Nani kakwambia kuwa wote unaowaona hapo wanampenda Magufuli? Sisi ambao tumezaliwa na kukulia vijijini, tunajua maana ya kwenda kumwona uso kwa uso mtu ambaye siku zote umekuwa ukimsikia redioni ama kumwona kwenye TV. Yaani kwenda kushangaa. Na isitoshe, usijifanye kuwa haujasoma nyaraka za ofisi zikilazimisha watu kwenda kwenye mikutano ya Magufuli, shule kufungwa ili wanafunzi na walimu waende kwenye mikutano ya Magufuli. Na hata picha kuletwa hapa JF na mitandao ya kijamii. Na picha za watu kusombwa pia haujaziona? Na Mama Maria Nyerere naye haukumsikia? It is an artificial audience kwa ajili ya kampeni ya kisaikolojia. Otherwise, haina maana yoyote.