Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Nikusahihishe kidogo. Sababu iliyowafanya Russia washindwe kuiteka Kiev mojawapo ni hizi.

1. Ukraine walibadili mbinu za kivita kutoka kwenye kutumia vifaru vya ki soviet na kutumia zaidi Javelin missiles (Portable missile Launcher) za mwingereza ambazo zilipukutisha vifaru, helicopita na Artillery nyingi za Russia. Wanajeshi wa Ukraine waliingia nazo mstuni na kuwasubiria warusi.

2. Drone ziliwasaidia sana kuangamiza tanks za Russia na kuwaua wanajeshi wa Russia walioanza kukimbia hovyo huku hawajui waelekee wapi sababu ya ugeni wa eneo. Askari wengi sana waliuawa.

3. Kikosi cha anga kilipambana sana kuilinda Kiev

4. Jiografia ya Kiev pia ilichangia warusi kushindwa kuingia. Ukraine troops waliwavizia kwenye maeneo ambayo lazima wangepita na kuwaangamiza.

5. Rais Zelenskyy aligoma kuondoka Kiev, alikuwa yuko tayari kufia Kiev. Hili nalo lilisaidia maana Ukraine troops waliimarisha ulinzi kwa Kiev zaidi.

Hizi ni baadhi ya sababu zilizochangia Russia kushindwa kuingia Kiev.
 
Urusi leo wamepoteza ndege mbili na Helkopta mbili. Safi sana
View attachment 2620308
Slava Ukraine [emoji1255]
 
Urusi leo wamelipua ndege zao nne
View attachment 2620523
Air defense systems zao itakuwa zimekuwa hacked na pengine hawajajua. Wanazirusha zinabutuliwa halafu wanasema zimepata hitilafu ya engine.

Hiyo coincidence ya ndege 4 kupata hitilafu ya engine zikiwa angani ndani ya siku mbili TASS na RT inabidi watusimulie vizuri πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Walianza kuzusha propaganda eti ndege mbili za Ukraine zimetunguliwa. Naona unga umezidi maji πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…