SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Oya Iran wamedhamiria aisee.
Naona hawataki masihara.
Ni noma aise. Iran amesema bado ataongeza nguvu ya mashambulizi kadri muda unavyozidi kwenda.

Kwa maana nyepesi kipigo cha jana na leo alichomfinya Israel ni cha mtoto.

Muajemi ni next level aise.

Fikiria Israel anasaidiwa na mabwana zake USA, Ulaya na baadhi ya nchi za kiarabu wanafiki lakini hakuna wanachofanikiwa vyuma vinapiga target kama vilivyoagizwa.😆
 
Najiuliza ingekuwaje kama Israel peke yake angesimama vitani na Iran?

Kama hivi tu anasaidiwa na mabwana zake kuanzia ulinzi wa anga hadi silaha lakini kipigo kipo pale pale, vipi angekuwa peke yake kama Iran alivyosimama peke yake?
Vita yoyote lazima kusaidiana hata Tanzania tulisaidiwa na Algeria na Msumbiji
 
Huko Haifa, Israel kiwanda cha kusafisha mafuta kimekung'utwa vibaya na makombora kinawaka moto.

Iran uwezo wa kupigana vita vya muda mrefu anao shida Israel plus mabwana zake hawana pumzi ya kupigana muda mrefu.

Pale Gaza tu mwaka wa pili huu anahangaika na wanamgambo ambao wanatengeneza magobole kienyeji na bado hajawapata mateka.

Halafu ndiyo upambane na Iran mwenye teknolojia ya juu kabisa ya zana za kivita?
 
Israeli ni wapumbavu sana, hii itamsaidia nini? Ukiuwa kiongozi anachaguliwa mwengine, Iran anapiga miundo mbinu, huwezi kushinda vita kwa kuuwa viongozi.
 
Safari hii inaonekana Israel imeumia seriously.
Sio kawaida Trump akurupuke kupiga simu Urusi ghafla.
Na inasemekana Putin ameshindwa mshawishi Iran,Iran wanasisitiza mapigano kuendelea na wanasema wao ndio wataomaliza.
Aliyepiga simu ni putin sio Trump au mimi ndio sielewi English vizuri
 

Attachments

  • Screenshot_20250615-074459.jpg
    189.9 KB · Views: 26
Kuna mtu nilimwambia Israel ashukuru sana yuko mbali na Irani.

Angekua karibu na Iran kama alivyo karibu na Syria lebanon au Misri angepasuka sana.

Mana zile shaheed drones zisingekuwa zinatembea umbali mrefu ni mwendo wa kuzimimina tu chap kwaa zipo Tel Aviv.

Ashukuru yupo mbali na Iran hiyo inamuokoa kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…