Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Wewe ndo wasema ila wenyewe wanatumia vizuri tu na tena kampuni kubwa kama Rossiya nusu ya ndege zake ni kutoka Urusi na chache ndo Boeing.kidogo wanatumia Airbus ya France. Kampuni kubwa kama Aeroflot imeachana na kununua Boeing kwa sasa.imeweka Order kwenye ndege mpya ya Kirusi.sasa unasemaje hazitumiki urusi?
Niliomba ujielimisha. Kwa nini vitatangazwe vikwazo kama viko?? Hakuna vikwazo vinavyotaja mkate, mayai au maji, ninavyojua. Nyundo na misumari unaweza kuuza Urusi pia.
Vifaa vilivyopo vilinunuliwa nje na kuingizwa. Au vilitengenezwa na makampuni ya magharibi yaliyokuwa na viwanda ndani ya Urusi na kuzalisha huko. Serikali inaweza kukamata viwanda hivi na kuamuru viendelee. Lakini baada ya muda mfupi wataona matatizo ya vipuli, mara kwa mara pia elimu ya wasimamizi kutoka nje walioongoza uzalishaji hadi sasa.
Hujajiuliza kwa sababu makampuni yoooote ya ndege za Urusi (yako mengi) yanatumia ndege za Boeing au Airbus? Kwa nini hawatumii Tupolev? Sema!
 
Zipo sehem nyingi tu ila moja wapo ni hii List of foreign aid to Ukraine during the Russo-Ukrainian War - Wikipedia

Ukaone namna hawa watu walivo wanyama. Kuna nchi zingine zimetuma silaha tupu ila hata ile sh 10 ya humantarian Aid hawajapeleka.

Hapo EU hiyo B1 Euro wanayoitaja ni ya Military Aid pekee ilhal Msaada wa kibinadam ni Just Euro Mil 500 tu.

Na katika nchi zilizomo ndani ya hyo Organization wengiwao vil vile wametuma zaidi Weapons kuliko mahitaji ya kiraia.

List iko ndefu mno...
Ukiachilia mbali nchi kuna makampuni zaidi ya 100 utayaona hapo kwa hapa ntayataja machache yako nyuma ya Ukraine kumpa support ya kila hali.
1. Microsoft Corp.
2. Meta Platforms
3. GOOGLE
4. SpaceX
5. Snap
6. Amazon
7. Kakao
8. Kel-Tec
9. SK Group n.k

Nikurudishe nyuma EU Aid iko hivi (kwa hapa tunazungumzia Ule umoja wao sio nchi moja moja)
1. Military Aid worth more than 1B euro
2. Humantarian Aid worth of 500Million Euro
3. Satellite intelligence ila bado wanakwapuliwa.

US pekee
1. More than 14B US dollars as Millitary Aid
2. 1B US dollars as Humantarian Aid

Hiyo list ukiitizama kisha wakaa chini unajiuliza kwa hii support bado mtu anakalishwa. Ni taasis za kimataifa, kuna Makampuni, kisha uje kwa nchi washirika kisha waambiwa Russia masikin kafilisika kwenye hii vita unabaki mdomo wazi.

Ukirudi tena kuitizama hio list ya hizo Aids kisha uone wanatoka kutangaza uhitaji wa silaha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wajiuliza kwani hizo walizopewa zimeyeyuka [emoji848][emoji848][emoji848]...

Some people with no brain wanaendela kusema kua Russia ni Super Power wa mchongo. [emoji119][emoji119][emoji119]

Misaada yote hiyo Hata chakula,maji hamna mpaka warusi wapeleke hatar sana,,,,nimeona clips kuna jamaa na wenzake walijifisha Kwenye bunker hawakua na chakula wala maji a kasema wengine wamekufa na njaa,hao NATO wanachojua ni weapons tu.
 
