Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Habarini za Leo Wadau !!

Kwanza niombe *Jazba ziwekwe pembeni , Akili zifanye Kazi na Tushindane kwa Hoja siyo Vioja !!!!*

Binafsi niwakumbushe Wapenda SIASA Kuwa SIASA ni *Hesabu* !!! Kama Haujuwi Hesabu huu mchezo utakuua na Pressure.

Kwenye Kila Uchaguzi Kuna Wapiga Kura wa aina 3.

*1. WAPIGA KURA wa Chama Chako* ( Hawa kwa lugha nyepesi tunawaita wafia Chama ) Hawa huwa wanapiga Kura kwa kuangalia Ubora wa mgombea wao, Mvuto wake, imani yao kwake na mwisho ni MAPENZI yao ya dhati kwa chama Chao. Mara nyingi inyeshe mvua liwake jua hawa huwezi kuwapindua utachoka wewe tu !!

*2. WAPIGA Kura wa Chama PINZANI.* Hawa ni wafia Chama wa Itikadi yao. Wengi ni wapinzani wakutoka TUMBONI mwa mama zao au walikuwa wanufaika wa mfumo flani kwa hiyo huongezeka kulingana na namna Maslahi yao yalivyokwama. Hawa hata uwaletee *PEPO MAJUMBANI* kwao hawawezi kukukubali.

*3. WAPIGA Kura wasiyo na Vyama ( Un decided Voters )*

Hawa hawana Vyama, hawa ni Bendera fuata upepo na ndiyo Kundi linalochanganya saana. Kwa Kuwa kila Mkutano wa Mgombea wao huudhuria kwa Raha zao. Na ni kundi Muhimu sana linalofanya maamuzi kulingana na kushawishika na Sera, kuvutiwa na mgombea na mabadiliko ya dhati waliyoyashuhudia.

*TAKWIMU ZINASEMAJE SASA !!!!!*

Wapiga KURA wa Uchaguzi wa Mwaka huu 2020 inakadiriwa Kuwa wapo *Milioni 29.*

Hilo ndiyo *Kombe lenyewe la kugombaniwa ( Wapiga KURA )*

Kati yao *CCM pekee ina wanachama Hai MILIONI 17* achana na Wakereketwa na *WAFURUKUTWA* ambao idadi yao inaongezeka kila Siku.

Sasa hili ni Kundi la Kwanza Tu !!! Hawa Ni wafia CHAMA. watukane utakavyo watakufa na Chama chao.

Wanachama hawa wa CCM MWAKA HUU wakikipigia KURA pekee Chama chao bila ongezeka la KURA moja ya Upinzani *CCM na Magufuli watakuwa wameshinda kwa 58.62%*

Kwa hiyo *MAGUFULI , CCM* na *mtandao* wake mkubwa ambao upo kila Kitongoji na KIJIJI wanapambana Kuongeza Kura tu kutoka KUNDI la Watu wasiyo na VYAMA *( Undecided Voters)* ili kutunisha MFUKO wao wa USHINDI kupandisha asilimia (%) Tu !!!

Jambo ambalo linaendelea kuipa NAFASI KUBWA CCM Kushinda kwa KISHINDO. Hayo magoti ya *UNYENYEKEVU yanayopigwa na Mgombea wa CCM na Wagombea wengine wa CCM wa Ngazi mbalimbali Nchi nzima matokeo yake yataonekana kwenye SANDUKU la KURA muda mchache Ujao TAREHE 28/10/2020.*

Wapiga KURA wanahitaji *Maendeleo, Heshima, Kuthaminiwa , AMANI na Utulivu.*

Hayo yote CCM ndani ya Miaka 5 imeyafanya kwa Kiwango KIKUBWA ZAIDI !!!!

Narudia tena kusema, SIASA ya MAENDELEO *( Political Development)* na Siasa ya HARAKATI *(Political Movement)* kwenye SANDUKU la KURA, SIASA ya Maendeleo ndiyo inalipa zaidi.

" NALITAKIA TAIFA UCHAGUZI MWEMA "
Huna uhakika na idadi kamili ya wanachama wa ccm. Watanzania wote ni wanachama wa ccm na katika hao ni 29m tu ndio wamejiandikisha kupiga kura.

