Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Kama huwezi kukomenti bila kutukana mtu au kudhalilisha mtu, nendeni kwenye uzi wenu wa urusi unaonuka matusi. Hapa tunataka watu wanaojenga hoja kistaarabu. Haya maneo unaweza ukayaongea mbele ya TV au kisa upo online? Wafuasi wa urusi sijui mumepata malezi gani. Hamjui kujadili bila matusi. Nenda katukane kwenye thread yenu sio kuja hapa kuniharibia uzi kwa matusi yenu.
 
Ni vyema ukajikita kujibu hoja yangu ya: Ni nani alikuwa nyuma ya matokeo ya kura iliyopigwa? Je, kulikuwa hakuna shinikizo kwenye Uchaguzi(referendum)
Hebu fuatilia :- 1. Vikundi vilivyokuwa vinaendesha hujuma dhidi ya Ukraine vilikuwa vinapata wapi Uungwaji mkono(support), Silaha na uwezeshwaji katika kampeni za kuhamasisha chuki dhidi ya Ukraine?
2. Ukabila ni sumu. Ukabila ni kifungo katika Akili na Nafsi za watu.
Inakuwaje hivo? Ni hivi...Anatokea mpuuzi mmoja (Mtu binafsi au Serikali)na kuanzisha kampeni ya kuwaaminisha watu kwamba wanaonewa, wanadhulumiwa, Hawatendewi haki, wanafanyiwa ulaghai n.k.n.k.
Sio hivo tu, Mpuuzi huyo anaendelea kwa kuwarubuni baadhi ya watu(Kuwanunua) na kuwapa ufadhili-uchwara (i.e. anawageuza kuwa wasakatonge)na hao wasakatonge ndio wanaoendesha kampeni za kichini-chini na hamasa za kueneza chuki na wanaounda vikundi dhidi ya Serikali. Vikundi hivyo vinapewa mafunzo, silaha na ufadhili wa kifedha. Je, katika hali ya namna hiyo unategemea matokeo gani katika kura ya maoni?
Katika Ramani uliyoonesha hapo juu, hujiulizi ni kwa nini blue iko pembezoni tu na iwe ni katika mpaka na Russia?
Katika hali ya kawaida ukitenda kosa na ikathibitika hivo unawajibishwa. Sasa uwajibishwaji kwa makosa ya kisiasa upo kwa wingi eneo lenye rangi ya blue. Wao wanadai kunyanyaswa. (Mengine kasome mwenyewe huko......)
 
Mkuu, Wananchi wa Crimea wameandaliwa kwa muda mrefu hata kabla ya 2014 na wamepandikizwa chuki iliyokolea dhidi ya Ukraine kwa ufadhili wa Mrusi. Kwa maneno rahisi ni kwamba watu waishio Crimea wamewezeshwa kutaka kujitenga na Ukraine.
Kwa mantiki hiyo; Hiyo hali ya hewa chafu iliyopo ki-demokrasia, ukiendesha uchaguzi kwa namna yoyote ile hata iwe kwa usimamizi wa UN, matokeo hayatabainisha UHALISIA.
Kitu cha Msingi ni kwa Pande mbili husika (Russia na Ukraine) kutambua na kuheshimu mipaka baina ya nchi hizo iliyotambulika kiMataifa. Aidha; Ubabe, Vitisho na kupenyeza Vimitego vya maneno ya kichini-chini yenye uongo (Umbea) visiwepo au viepukwe kwani vinachochea mafarakano na kuanzisha mtafaruku wa kisiasa baina yao.
#Kwenye Paragrafu ya pili sikukuelewa - samahani mkuu.
 
Kuna sehemu badala ya Ukraine nimeweka Crimea,kiufupi namaanisha Fanya Crimea ingekuwa Russia,halafu Ukraine akaikimboa na ikapigwa kura!Wananchi wa Crimea wakaamua kuwa upande wa Ukraine!Unadhani msimamo wa US ungekuwa Crimea irudi Russia au wangewaunga mkono Crimea kujiunga na Ukraine?
Wakati unafikiria Hilo,angalia na suala la Taiwani na China!
 
Hoja nzito uliyoulizwa na hutaki kujibu ni hii

1. Uhuru Kenyatta akisema "watu wa mkoa wa Arusha wamesema wanataka wawe wakenya", wewe binafsi utakubali au Tanzania itakubali?
2. Uhuru Kenyatta akisema " Arusha ni territory ya Kenya na anataka kuikomboa" utakubali?

3. Kwa mantiki hiyo, "U.S au Ujerumani wakisema Arusha ni Ardhi ya Tanzania", na wakasema wako tayari kuisaidia Tanzania kutetea ardhi yao, kwako kuna nongwa/shida?.
 
Kwa kuwa Arusha kuna wamasai na Kenya wapo hivyo ni ethnicity moja so HE Uhuru anataka "kuikomboa" Arusha irudi Kenya wamasai wakaungane na wenzao.

Umetoa mfano wa karne Kiongozi! Short, clear, and to the point! Similar case to Crimea.
 
Watapima wenyewe; mm siwezi kuwasemea. Lakini busara itatumika kwa kujiuliza maswali haya:
1. Je, Crimea ni nchi inayotambulika kimataifa? Ni Mkoa au Jimbo halali la nchi gani?Ukraine au Russia.
2.Je, Kura iiliyopigwa haikuwa ni kura iliyojaa mizengwe au shinikizo kutoka nje au ndani i.e. Iliendeshwa na kusimamiwa na nani e.g. Tume huru kwa weledi na kihalali?
Kwa kuzingatia majibu yatokanayo na Uchunguzi kwa #1 na # 2, US angetulia au kuacha mambo yakae kama yalivyo - hatakuwa na sababu ya kuingilia.. Lakini pia Kumbuka siasa ni mchezo mchafu.
Kwa habari ya China na Taiwan sina details ya kinachoendelea ila najua kuna sintofahamu fulani.
 
Hapa ni Kyiv jana katika Sherehe za Uhuru. Urusi wanaumia kuona Ukraine wanafurahi. Wapo pamoja na hawaogopi. Mrusi si chochote. Alisema atafika Kyiv na kuiteka ndani ya Siku 3,lakini huu ni mwezi wa 6, wameshinda hata kuikatia umeme tu achilia mbali kuipiga makombora
Your browser is not able to display this video.
 
Mvamizi kutoka Urusi amekamatwa akiwa anabaka Kondoo. Anajeshi wa Ukraine walimuona kupitia thermal scope. Walipomshitua akakimbia bila kujali kashazungukwa
Your browser is not able to display this video.
 
Mvamizi kutoka Urusi amekamatwa akiwa anabaka Kondoo. Anajeshi wa Ukraine walimuona kupitia thermal scope. Walipomshitua akakimbia bila kujali kashazungukwa
View attachment 2334018
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hawajapata hiyo kitu miezi 6 sasa. Jamaa kakatizwa game lake. Hatari πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ngome ya Frontline ya Ukraine ni Imara. Urusi wameshindwa kabisa kusonga mbele. Wameaza kurudi nyuma hatua moja moja. Hii sehemu yenye rangi nyekundu ndo tumebakiza kuikomboa. Sehemu ya Ukraine iliyobaki ipo chini ya majeshi ya Ukraine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…