SPECIAL THREAD: Yanayojiri kwenye Mgogoro wa Israel na Iran na hatma yake kwenye siasa za dunia

Naomba unisadie Iran kapiga na nchi ngapi mpaka sasa na Israel kapigana na nchi ngapi mpaka sasa?
Wazee wa kutafuta sababu wakishindwa vita hawakosi visingizio!!

Ili na wewe upate faraja basi tufanye Israel inasaidiwa na nchi za Marekani,Ulaya na Afrika na Iran yeye anapigana peke yake. Naona hapo unafurahia sana sana!!!
 
#BREAKING Pakistan has closed its border with Iran
 
Hakuna kitu kama hicho mkuu.
Anaongea ndoto ambayo ngumu kutimia.
Acha tuone wakina Netanyahu ni wehu hawashindwi kufanya jambo kama hilo.

Ila Iran sijui niseme ipo uchi ama imevurugika ama imeingilika vibaya mno na Mossad aloo Iran ina hitaji usafishwaji mkubwa hasa kwenye jeshi na vitengo vya usalama maana ina ingilika mno na Israel.

Pia Iran ina hitaji msimamo thabiti utakao eleweka wanataka mazungumzo ama wanataka Nyuklia japo mimi naona wanapaswa kuwa nazo kinyume na hapo kufikiri marekani na washirika wake wa magharibi wana mchekea atakuwa anakosea.

Usalama wa utawala wa kiimani wa Iran kwa sasa jukumu ni kuimarisha jeshi kwa vyovyote vile watakavyo weza na kwa silaha zote zile ambazo maadui zake wanazo na hata wasizo kuwa nazo sometimes namuelewa Kim na North Korea yake
 
Baada ya mashambulizi ya awali yaliyolenga safu ya juu ya uongozi wa kijeshi wa Iran — yakiwemo kuuawa kwa Mkuu wa Majeshi pamoja na wanasayansi wakuu wa mpango wa nyuklia — serikali ya Tehran imekuwa ikichukua hatua za tahadhari kwa kuhamisha baadhi ya viongozi waliobaki katika maeneo ya siri yenye ulinzi wa hali ya juu.

Katika mwendelezo wa mashambulizi yenye usahihi wa hali ya juu, vikosi vya Israel leo vimetekeleza oparesheni iliyolenga chumba maalum cha siri ndani ya jengo la Wizara ya Intelijensia, ambapo viongozi wawili waandamizi wa ujasusi wa Iran walikuwa wakijificha: Waziri wa Intelijensia, Brigedia Jenerali Mohammad Kazemi na Naibu wake, Jenerali Hassan Mohaqiq.

Hili linachukuliwa kama pigo jingine kubwa kwa mifumo ya ulinzi na ujasusi ya Iran, na linaashiria kuendelea kwa mkakati wa Israel wa kuondoa vipengele muhimu vya uwezo wa kiusalama na nyuklia wa Tehran, huku ikiepuka maangamizi makubwa ya raia au uharibifu mpana wa miundombinu.
 
Huu ndio udhaifu wao, mossad imeigeuza Iran kama choo cha stendi ambapo tu yeyote anaweza kuingia, cha ajabu zaidi haya matukio yanajirudia na hakuna siku intelligence ya Iran wamefanikiwa kukamata hata mamluki mmoja wa mossad achilia mbali kuuvunja huo mtandao.
 
Ulifuatilia wakati vita vya Urusi na Ukraine vinaanza ? Target ya majeshi ya Ukraine kwa Urusi ilikuwa nini ? Na je walifanikiwa au wamefanikiwa kipi mpaka sasa kuwatoa Urusi katika nchi yao ?
 
Naendelea kusema watakuwa wajinga sana kuingia ofisini kwenye vyumba vyao vya Siri kwenye mazingira ambayo wanawindwa.

Kwamba walishindwa kufanya kazi kutoka maeneo tofauti Hadi waende ofisini?

Kiufupi Israel itawamaliza maana inaonesha wanajua Kila kitu na Kila mahala.
 
Iran alitegemea yale mazungumzo na Marekani kununua muda,Israel kamfanyia surprise.
 
Hii vita mkuu imeshaingiliwa na propaganda.
Walidai kuwa Foreign ministry ya Iran iliifuata Qatar kuomba mediation,Iran foreign minister akakanusha hiyo taarifa.
Propaganda zishakua nyingi kwenye hii vita.
Vita yoyote unayo ijua lazima inatumia propaganda mfano videos clips za ballistic missile za Iran tunazoziona kwenye media au ukubwa anao pewa Israel na mossad ni Propaganda

Propaganda ina deals na kuharibu au kutengeneza psychology ya watu kuhusu jambo frani

Propaganda zinatumika kutengeneza molari Kwa Askari huwez kupigana vita ukiwa na akili timamu inatakiwa tukutoe fyuzi kichwani ndio maana unaona watu wanashangilia vitoto vidogo vinauawawa Gaza na watu Wana shangilia

Check this hili ni gazeti enzi hizo inawatayalisha watu kwenda front kupiga joka jeusi nduli idd Amini
 
Bado kwa Kiduku
Ni nani atamfunga paka kengele ?

Nitajie taifa moja tu lenye guts za kurusha makombora Pyongyang ?

Mind you kuishambulia North Korea ni kuishambulia China maana China ina mkataba na nchi moja tu duniani kuilinda pale ikivamiwa kijeshi sasa sijui ni nani huyo kichaa yupo tayari kupigana na China na North Korea kwa wakati mmoja kwa faida zipi pia hao wawili ni nuclear power countries
 
Kunywa soda tukasikilize mawaidha!!!
 
Iran alitegemea yake mazungumzo na Marekani kununua muda,Israel kamfanyia surprise.
Kuna namna Iran ilirudisha imani kwa marekani rafiki wa kufa na kuzikana na Israel lilikuwa ni kosa.

Inapaswa pia kupiga marufuku vinu vyake kuchunguzwa kutoa uhuru kuchunguzwa hili ni kosa pia naona wanafanya maana mifumo ya kidunia haipo upande wao ila wao wana iamini.

Jambo lengine nalo ona siasa za Iran zimegawanyika kiasi fulani kati ya moderate na hard-core sidhani kama ni nzuri sana ndani ya serikali kuwe na mgawanyiko huo ukizingatia adui anaye mkabili atatumia udhaifu huo huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…