Ni kweli kabisa Israel Inajiandaa kwa shambulio kubwa nchini Iran
Idara ya ujasusi ya Israel imechunguza harakati zinazolenga kurejesha mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran na kuweka upya virusha makombora. Tangu kumalizika kwa Operesheni Rising Lion, kumekuwa na mabadiliko yanayoonekana katika shughuli za Irani karibu na vifaa vya nyuklia. Hapo awali, hii ilihusisha kukarabati njia za kufikia sehem zilizoharibiwa katika shambulio la awali. Walakini, katika siku za hivi karibuni, vyanzo vya kijasusi vimegundua juhudi za kuchimba urani na kuanza kurejesha vifaa hivyo.
Tathmini za Israeli zinaonyesha kuwa baadhi ya sehem hazikuharibiwa kikamilifu na kwamba shambulizi lenye nguvu zaidi linahitajika ili kuzima kabisa ndoto za Iran Kwa sababu hiyo, Israel inajiandaa kwa mashambulizi mengine makubwa zaidi.