kama hautojali.... hio[emoji115] aya ya mwisho inahitaji maelezo zaidi maana naona umeandika vitu complex sana kwa mchanganyiko nashindwa kuelewa kwa ufasaha unamaanisha nini
kama hutojali kushea maarifa
Nchi inavutia wawekezaji kwenye uchumi wake kulingana na sera zake rafiki na imara. Udhaifu waliouonesha Western countries ndani ya mwezi mmoja inatoa alert kwa Investors na nchi zingine kujitafakari kwa umakin zaidi. Hiyo sera ya unyang'anyi ni wizi mkubwa kwa watu wasiohusika.
Fikiria nchi zilizohifadhi Assets zao katika fedha za kigeni kutoka nchi zenye sera za namna hiyo. Siku wakipigwa stop kuzitumia fedha hizo watapoteza kiasi gani katika Reserves zao? So kitachoendelea uko mbele ni kuanza kubadil reserves zao kwenda stable assets kama Gold n.k
Nchi hizi (Western Countries) zimekuwa na mwelekeo wa nchi nyingi kwenda kuhifadhi na kuwekeza kutokana na hii "stability" ambayo kwa sasa ni kama imeyumba. High inflation inapunguza Power of purchase ya Currency husika.
Hasa Dollar, iko active kwasabab ya Uhitaji wake sokoni katika biashara. Uhitaji huu ukipungua na stability inapotea. So nchi zilizohifadh Dollar notes zitaanza kuzifanyia exchange to others assets ambazo ni stable kuendelea kuhifadh thaman yake.
"Shifting" hiyo itapelekea US na western kupoteza control ambazo wangez'impose kupitia uko. Na hii kwa mfano ni mbaya kwa US (kwa mujibu wa wachambuzi kutoka huko huko US) wanaosema deni la taifa ni kubwa. Inflation itarise high interest kwenye hilo deni na kupelekea hilo deni kua gumu kulipa.
Kingine kibaya zaidi kwa Europe katika jitihada za kumridhisha US, wanamsukuma Russia kua rafiki wa kufa na kufaana na China zaidi apo uone kua Nchi nyingi hasa Middle East ni kama vile zimechoka utawala wa amri na vitisho kutoka magharibi... Hii italeta pigo kubwa zaidi Europe na Western uko kwa Canada na USA.
Na wengine wanaenda mbali zaidi wanadai kwa vita hii ya kiuchumi itapelekea mgawanyiko wa kimipaka. Kwamba kutakuwa na North West ikiongozwa na US na washirika wake apo Ulaya kisha East South ikiongozwa na India Russia na China na wengineo...
Ukumbuke Russia ana Resources nyiiiingi sana na China ana viwanda viiingi kupindukia. Huo muungano uko much beneficial kupitiliza. Apo ndio utakapotofautisha Quantity na Quality.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hayo sio maneno yangu ni maneno ya wachambuzi kutoka apo apo baran ulaya. Ndio maana utaona nchi kama Hungary kawa mbishi kushiriki kikombe cha jumuiya dhidi ya Russia.
Europe mambo si mambo ingawa media zinaficha ila za pembeni zinapatikana. Sawa na hali mbovu ya kiuchumi apa TZ media hazisemi ila kuna wakereketwa apa JF wanazizungumza vizuri tu mtu unaelewa.
Ni mengi meeengi mengine kuandika ni issue, sema kikubwa hii transform ya power kutoka kanda moja kwenda nyingine ifanyike kwa salama. Kwasaba ukigeuka nyuma kwenye historia inaonesha kila Power imedondoka kwa vita... Hii USSR na rise of US imetokea kwa vita. So kwa hii nayo dah yetu macho tu.