Vyama vingine wanachama wao ni raia wa nchi jirani.

Hivyo kwa hesabu hiyo ccm inaenda kushinda kwa asilimia 100% hasa ukizingatia Rais Magufuli anapendwa sana na watanzania.

Ukitaka kujua hilo angalia watu wanaohudhuria mikutano ya kampeni za vyama pinzani ni watu wachache sana ambao ni wageni kutoka nchi jirani wanaokuwa wamekuja kwa shughuli za kibiashara au matembezi tu.

Ndio maana mikutano yao inadoda huwezi kukuta wahudhuriaji wanazidi 50.

Sent from my A37f using JamiiForums mobile app
 
Bagbo wa Ivory Coast naye alitangazwa na NEC na CCM ya Ivory Coast, sasa ananyea debe
Wewe hata huelewi nini kilitokea Ivory Coast miaka hiyo

Ni hivi: electoral commission (NEC yao) ilimtangaza kwanza opposition candidate Alassane Ouattara kama mshindi wa urais. Then President Gbagbo akakataa na kukata rufaa. Read that again. Kule walikuwa wanaruhusu matokeo kuwa challenged mahakamani.

Japokuwa Constitutional Council ilioverturn earlier poll results na kumdeclare Laurent Gbagbo kama mshindi, Outtara alikomaa kinomaa na jeshi likamsupport kiaina.

Hapa bongo Dr. Mahera hatofanya kosa kumtangaza Lissu, afterall Katiba imemcover tayari. Huu ni ukweli mchungu.
 
Chadema watapigiwa kura na kutangazwa na Robert Amsterdam
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wewe hata huelewi nini kilitokea Ivory Coast miaka hiyo

Ni hivi: electoral commission (NEC yao) ilimtangaza kwanza opposition candidate Alassane Ouattara kama mshindi wa urais. Then President Gbagbo akakataa na kukata rufaa. Read that again. Kule walikuwa wanaruhusu matokeo kuwa challenged mahakamani.

Japokuwa Constitutional Council ilioverturn earlier poll results na kumdeclare Laurent Gbagbo kama mshindi, Outtara alikomaa kinomaa na jeshi likamsupport kiaina.

Hapa bongo Dr. Mahera hatofanya kosa kumtangaza Lissu, afterall Katiba imemcover tayari. Huu ni ukweli mchungu.
Wewe ngoja tu! Don’t panick
 
Habarini za Leo Wadau !!

Kwanza niombe *Jazba ziwekwe pembeni , Akili zifanye Kazi na Tushindane kwa Hoja siyo Vioja !!!!*

Binafsi niwakumbushe Wapenda SIASA Kuwa SIASA ni *Hesabu* !!! Kama Haujuwi Hesabu huu mchezo utakuua na Pressure.

Kwenye Kila Uchaguzi Kuna Wapiga Kura wa aina 3.

*1. WAPIGA KURA wa Chama Chako* ( Hawa kwa lugha nyepesi tunawaita wafia Chama ) Hawa huwa wanapiga Kura kwa kuangalia Ubora wa mgombea wao, Mvuto wake, imani yao kwake na mwisho ni MAPENZI yao ya dhati kwa chama Chao. Mara nyingi inyeshe mvua liwake jua hawa huwezi kuwapindua utachoka wewe tu !!

*2. WAPIGA Kura wa Chama PINZANI.* Hawa ni wafia Chama wa Itikadi yao. Wengi ni wapinzani wakutoka TUMBONI mwa mama zao au walikuwa wanufaika wa mfumo flani kwa hiyo huongezeka kulingana na namna Maslahi yao yalivyokwama. Hawa hata uwaletee *PEPO MAJUMBANI* kwao hawawezi kukukubali.

*3. WAPIGA Kura wasiyo na Vyama ( Un decided Voters )*

Hawa hawana Vyama, hawa ni Bendera fuata upepo na ndiyo Kundi linalochanganya saana. Kwa Kuwa kila Mkutano wa Mgombea wao huudhuria kwa Raha zao. Na ni kundi Muhimu sana linalofanya maamuzi kulingana na kushawishika na Sera, kuvutiwa na mgombea na mabadiliko ya dhati waliyoyashuhudia.

