SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Iran inavyopiga makazi ya RAIA kule The Aviv ni sahihi?
Alieanza mashambulizi ni Israel, hivyo Iran inajibu kwa self defence.

Ndo maana Marekani na West hawawezi kuingia kwenye hiyo vita sanasana wataendelea kutoa msaada wa vifaa.

Lakini mkutano wa G7 umetoa azimio la kusitisha vita.

Ukweli wabakia kuwa hapo Aggressor ni Israel.

Kupiga hadi kituo cha TV ni desperation ya Israel kwamba kwamba Marekani aingine lakini Trump amekataa.

Ipi ni justification ya kupiga kituo cha televisheni?
 
Israeli yashambulia televisheni ya taifa ya Iran baada ya kutoa agizo la wananchi kuondoka Tehran
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema awali kuwa Israeli imedhibiti anga ya Tehran, jambo alilolieleza kama β€œmabadiliko katika kampeni nzima”.


Makombora ya Israeli yamepiga kituo cha televisheni ya taifa ya Iran kilichopo Tehran, baada ya Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) kutoa agizo kwa raia kuondoka katika eneo fulani la mji mkuu huo.


Shambulizi hilo lilisitisha kwa muda matangazo ya moja kwa moja, huku mtangazaji akiondoka ghafla wakati studio ilipojaa moshi.


Shambulizi hilo lilitokea muda mfupi baada ya IDF kuitaka jamii kuondoka katika maeneo ya Wilaya ya Tatu ya Tehran, ambako ndiko studio hiyo ya televisheni ilipo.


β€œKatika saa chache zijazo, jeshi la Israeli litafanya mashambulizi katika eneo hili dhidi ya miundombinu ya kijeshi ya utawala wa Iran... uwepo wenu katika eneo hili unaweka maisha yenu hatarini,” IDF ilichapisha kwenye X.


Netanyahu aliongeza kuwa Israeli iko β€œkatika njia ya” kuangamiza mpango wa nyuklia wa Iran na uwezo wake wa makombora ya masafa marefu.


Wakati mzozo kati ya mataifa haya mawili ya kikanda ukizidi kupamba moto, waokoaji wa Israeli walisema watu wanane wameuawa kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran kwenye miji ya Israeli, na kufanya idadi ya waliouawa tangu Ijumaa kufikia 23.


Mamlaka za Iran zilisema jioni ya Jumapili kuwa raia 224 wameuawa kutokana na mashambulizi ya Israeli, pamoja na maafisa 17 wa juu wa kijeshi.


Mashambulizi haya ya hivi karibuni yametokea wakati viongozi wa kimataifa wakiwasili nchini Canada kwa ajili ya...
 
Kuua raia wa Israel ni ushujaa sio? Hicho kimama kinaongea kibabe lakini kumbe kinaogopa kifo
Huyo mtangazaji ni maarufu sana Iran na hicho ndicho kituo chao wairan.

Hapo alikuwa akitoa ujumbe kwa wairan kwamba Ukweli ni lazima uonyeshwe.

Israel watumia playbook ileile ya Gaza kutotaka uhuni wao uonyeshwe ndo maana wamepiga marufuku hakuna Media kule Gaza.
 
Kumbe Iran Bado Ina Air defense system zinafanya kazi?
Si mlituambia zote zimebutuliwa?
Mkuu Waajemi kichwa sana!! Walitafuta mbinu za kuwachota akili Wayahudi wakatengeneza rada ambazo zilikuwa ni Matoyi tu yaani DECOYS, wakahakikisha zinatoa mawimbi ya radio kama RADA alisi kabisa, kumbe hiyo ilikuwa ni gheresha tu, wakajengea na minara ya kushikiria madishi ya kusambaza mawimbi kama ya RADA - sasa ndege za wayahudi zilipokuja no kudetect hayo mawimbi no kuona madishes na minara wakafikiri ni air defense systems za jeshi la anga LA Iran wakadondosha mabomu na pia air to ground missiles,wakajipongeza kwamba kwamba hivi sasa Iran hawana Air defense system zozote, kesho yake wakaingia kichwa kichwa no F-35 wanayo sema no stealth ikatunguliwa, hawakuamini kesho kutwa yake wakaja no F-35 zikatunguliwa mbili, hivyo jeshi la anga la Iran lilifanikiwa kutungua jumla ya ndege 3 aina za F-35, mmoja.wa rubani alikuwa mwanamke.
 
BREAKING: IRAN HAS VOWED TO CARRY OUT A RETALIATORY TV STRIKE ON ISRAEL’S CHANNELS 12 AND 14THE IRGC HAS ISSUED A WARNING STATING THAT CIVILIAN EMPLOYEES AT ISRAELI TV CHANNELS SHOULD LEAVE THEIR OFFICES



Kama una ndugu yako anafanya kazi kwenye hivyo vituo vya TV, mtaarifu asifike kazini... kimondo kinatua hapo.. tusije kulaumiana..
 
Check ulivyo muongo we jamaa hakuna media inayoripoti mambo yanayoendelea Gaza?
 
Umeamini hiko kilichoandikwa hapo?
 
Kobazi ni waongo hatari πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Alitaka mpaka aone Iran anarusha mabomu ya nyuklia ndio ajue wapo karibu kutengeneza?

Alitaka mpaka aanze kuifuta Israel ndio ajue kuwa anaanzisha vita kuifuta Israel?

Tangazo tu la Iran kuifuta Israel ni ushahidi tosha na ni tangazo la vita. Iran analea na kufadhili makundi ya kuifuta Israel, unategemea

Sikutegemea nchi kama UK inaweza kuwa na balozi kilaza namna hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…