SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Iran hana ICBM yoyote. Hata Israel haina true ICBM ila ina intermediate range ballistic missile Jericho-3 specifically kama nuclear tu sio conventional warhead.

Iran hana uwezo wa kushambulia direct ndani ya US. Na mara ya mwisho US anashambuliwa direct na adui ni Pearl Harbour mwaka 1942 ambapo alitangaza vita na mobilization kubwa.
Iran hana ubavu wa kukabili hiyo hasira ya raia American public. Angalau ashambulie US bases za Middle East na penyewe atapigwa ila kwa huruma kidogo sababu litawahusu wanasiasa na jeshi tu, ila ukigusa raia mara wakaandamana vita itangazwe unakuwa umefanya maamuzi ya akili fupi.
Ni nchi chache sana zenye makombora ya mabara, Marekani, Urusi, China, India,N.korea, Ufaransa, na Uingereza tu.

Kuhusu vita inayo endelea maoni ni kuwa Iran ina silaha nzuri sana za kupambana na maadui zake hilo uhitaji kuvaa miwani kuliona tukiondoa ushabiki ila ina Intelegensia ya hovyo kabisa inayo hitaji marekebisho makubwa sana.

Kitendo cha Mifumo ya ulinzi ,majenerali, wanasayansi kuuliwa na drone kutoka ndani ya Iran kwenyewe unadhihirisha hilo.
 
No moja ya sababu ameamua akadeal na chanzo cha huo mgogoro, Iran.
Mbona na Iran napo kashindwa kufanya regime change, kashindwa kuharibu nuclear project, halafu Hamas walkatzwa na Iran kuhusu Oct 7, Iran haikuwatuma Hamas wakavamie Oct 7... Israel imeshindwa kila kitu..
 
Marekani ni nchi yenye nguvu huwezi kuamini majeshi yote duniani yanaweza yakakusanyika lakini marekani ikiamua kutumia nguvu zake zote haizidi masaa 24 dunia inakuwa unga. Hamna mwenye sauti juu ya marekani
Mkishiba Makande huwa mnaropoka Chochote kinacho kuja kichwani, bila kufikiria na kufanya analysis yoyote.

Kwa akili yako ndogo hii Marekani huo uwezo autoe wapi? Korea pale ameshindwa kupagusa, Pakistan na Venezuela palimtoa jasho mpaka akaamua kukimbia vitani, aje apambane na Dunia ambayo ina Most powerful countries kama China, Russia hapo baado kule south America.

Punguzeni uropokaji tafute information, msilishwe hizo propaganda.
 
Ila mtaalam unasource za maana sana
Huyo jamaa ni noma sana kaja kuwaokoa sana wagalatia humu ndani kawafanya kobazi waishi kinyonge sana

Utasikia tu ana report Israel anashambulia kwa makombora mda huu magharibi mwa Tehran MLIPUKO MKUBWA SANA

Iran katuma drone huu pale Jerusalem sema zimekuwa intercepted
 
Trump naona anatupa Taulo

1750709699255.png
 
Walichukua mateka zaidi ya 300, hadi sada wamesalia mateka 53, habari zako unazitoa wapi jamaa?
Ilikuwaje mateka waliokuwa na Hamas walipigana pale pale Gaza, maeka wapo pale pale, kieneo ukubwa wa kata, lakini wamezungushwa hadi wakakubali kubadilishana mateka?

Hao Hamas wenyewe hawana ndege vita, hawana kifaru, satellite, hawana hypersonic, wana bunduki na maroketi ya kutengeneza kienyeji... ilikuwaje IDF ika kubali kuingia makubaliano ya kubadilishana mateka, hio intel yao ilishindwa kubaini mateka pale Gaza?
 
Trump, ni mzuri sana wa maneno hasa pale anapokutana na mtu ambaye ni dhaifu, mtakubaliana na mm Kipindi Cha Kampeni na interview alizofanya na Kamara. Anajua namna ya kucheza psychology za watu.
Mtu wa aina hii ni ngumu sana kumuamini coz vitu vingi anaongea Ili kumdhofisha adui kwa maneno.

Ila naamani round hii kachezea pabaya , kama alifikiri kufanya vile kumshambulia muajemi ndiyo kumuangusha basi amejidanganya , mwarabu ni aina ya watu wenye mioyo na Imani ngumu sana siyo rahisi kukubali kumaliza vita, rejea Hamas, Hezbollah, Osam Bin Laden wakina Sadaam Hussein Marekani anajua ugumu wao round hii kajichanganya hato amini.

Kile alicho mwambia Zelensky anacheza na WWIII Sasa yeye ndiyo anachofanya.
 
Back
Top Bottom