*TAKWIMU ZINASEMAJE SASA !!!!!*

Wapiga KURA wa Uchaguzi wa Mwaka huu 2020 inakadiriwa Kuwa wapo *Milioni 29.*

Hilo ndiyo *Kombe lenyewe la kugombaniwa ( Wapiga KURA )*

Kati yao *CCM pekee ina wanachama Hai MILIONI 17* achana na Wakereketwa na *WAFURUKUTWA* ambao idadi yao inaongezeka kila Siku.

Sasa hili ni Kundi la Kwanza Tu !!! Hawa Ni wafia CHAMA. watukane utakavyo watakufa na Chama chao.

Wanachama hawa wa CCM MWAKA HUU wakikipigia KURA pekee Chama chao bila ongezeka la KURA moja ya Upinzani *CCM na Magufuli watakuwa wameshinda kwa 58.62%*

Kwa hiyo *MAGUFULI , CCM* na *mtandao* wake mkubwa ambao upo kila Kitongoji na KIJIJI wanapambana Kuongeza Kura tu kutoka KUNDI la Watu wasiyo na VYAMA *( Undecided Voters)* ili kutunisha MFUKO wao wa USHINDI kupandisha asilimia (%) Tu !!!

Jambo ambalo linaendelea kuipa NAFASI KUBWA CCM Kushinda kwa KISHINDO. Hayo magoti ya *UNYENYEKEVU yanayopigwa na Mgombea wa CCM na Wagombea wengine wa CCM wa Ngazi mbalimbali Nchi nzima matokeo yake yataonekana kwenye SANDUKU la KURA muda mchache Ujao TAREHE 28/10/2020.*

Wapiga KURA wanahitaji *Maendeleo, Heshima, Kuthaminiwa , AMANI na Utulivu.*

Hayo yote CCM ndani ya Miaka 5 imeyafanya kwa Kiwango KIKUBWA ZAIDI !!!!

Narudia tena kusema, SIASA ya MAENDELEO *( Political Development)* na Siasa ya HARAKATI *(Political Movement)* kwenye SANDUKU la KURA, SIASA ya Maendeleo ndiyo inalipa zaidi.

" NALITAKIA TAIFA UCHAGUZI MWEMA "

Kwa nyongeza, CCM itavuna kura zaidi ya 90% katika ngazi zote (Urais, Ubunge na Udiwani) kwa sababu kuu zifuatazo:
√ Mgombea Urais kupitia CHADEMA anavvyoendelea kumdharilisha Mgombea Urais kupitia CCM, ndivyo chuki za wanaCCM dhidi yake zinavyoongezeka. Matokeo yake ni hasi kwa wagombea wote wa upinzani (Kura 17m ~ 58.62%);
√ Lugha anayotumia Mgombea Urais kupitia CHADEMA, kwenye kampeni ya kudharau mamlaka zilizopo Kikaytiba, inamnyima kura za kundi lisilo na vyama la watu wenye busara na hekima (3m ~ 10.33%);
√ ACT Wazalendo kumtosa mgombea wa Urais, ni usaliti. Kura za wafuasi wake na wapiga kura watakaoguswa, zitaelekezwa kwa CCM, alikokuwa awali (5m ~ 17.24);
√ Nguvu ya CCM kisiasa, kupitia Jumuiya zake (Wazazi, UWT, Vijana) ambazo wajumbe wake wanafanya kampeni nyumba kwa nyumba wakielezea mafanikio ya Serikali na ahadi mpya za chama (0.5m ~ 1.77%);
√ Isitoshe Watendaji wakuu wa Serikali (Makamu wa Rais na Waziri Mkuu) wanaendelea na kampeni wakijibu shutuma na hadaa za wagombea wa vyama vya upinzani kuhusu maendeleo huku wakitoa ahadi za kuaminika kutokana na rekodi nzuri ya Serikali kwa miaka 5 (1.5m ~ 5.77%)

Hii inatupa jumla ya 93.73% kama wote waliojiandikisha watajitokeza na kupiga kura. Hesabu hii inafuta kabisa madai ya upinzani, hasa CHADEMA, kuwa wataibiwa kura na kwamba vyombo vya Dola ni CCM.

