahanati hawana jipya!
Mtaani hali mbaya,wanyonge mlo moja taabu.
Tangu tupate uhuru hakuna rais aliyesifiwa kwa kuleta hali nzuri mtaani.

Huwa tunasubiri rais aondoke ikulu ndio tumpe sifa za kinafiki, tatizo ni zaidi ya kumnyooshea kidole rais anayekuwepo madarakani.
 
Yaan hii nayo hoja? Rudi kajifue
Mbishi anahisi anachofikiria yye ni sahihi kwenye kila jambo. Hivi unamtoza mmachinga kodiak ya 20 kwa mwaka wakati wewe mshahara wako hulipi kodi . Unapora KOROSHO za watu na kuwalipa kwa mafungu ili uonekane una maamuzi yasiyoyumbaa kisha kesho unaenda kuomba kura siyo ujinga nn
 
Mwingine anaweza kusema mwaka 2015 alitumia nguvu kubwa na akapita maeneo mengi kwa sababu kazi ilikuwa ngumu hata matokeo ya Uraia yalisadifu hilo.
Mwaka huu kazi ni nyepesi mno, kila mtu anaona kinachotokea, mwitikio wa Raia kwake na kwa wapinzani wake. ACT wameshanyosha mikono, CDM ndiyo Kama hivo, Juzi uliona Raia wa pwani Kama vile hawamjui, Jana Morogoro mjini umeona hali mwenyewe, kule Mheza ilikuwa aibu. Hata Makamanda tangu Mlivyoposti picha za Mbeya, hamjaposti tena, utafikiri Mgombea wenu yupo likizo naye.
Sasa kwa namna hiyo kwanini asipumzike Budha. Game imekuwa nyepesi mno.
Kama umegundua, wanachokifanya CCM baada ya uhakika wa Kushinda, ni kuhakikisha mtu anapata kipigo cha mbwa koko, hicho ndicho kinachofanyika kwa Sasa.
The


Idiot !!!Morogoro hukuona picha?
 
Kusema kampeni za CCM ni ngumu ni vichekesho. Rais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%

Rafiki zetu wa CHADEMA mtaula wa chuya huu mwaka hampati hata mbunge.

Hivi kama kwa miaka yote mitano alivipiga pin vyama vingine akabaki yeye na ccm yake kupiga kampeni na kutoa rushwa kila alipopita, mpaka sasa hajiamini, na anendelea na hizo kampeni, kwa nini kama tayari ana ushindi si angetulia tu ili oa wengine kwa hii miezi michache ya kampeni wagawane hizo 10% iliyobaki?

Kati ya mwaka atakaopata ugumu wa kampeni ni mwaka huu maana mbinu za ccm zimefeli na imebakia moja tu ya kutangaza kwa nguvu/mabavu aliyeshindwa kuwa kashinda.
 
Mikutano mingi haimaanishi kuwa ni ubora. Watu wanapima ubora na sio wingi. Hayo kwenye soka tunasema chenga twawala.
Ukiwa na viongozi wanne wanaofanya kampeni katika maeneo manne tofauti sio sawa na mmoja anaye kampeni sehemu moja tu.

Suala la ubora wa utekelezaji wa sera ndio linaloibeba CCM.
 
Morogoro hukuona picha?
Ukweli ni kwamba, mkitukana huwa ni dalili kuwa kilichoandikwa kimewashika, so najua hapa hoja imekuingia. Morogoro niliona tena UTV achana na editing ya mitandaoni. Wale watu kwa mji mkubwa wa Morogoro walipaawa wawe kwa level ya Mgombea udiwani
 
Back
Top Bottom