SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Kwani netanyahu katoka mapangoni?
Netanyau yuko hadharani, anaendelea kuonekana Live 24/7, madevu akirogwa aaze ku-chart na kisimu chake huko pangoni amekwisha, so yuko kipweke sana, and they know exact location aliko, ila wanamwacha ateseke kisaikolojia kwanza😀
 
Mimi Nina uhakika nimekuzidi elimu ya darasa.
Uhakiko huo ninazo.

Kwa akili yako unafikili radiation zinasambaa nchi mzima.

Heroshima Japan ilipigwa na nuclear radiation zilisambaa nchi mzima???
Tena nchi ya Japan ni dogo sana, na iran ni kubwa sana
Basi mfumo wetu wa elimu unachangamoto
 
mifumo ya nyuklia ya iran iko scattered, unakuta unit hii iko mkoa huu, unit hii mkoa ule.. so kumaliza mfumo mzima kwa vilipuzi sio kazi rahisi..pia inawezekana kwamba inahitaji mabomu yenye nguvu kubwa ambayo ni heavy sasa ungeyapitishaje kinyamela?
Umejenga hoja nzuri..
Lakini hivi vinu ilikuwa rahisi zaidi kuvilipua ukiwa kwa ndani, yaani kwa ndani hata vilipuzi vya kawaida vingeweza kufanya uharibifu mkubwa..
 
Iran imeanza mashambulizi makubwa ya makombora dhidi ya Israel, ambayo yamelenga miji mikuu ikiwemo Haifa na Tel Aviv. Viwanda vya mafuta na kemikali, kama Bazan Group, vimeharibiwa vibaya huku moto mkubwa ukiripotiwa.

Wimbi la pili la makombora limeanza kutua, na majengo kadhaa mjini Tel Aviv yamepigwa, watu 15 wakijeruhiwa. Taarifa za vifo pia zimeanza kuripotiwa kutoka maeneo mbalimbali ya Israel.

Pakistan imetangaza kuwa itaishambulia Israel kwa nyuklia endapo Iran itashambuliwa kwa silaha hizo, na iko tayari kuingia vitani upande wa Iran iwapo mataifa ya Magharibi yataingilia moja kwa moja.

Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Israel (Shin Bet) ameripotiwa kujiuzulu kufuatia hali hiyo ya taharuki.

UPDATE:
Mpaka muda huu miji yote ya Israel imeshambuliwa na Iran na taarifa za vifo huko Israel zimeanza kutoka

UPDATE:
Israel imetoa onyo la kuwataka wakazi wa eneo la Manispaa lililoko kaskazini-mashariki mwa jiji la Tehran waondoke haraka kabla ya mashambulizi ya anga.

Kupitia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kwa lugha ya Kiajemi na Kiarabu, msemaji wa jeshi la Israel, Avichay Adraee, alisema jeshi litashambulia eneo la(District C)ikiwa na lengo la kulenga miundombinu ya kijeshi ya Iran.

“Uwepo wenu hapo unaweka maisha yenu hatarini. Kwa usalama wenu, ondokeni mara moja,” alisema Adraee.

Eneo hilo lina taasisi muhimu za serikali, ofisi za umma na mashirika ya mawasiliano na ujasusi.

Taarifa ya jeshi la Israel ilisema kuwa ndege zake za kivita zimeshambulia malori yaliyokuwa yamebeba silaha na makombora, yakielekea Tehran kutoka magharibi mwa Iran.

UPDATE:

Iran yashambulia hospitali Israel


Kombora lililorushwa kutoka Iran limelenga hospitali kuu ya Beersheba Kusini mwa Israel na kusababisha majeruhi kadhaa, huku makombora mengine yakipiga majengo mawili Tel Aviv na kujeruhi watu 40. Israel imejibu kwa kushambulia mtambo wa urutubishaji nyuklia wa Iran.

Waziri Mkuu Netanyahu ameapa kulipiza kisasi, akisema madikteta wa Iran wataadhibiwa kwa matendo yao.

Iran wakapige ktk military bases za israel sio kwenye supermarkets.. vinginevyo, hawashindi hii vita hata jwa asilimia 2.
 
Back
Top Bottom