Nami "NALITAKIA TAIFA UCHAGUZI MWEMA"
 
Wametumwa humu kujaza upupu wao. Wako wengi sana hawa nzi wa kujani!!!

Mie mwenyewe nilikuwa CCM na Nina kazi ya CCM ila sasa Niko na Lissu na Chadema. Na Tupo wengi sana karibu 70 ninaowajua tulio na msimamo huu

Hatuwezi kuchagua muuaji na mbaguzi Jiwe. Never
Watu tuko ccm ili tusiibiwe asset zetu , mfano mimi mama yangu ni Mwenyekiti wa UWC Bukoba lakini anapigiaga kura upinzani , the same na mimi Niko ccm na kadi ya ccm lakini nachaguaga cdm kila uchaguzi.
 
Having muujiza zaidi ya hapa ilipotufikisha hadi Korea imetuacha mbali sana
 
Ccm itashinda kwenye kura Za bao la mkono ila sio kura Za mioyo ya watu. Kuna mda inabidi chama kijitafakari watu wamewachoka waliokuwa ndani na hawasemi na waliokuwa nje hawana nguvu ya kuwaondoa ila mda unavozidi kwenda kuna kundi la tatu la system hili likiwachoka ndio ccm itaondoka madarakan wazungu wanasema ‘’Time will tell’’ napita tu mungu kaumba Akili sio Elimu
Sema umeichoka ww sio watu
 
Ccm bila system sio chochote si lolote ukitaka kushika nchi lazma ucheze na system sio watu hawa wanatumika kusupport tu yaliyopangwa na kuamuliwa n system hvo chadema kuchukua nchi bado sna ni mawazo tu ila wenye akili wamenielewa na wenye Elimu wameelewa
 
Kwa nyongeza, CCM itavuna kura zaidi ya 90% katika ngazi zote (Urais, Ubunge na Udiwani) kwa sababu kuu zifuatazo:
√ Mgombea Urais kupitia CHADEMA anavvyoendelea kumdharilisha Mgombea Urais kupitia CCM, ndivyo chuki za wanaCCM dhidi yake zinavyoongezeka. Matokeo yake ni hasi kwa wagombea wote wa upinzani (Kura 17m ~ 58.62%);
√ Lugha anayotumia Mgombea Urais kupitia CHADEMA, kwenye kampeni ya kudharau mamlaka zilizopo Kikaytiba, inamnyima kura za kundi lisilo na vyama la watu wenye busara na hekima (3m ~ 10.33%);
√ ACT Wazalendo kumtosa mgombea wa Urais, ni usaliti. Kura za wafuasi wake na wapiga kura watakaoguswa, zitaelekezwa kwa CCM, alikokuwa awali (5m ~ 17.24);
√ Nguvu ya CCM kisiasa, kupitia Jumuiya zake (Wazazi, UWT, Vijana) ambazo wajumbe wake wanafanya kampeni nyumba kwa nyumba wakielezea mafanikio ya Serikali na ahadi mpya za chama (0.5m ~ 1.77%);
√ Isitoshe Watendaji wakuu wa Serikali (Makamu wa Rais na Waziri Mkuu) wanaendelea na kampeni wakijibu shutuma na hadaa za wagombea wa vyama vya upinzani kuhusu maendeleo huku wakitoa ahadi za kuaminika kutokana na rekodi nzuri ya Serikali kwa miaka 5 (1.5m ~ 5.77%)

Hii inatupa jumla ya 93.73% kama wote waliojiandikisha watajitokeza na kupiga kura. Hesabu hii inafuta kabisa madai ya upinzani, hasa CHADEMA, kuwa wataibiwa kura na kwamba vyombo vya Dola ni CCM.

Nami "NALITAKIA TAIFA UCHAGUZI MWEMA"
Umesahau watumishi wote tumeitwa takataka tunahasira sana na huyu jamaa
 
Watu tuko ccm ili tusiibiwe asset zetu , mfano mimi mama yangu ni Mwenyekiti wa UWC Bukoba lakini anapigiaga kura upinzani , the same na mimi Niko ccm na kadi ya ccm lakini nachaguaga cdm kila uchaguzi.
Ccm haijawahi kuwa na wanachama kama ww, sema tu ukwer
 
Back
Top Bottom