Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Mkuu nafikiri umesahau mambo muhimu, Mheshimiwa alikwenda kujificha Chattle, ilikuwa ni pale juisi ya Madagascar ilipoletwa na Kabudi, ndipo Mkuu alipata ujasiri wa kutoka mafichoni kama mshindi wa picha ya Kihindi, yaani Mithun ama Amitha ktk muvi zao enzi zao walipokuwa wakibamba sana miaka ya 1980s
 
Push up Inakwenda Kupigwa Kwenye Mkoa Ule Ule!! Subiri Uone 🙄😀😁
 
Kwahiyo hata TBC wanaokatiza hotuba za wapinzani wana wrong perception kwa wapinzani, so ndiyo?

Maana kwa mujibu wa maelezo yako ukali wa maneno unategemea na tafsiri ya mlengwa au msikilizaji na siyo kwa mujibu wa tafsiri ya jumla inayokubalika katika jamii..mkuu utakuwa haupo serious.
TBC wanakatiza kwa kuwa Chadema baadhi yao ni wahuni...baadala ya kuta gaza sera wao wanasema kitanuka mara sijui watalala barabarani...yaani Chadema wanahamasisha vurugu na uvunjifu wa amani ...Kama TBC watatangaza mambo hayo ina wanashabikia hayo...na mbaya zaidi TBC hata wao wanaweza kushitakuwa na mamlaka husika ikiwemo TCRA...
 
Mwaka 2015 wagombea wa CCM maeneo mbalimbali wakati wa kampeni walipiga Sana pushap. Mwaka huu nafuatilia kampeni lakini sioni dalili za wagombea kupiga pushap?

Nini kimefanya pushap kupuuzwa awamu hii?

Siku za Kampeni 'Kiratiba' ni 62 na ndiyo Kwanza 'Wagombea' wapo katika Siku za Tatu na wengine za Pili hivyo Siku za 'Pushapu' bado zipo nyingi.
 
TBC wanakatiza kwa kuwa Chadema baadhi yao ni wahuni...baadala ya kuta gaza sera wao wanasema kitanuka mara sijui watalala barabarani...yaani Chadema wanahamasisha vurugu na uvunjifu wa amani ...Kama TBC watatangaza mambo hayo ina wanashabikia hayo...na mbaya zaidi TBC hata wao wanaweza kushitakuwa na mamlaka husika ikiwemo TCRA...
Mkuu hoja yangu ya msingi ni IPI lugha Kali IPI so lugha Kali...
Kwa mujibu wa maelezo yako ni kuwa lugha kuwa kali ama sj Kali inatokana na perception ya MTU ..Mimi sikubaliani na wewe! Maelezo yako hayajitoshelezi..kuyatamka matiti ya mwanamke au kuwahamasisha wanawake wafanye ngono(yaweza kuwa zembe) ni ukakasi mbele ya jamii yetu kutokana na utamaduni wetu uliojaa staha.
 
Haihapita nchi zote zinazotuzunguka wanahaha nayo,Ulaya Wana haha nayo, Marekani wanahaha nayo sisi hao wazima wa afya tunadunda mitaani

Hata Ubelgiji Lisu alikotoka alitua na Libarakoa akadhangaa watu wako fit

Magufuli hiyo ya kumshukuru Mungu kea kutushindia corona Ni kick kwake kwa Mungu sio kwa watu ukiwemo wa Aina ya wewe

Mungu ndio huamua yupi anampa kick ya kumtukuza ampe utawala .Kick ya Magufuli Mungu kwake anaikubali atampa uraisi hata wewe usipompa kura sababu utawala hutoka kwa Mungu . Magufuli hahitaji kick yako mpagani wewe
Wenye akili zinazojielewa wamemuelewa sana kuanzia kipindi kile cha corona. Hawa wenye kuongozwa na dhihaka na utoto wa mitandaoni hawawezi kumuelewa.
 
Ndio maana tulishauri wagombea wapimwe akili zao kabla ya kuteuliwa🤔🤔😒😒
 
Magufuli lazima Mungu ampe Uraisi Ni Raisi pekee duniani ambaye anatamka wazi watu wamshangilie Mungu kwa kutushindia Corona Tanzania

Hafichi anasema Kama watu wanataka ushuhuda wa Mungu jinsi anavyoweza waje Tanzania waone ukuu wa Mungu

Hakuna Raisi popote duniani awe mfalme au Raisi aliyekiri uwezo wa Mungu mbele ya eating na ushahidi wa ushuhuda wa wazi wa ukweli Kama Magufuli

Kamtukuza Mungu na Mungu atamtukuza kwa kumpa uraisi.Sababu anataka Watu wote wamshukuru Mungu na kamtukuza kwa kazi kubwa aliyoifanya Tanzania na hampaki Mungu kwa sifa za uongo au za kutunga anampa sifa halisia sio fake au za kuandaa watu wamsifie

Uraisi Mungu atakupa Magufuli Hakuna nchi duniani hata Moja iliyoona God factor Ni muhimu kupambana na Corona umejipambanua pekee na Mungu .Wengine walifunga majumba ya ibada hata dini zilikotoka iwe Ulaya , Marekani , Uarabuni au Vatican nk ulikataa kuheshimu Mungu .

October 28 Mungu lazima atakupa uraisi kwa kumheshimu Mungu mikutano ya kampeni zako kwa kazi kubwa Mungu kalifanyia Taifa kuliokoa na janga la Corona

Wapinzani wako wao na Mungu kwenye Corona hawana muda wa kumsifu wanaponda tu!! Hawaoni kazi kubwa aliyofanya Mungu kwenye Hilo seals
Jiandae tu kuapishwa maana Mungu kakukubali sababu unakiri uwezo wake hadharani

Anza kushona suti ya siku ya kuapishwa
labda kama unamaanisha "miungu".

Mungu wa mbinguni hapendi watu wanaojulikana wawatume wasiojulikana kudhuru watu!
 
Hayo ameyasema raisi Pombe, muda siyo mrefu kwenye kampeni zinazoendekea mkoani Singida, nanukuu.

"Elimu ni bure, wakinamama zaeni hakuna haja ya kupanga uzazi, matiti ya kunyonyesha mnayo, wanaume wa kuwapeni mimba wapo."

Toa maoni je ni kweli kupanga uzazi hakuna maana kama wataalamu wanavyo shauri, hii siyo mara ya kwanza Magufuli kuwaambia watanzania kuwa zaeni, msipange uzazi.
Hii ni kweli kaisema mkuu!?
Mwenye kavideo tafadhali tuwekee sisi matomaso na tuliokosa.
 
Mwaka 2015 wagombea wa CCM maeneo mbalimbali wakati wa kampeni walipiga Sana pushap. Mwaka huu nafuatilia kampeni lakini sioni dalili za wagombea kupiga pushap?

Nini kimefanya pushap kupuuzwa awamu hii?
Waisraeli Wana kanuni yao kwamba mkakati uliofanikiwa haurudiwi
 
Back
Top Bottom