Baada ya kushuhudia ya leo nimeamua kupiga kambi humu humu Chato ambapo kesho kuna burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii takribani 10 wakiongozwa na Harmonize, Juma Nature na Zuchu wakinogesha kampeni za urais za CCM
Awamu hii wasanii zaidi ya 100 wamegawanyika maeneo mbali mbali ya Zanzibar na Tanganyika kwaajili ya kunogesha kampeni za CCM ambapo kwa jana pekee huko Tanga mgombea ubunge wa Tanga mjini kupitia CCM Ummy Mwalimu alikuwa na wasanii kumi akiwa mgombea ubunge wa kwanza kutia fora kwa lundo la wasanii.