SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Iran na Israel, nani taifa la Mungu?
 
Kuna watu wanajitoa ufahamu kukejeri jinsi anga la Iran linavyopitika na ndege za kivita za Israel na shoga yake USA. Ila wanashindwa kutambua kinachotokea upande wa pili ambapo Israel naye anapigika tu na missile za Iran utadhani Iron dome imeenda likizo.

Nakumbuka hii Iron Dome imekuwa ikisifiwa sana kuwa inadaka hata nzi wenye itikadi/imani ya kiislamu kumbe propaganda tupu!
 
Irone demo imeshidwa.
Ule mfume umedesign kustop shells,
Na rocket zile kama hamas and Hezbollah na sio ballistic missile na hypersonic missile.


Ballistic missile ni kubwa sana ni ngumu kuzuia.
Arrow ndo ilitengenezwa kwa ajili ya ballistic missile lkn nayo imeshindwa kufanya kazi vizuri.

Anyway hakuna air defense system upo sahihi 100%.

Maana hata za iran nazo zimefeli.
Na S300 za urusi uko iran.
 
Tangu tumeanza kuripotiwa taarifa za kulipuliwa Iran, tulitegemea kwa sasa taifa lao liwe kwenye hali ya nusu kuanguka ila ndio kwanza na wao wanajibu mapigo.
Mkuu kuanguka taifa sio suala dogo, hata Israel inavyoshambuliwa haiwezi kuanguka hivyo unavyofikiri
Russia amepiga sana Ukraine mwaka.wa 3 huu unahisi kwa nn Ukraine haijaanguka?
 
Tangu tumeanza kuripotiwa taarifa za kulipuliwa Iran, tulitegemea kwa sasa taifa lao liwe kwenye hali ya nusu kuanguka ila ndio kwanza na wao wanajibu mapigo.
Iran ni nchi kubwa sana sio rahisi kuipindua.

Afu uwezi angusha serikali ya nchi nyingine kwa attack za anga.
Jeshi la ardhini tuu ndo linaweza kufanya hivyo.
 
Tatizo ni hayo matango pori ya SUCCESSFULLY INTERCEPTED tokea upande wa yahudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…