Huna uhakika na idadi kamili ya wanachama wa ccm. Watanzania wote ni wanachama wa ccm na katika hao ni 29m tu ndio wamejiandikisha kupiga kura.Habarini za Leo Wadau !!
Kwanza niombe *Jazba ziwekwe pembeni , Akili zifanye Kazi na Tushindane kwa Hoja siyo Vioja !!!!*
Binafsi niwakumbushe Wapenda SIASA Kuwa SIASA ni *Hesabu* !!! Kama Haujuwi Hesabu huu mchezo utakuua na Pressure.
Kwenye Kila Uchaguzi Kuna Wapiga Kura wa aina 3.
*1. WAPIGA KURA wa Chama Chako* ( Hawa kwa lugha nyepesi tunawaita wafia Chama ) Hawa huwa wanapiga Kura kwa kuangalia Ubora wa mgombea wao, Mvuto wake, imani yao kwake na mwisho ni MAPENZI yao ya dhati kwa chama Chao. Mara nyingi inyeshe mvua liwake jua hawa huwezi kuwapindua utachoka wewe tu !!
*2. WAPIGA Kura wa Chama PINZANI.* Hawa ni wafia Chama wa Itikadi yao. Wengi ni wapinzani wakutoka TUMBONI mwa mama zao au walikuwa wanufaika wa mfumo flani kwa hiyo huongezeka kulingana na namna Maslahi yao yalivyokwama. Hawa hata uwaletee *PEPO MAJUMBANI* kwao hawawezi kukukubali.
*3. WAPIGA Kura wasiyo na Vyama ( Un decided Voters )*
Hawa hawana Vyama, hawa ni Bendera fuata upepo na ndiyo Kundi linalochanganya saana. Kwa Kuwa kila Mkutano wa Mgombea wao huudhuria kwa Raha zao. Na ni kundi Muhimu sana linalofanya maamuzi kulingana na kushawishika na Sera, kuvutiwa na mgombea na mabadiliko ya dhati waliyoyashuhudia.
*TAKWIMU ZINASEMAJE SASA !!!!!*
Wapiga KURA wa Uchaguzi wa Mwaka huu 2020 inakadiriwa Kuwa wapo *Milioni 29.*
Hilo ndiyo *Kombe lenyewe la kugombaniwa ( Wapiga KURA )*
Kati yao *CCM pekee ina wanachama Hai MILIONI 17* achana na Wakereketwa na *WAFURUKUTWA* ambao idadi yao inaongezeka kila Siku.
Sasa hili ni Kundi la Kwanza Tu !!! Hawa Ni wafia CHAMA. watukane utakavyo watakufa na Chama chao.
Wanachama hawa wa CCM MWAKA HUU wakikipigia KURA pekee Chama chao bila ongezeka la KURA moja ya Upinzani *CCM na Magufuli watakuwa wameshinda kwa 58.62%*
Kwa hiyo *MAGUFULI , CCM* na *mtandao* wake mkubwa ambao upo kila Kitongoji na KIJIJI wanapambana Kuongeza Kura tu kutoka KUNDI la Watu wasiyo na VYAMA *( Undecided Voters)* ili kutunisha MFUKO wao wa USHINDI kupandisha asilimia (%) Tu !!!
Jambo ambalo linaendelea kuipa NAFASI KUBWA CCM Kushinda kwa KISHINDO. Hayo magoti ya *UNYENYEKEVU yanayopigwa na Mgombea wa CCM na Wagombea wengine wa CCM wa Ngazi mbalimbali Nchi nzima matokeo yake yataonekana kwenye SANDUKU la KURA muda mchache Ujao TAREHE 28/10/2020.*
Wapiga KURA wanahitaji *Maendeleo, Heshima, Kuthaminiwa , AMANI na Utulivu.*
Hayo yote CCM ndani ya Miaka 5 imeyafanya kwa Kiwango KIKUBWA ZAIDI !!!!
Narudia tena kusema, SIASA ya MAENDELEO *( Political Development)* na Siasa ya HARAKATI *(Political Movement)* kwenye SANDUKU la KURA, SIASA ya Maendeleo ndiyo inalipa zaidi.
" NALITAKIA TAIFA UCHAGUZI MWEMA "
Vyama vingine wanachama wao ni raia wa nchi jirani.
Hivyo kwa hesabu hiyo ccm inaenda kushinda kwa asilimia 100% hasa ukizingatia Rais Magufuli anapendwa sana na watanzania.
Ukitaka kujua hilo angalia watu wanaohudhuria mikutano ya kampeni za vyama pinzani ni watu wachache sana ambao ni wageni kutoka nchi jirani wanaokuwa wamekuja kwa shughuli za kibiashara au matembezi tu.
Ndio maana mikutano yao inadoda huwezi kukuta wahudhuriaji wanazidi 50.
Sent from my A37f using JamiiForums mobile app