Hoja nzuri sana hiyo. Maeneo mengi ya Tabata viwanja ni high density. Yaani kuanzia sqm400(20*20) hadi sqm600(30*20). Utakuta nyumba ikisha simama basi kunakua hakuna eneo kubwa la wazi lililobakia kwa ajili ya shughuli nyingine
Finishing ya nyumba kwenye picha inaonekana iko sawa lakini kuna factors nyingine kama location na neighborhood (kama ni decent au la) n.k ni vitu muhimu kuangalia katika kupanga bei
Kumbuka mnunuzi ataanza kupiga hesabu ya 155m, je akinunua kiwanja kikubwa mahali na anze kujenga nyumba ya ndoto yake against kununua nyumba ipi itakua na advantage kwake na kw namna gani
Kibongobongo naona Real Estate Agents wengi wanfanya biashara ya property hasa real estate kama biashara ya kimachinga. Hawaweki bei kiuhalisia. Wanafanya kama wauza nguo au viatu barabarani. Anakuanzia bei ya kitu elfu 30 mwishoe anakuuzia kwa buku 5
Tena afadhali madalali wa magari maaana angalau magari yana bei zinazojulikana range yake kutegemea na aina, mwaka iliyotengenezwa, rangi, muonekano na uharaka wa muuzaji
Kwa maoni yangu muuzaji angeweka wazi Zaidi vitu ulivyomuuliza