Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Katika hali inayoashiri mikikimiki ya Campaign, Mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi amepumzika kufanya kampeni.

Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa kampeni za Mwaka huu zimekuwa siyo nyepesi kama zilivyodhaniwa.

Magufuli ambaye mwaka 2015 alizunguuka kwa barabara nchi nzima, inaonekana dhahiri kuwa safari hii hawezi kuifikia rekodi ya mwaka huo. Safari hii inaonekana ameweka nguvu zaidi katika mikoa ya ukanda wa ziwa huku Wapiga kampeni wengine wakienda kanda nyingine.

Hata hivyo wapiga kampeni wake yaani Mama Samia na Kassim Majaliwa hawana mvuto mkubwa wa kisiasa wa kuweza kuchangia kura za maana kwa Magufuli.

Wakati huohuo mgombea wa Chadema Tundu Lissu ambaye ana faida ya kujinadi mapema makhsusi kwa ajili ya uchaguzi huu kwa kisingizio cha "kutafuta wadhamini" ameendelea kuchanja mbuga kwenye ngazi ya jimbo kwa jimbo baada ya kumaliza kupiga show kwenye ngazi ya kanda kwa kanda.

Sambamba na ngazi ya Jimbo kwa jimbo, Chadema watafanya mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanamng'oa Magufuli madarakani.

Bado haijajulikana kama kupumzika huku kwa mgombea wa CCM ni routine ya kawaida tu au uchovu au afya, tunangoja chama cha mapinduzi kitujuze zaidi.

View attachment 1567050
Ibilisi israel afanye kazi yake basi
 
Mwingine anaweza kusema mwaka 2015 alitumia nguvu kubwa na akapita maeneo mengi kwa sababu kazi ilikuwa ngumu hata matokeo ya Uraia yalisadifu hilo.

Mwaka huu kazi ni nyepesi mno, kila mtu anaona kinachotokea, mwitikio wa Raia kwake na kwa wapinzani wake. ACT wameshanyosha mikono, CHADEMA ndiyo Kama hivo, Juzi uliona Raia wa pwani Kama vile hawamjui, Jana Morogoro mjini umeona hali mwenyewe, kule Mheza ilikuwa aibu. Hata Makamanda tangu Mlivyoposti picha za Mbeya, hamjaposti tena, utafikiri Mgombea wenu yupo likizo naye.

Sasa kwa namna hiyo kwanini asipumzike Budha. Game imekuwa nyepesi mno.

Kama umegundua, wanachokifanya CCM baada ya uhakika wa Kushinda, ni kuhakikisha mtu anapata kipigo cha mbwa koko, hicho ndicho kinachofanyika kwa Sasa.
Tulivyoposti za MBEYA ulikubali. We muha wa hovyo sana. Kamsaidie Zitto kule anaangusha mbuyu kigoma. Acha kubwabwaja hapa. Hali ni tete kwa ccm. Zee lenu pumzi imekata wakati mwafaka kabisa
 
Kusema kampeni za CCM ni ngumu ni vichekesho. Rais Magufuli hata asipopiga kampeni kuanzia leo ushindi ni 90%

Rafiki zetu wa CHADEMA mtaula wa chuya huu mwaka hampati hata mbunge.

IMG_5160.JPG
 
Chama tawala katika kampeni hizi ndio kimehodhi vyombo vyote vya habari, mabango nchi nzima na wasanii wa kumwaga.

Jambo la ajabu timu yao ya kampeni ndiyo inatetemeka na kukosa formation ya wakifanyacho hadi kujikita kufanya faulo wakilindwa na vyombo vya dola.

Sasa hivi hata ilani yao wameitupa ni kudandia dandia Sera za vyama vingine.
Polepole na Bashiru kila mtu kivyake.
Wanakwama wapi?
Aliyeona bango hata moja mtaani kwake la Lissu anishtue nione.
 
ccm ndio chama pekee kinachofanya kampeni zake kisayansi na kujaribu kuwafikia wapiga kura
Ni jimbo kwa jimbo,kata kwa kata
Tundu lissu anatoka anaenda bagamoyo kwa helicopter!kilometa 60 tu,hapo kati kawaacha wapiga kura kibao
Kisayansi.....gharama kubwa kuhonga na kubeba watu ndio sayansi. Sayansi lazima iwe effective na efficient kupunguza gharama cheki mabango nchi nzima kila kona bilions of money zimesagika. Angalia TAL hata bango moja hakuna lakini anahenyesha watu hadi vichwa vinauma wameenda kunywa maji kwanza
 
Umesahau na lile kundi la wasanii 100! Huku wengine wakimtungia nyimbo zenye maudhui ya kabila lake.

Sababu Watanzania kwa umoja wetu tumeamua kwa dhati kabisa kuikataa CCM!
CCM imefanyiwa ukatili sana na watanzania yaani miaka mitano yote usingejua kama kuna upinzani. Wananchi wamepiga U-turn hadi Magufuli haamini
 
Chama tawala katika kampeni hizi ndio kimehodhi vyombo vyote vya habari, mabango nchi nzima na wasanii wa kumwaga.

Jambo la ajabu timu yao ya kampeni ndiyo inatetemeka na kukosa formation ya wakifanyacho hadi kujikita kufanya faulo wakilindwa na vyombo vya dola.

Sasa hivi hata ilani yao wameitupa ni kudandia dandia Sera za vyama vingine.
Polepole na Bashiru kila mtu kivyake.
Wanakwama wapi?
Wamegundua wananchi hatuwasikili, ilani yao imejaa ulaghai mtupu, eti ajira mil, 8, zitatoka wapi?
 
Wewe haumo utakuwa unalia na mademu zako wa Kinondoni kwa Mboka.
Mkuu hakuna anayetetemeka, siku tatu Rais Magufuli amepumzika nyumbani maana ushindi ni ni uhakika zaidi ya 95%

Upande wetu Chadema hali ni mbaya tumeamua tusombe watuView attachment 1567356
Hivi kwa akili yako, chama ambacho hakina fedha za wizi ndani ya serikali na kinawaomba wananchi wachangie gharama za kampeni hata kwa elfu elfu kinaweza katika limited funds kiasi hicho kuwakodia watu malori?
 
Chama tawala katika kampeni hizi ndio kimehodhi vyombo vyote vya habari, mabango nchi nzima na wasanii wa kumwaga.

Jambo la ajabu timu yao ya kampeni ndiyo inatetemeka na kukosa formation ya wakifanyacho hadi kujikita kufanya faulo wakilindwa na vyombo vya dola.

Sasa hivi hata ilani yao wameitupa ni kudandia dandia Sera za vyama vingine.
Polepole na Bashiru kila mtu kivyake.
Wanakwama wapi?
Matatizo yao ni kwamba, wamezoea kushinda kwa asilimia zaidi ya 50! Sasa wamepania kushinda 100% - ndiyo maana unawaona hawatulii!
 
Back
Top Bottom