Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

20230513_153732.jpg
 
Fanfa hii vita imenifundisha mambo mengi sana.

Kwanza niliwaza ni kwa nini Russia alifika hadi kwenye viunga vya Kiev lakini akatoka. Nilichokuja kufahamu kuwa alikuja kugundua teknolojia ya vita imebadilika pale misafara yake ya kijeshi ilivyopigwa picha toka angani.

Leo ule "Usupa Pawa" wa kuwa na vifaru na ndege kadhaa za kivita unaonekana hauna maana mbele ya nguvu ya Drone.

Hii vita watu wa NATO wanaitumia kutesti mitambo yao.
Nikusahihishe kidogo. Sababu iliyowafanya Russia washindwe kuiteka Kiev mojawapo ni hizi.

1. Ukraine walibadili mbinu za kivita kutoka kwenye kutumia vifaru vya ki soviet na kutumia zaidi Javelin missiles (Portable missile Launcher) za mwingereza ambazo zilipukutisha vifaru, helicopita na Artillery nyingi za Russia. Wanajeshi wa Ukraine waliingia nazo mstuni na kuwasubiria warusi.

2. Drone ziliwasaidia sana kuangamiza tanks za Russia na kuwaua wanajeshi wa Russia walioanza kukimbia hovyo huku hawajui waelekee wapi sababu ya ugeni wa eneo. Askari wengi sana waliuawa.

3. Kikosi cha anga kilipambana sana kuilinda Kiev

4. Jiografia ya Kiev pia ilichangia warusi kushindwa kuingia. Ukraine troops waliwavizia kwenye maeneo ambayo lazima wangepita na kuwaangamiza.

5. Rais Zelenskyy aligoma kuondoka Kiev, alikuwa yuko tayari kufia Kiev. Hili nalo lilisaidia maana Ukraine troops waliimarisha ulinzi kwa Kiev zaidi.

Hizi ni baadhi ya sababu zilizochangia Russia kushindwa kuingia Kiev.
 
1. Ndiyo maana mimi huwa nasema vita hii haiwezi kuisha mapema sababu mojawapo ni kwamba Ukraine inatumika kama testing field ya military equipment. USA & German wana test Technology zao. Kama zina weakness wataziboresha (Upgrade the software) na kuendelea na testing.

2. Wanaume hawa (German & USA) wakiamua kumaliza vita ndani ya miezi 3 wanaimaliza. Ila wanataka wamjue adui ana nini. Wanajua ana nini ila wanataka ku prove alichonacho kina uwezo gani?

3. German katoa package nyingine ya IRIS-T nne (4), Leopard kadhaa na machine zingine. USA naye hivi karibuni katoa package yenye air defense systems nyingi likely Patriots.

4. Swali nalojiuliza, Russia atahimili wave ya silaha hizi kama amefikia hatua ya kuomba silaha kutoka South Africa?
Urusi leo wamepoteza ndege mbili na Helkopta mbili. Safi sana
View attachment 2620308
Slava Ukraine [emoji1255]
 
Urusi leo wamelipua ndege zao nne
View attachment 2620523
Air defense systems zao itakuwa zimekuwa hacked na pengine hawajajua. Wanazirusha zinabutuliwa halafu wanasema zimepata hitilafu ya engine.

Hiyo coincidence ya ndege 4 kupata hitilafu ya engine zikiwa angani ndani ya siku mbili TASS na RT inabidi watusimulie vizuri 😂😂😂

Walianza kuzusha propaganda eti ndege mbili za Ukraine zimetunguliwa. Naona unga umezidi maji 😂😂😂
 
Back
Top Bottom