Hii nondo inastahili Uzi kivyake, tuchambue uchumi hafifu wa Urussi. Sijui hiki cheo cha Super Power na kawapa sababu hawastahili kabisa.
Sitaki kushiriki katika ushabiki kupunguza hadhi ya Urusi. Ila wale wanaopoteza sauti hapa kusifu ubora wake hawaoni hali halisi. Tangu kushambuliwa vibaya na Ujerumani wakati wa vita ya pili, Urusi ilitumia sehemu kubwa mno ya uchumi wake kujenga jeshi na kuwekeza katika silaha. Hivyo walikuwa miaka yote ya ukomunisti na uchumi iliyoweza kutengeneza silaha nyingi, silaha kadhaa bora, hawakufaulu kutengeneza gari la kawaida bora, waliwapa wananchi chakula cha kimsingi lakini sehemu kubwa ya watu ilibaki maskini. Walipojitahidi na kukazia nguvu zote walipeleka watu angani (Mwezi walishindwa) na vyomboanga hadi sayari nyingine. Hii waliweza kwa kutuia uchumi wa kiimla, bei yake ilikuwa hali duni ya watu wengi.
Baada ya ukomunisti wanakabiliwa na ufisadi na rushwa kupita kiasi. uchumi unakosa uhakika na hapo watu wenye hela wanajitahidi kuwekeza nje ya nchi, na watu wa nje wanasita kuwekeza katika Urusi kwa sababu ya mashaka. Yaani wawekezaji wako lakini idadi si vile jinsi inavyowezekana...
Viwanda vingi vilivyopo vinategemea tekinolojia ya nje - sasa haina nuhakika kutokana na vikwazo
Urusi kuna wataalamu wazuri, mahandisi wazuri - ila nusudikteta (siku hizi imefikia 3/4 au 5/6) inasababisha wengi wenyi vipaji kuondoka na kutafuta maisha nje.
 
Na siku zote ukitumia mabavu utafail tu,Ulimwengu wa sasa ni wa kutumia akili zaidi.Sasa atapigana na wangapi kwa wakati mmoja wakati tu hapo Ukraine bado ndiyo kwanza kumekucha
Ni kweli. Mabavu hayajawahi kuwa na hitimisho sahihi la muda mrefu. Mwisho wa siku lazima uweke silaha chini mzungumze kama binadamu.
 
Wewe ndo wasema ila wenyewe wanatumia vizuri tu na tena kampuni kubwa kama Rossiya nusu ya ndege zake ni kutoka Urusi na chache ndo Boeing.kidogo wanatumia Airbus ya France. Kampuni kubwa kama Aeroflot imeachana na kununua Boeing kwa sasa.imeweka Order kwenye ndege mpya ya Kirusi.sasa unasemaje hazitumiki urusi?
Mimi ningefuata hapa habari za wikipedia, usipopenda lete vyanzo vyako (WIkipedia inaonyesha vyanzo vyake):
The Aeroflot passenger fleet consists of narrow-body and wide-body aircraft from six aircraft families: the Airbus A320, the Airbus A330, the Airbus A350, the Boeing 737, the Boeing 777, and the Sukhoi Superjet 100. As of March 2020, there are 247 passenger aircraft registered in the Aeroflot fleet

Kati ya hizi ndege 247, 10 zinatajwa kuwa Sukhoi, ndege ya Kirusi ("regional jet", si ya mbali, nikielewa vema ya abiria 100, bado nusu ya thamani yake ni vipuli kutoka magharibi - tafadhali uone kama unapata habari tofauti).

Kwa hiyo - watumie ndege gani wasipotaka kutumia Boeing au Airbus??
 
😂😂😂 wenzako humu wanalalamika kuwa 🇷🇺🇷🇺 anapigana huko vitani na mataifa zaidi ya 30 akiwemo 🇺🇸🇺🇸. Harafu wewe unasema kama wanauwezo waingie vitani 😂😂😂
Mbna mnajichanganya was🇷🇺 wa buza ?
Umeshauriwa uandike vizuri utaeleweka!
 
Tatizo Tunaamini habari zinazoandikwa na google bila kujua hawa wanaomiliki mitandano ni washirika wa Marekani na NATO, kipigo amabacho kinaendelea huko ni kikali sana ndio maana Marekani wala nchi yeyote ya Nato haijaenda kule directly , wanasingizia kuwa UKREIN sio mwanachama wa nato bado, SIWAMPE UANACHAMA KWA DHARULA halafu wamsaidie wanajua MZIKI WAKE
Mara mnasema Urussi inapigana na NATO Ukraine tena mnageuka mnasema NATO iingie Ukraine. Mbona mnarukaruka kama chura juu ya gogo.
 
Mngekuwa mnaweka na time frame kabisa,Huo muda kidogo ni muda gani?
Vikwazo vya awali zaidi ya mwezi vilionekana havizaa matunda ndio maana wanazidi kukaza!Russia naye amekuwa na counter measures dhidi ya vikwazo!
Na Bado Putin anasema operation itakwisha pale malengo yatakapifikiwa!
Sidhani kama Russia alikurupuka,alijua yatakayitokea na athari za vikwazo kwako na namna ya kukabiliana navyo!Hapo hapo ana support ya mataifa makubwa kama China na India yenye watu zaidi ya billion kila mmoja!
Athari za vikwazo Russia zipo lakini si Kwa kiwango kilichotegemewa na waweka vikwazo!
Kaka tumia akili, usipuuze!
Muda kidogo kwa vikwazo naona nusu mwaka, mengine zaidi. Mwaka 1, 2.
Ukiamua alijua kila kitu - basi.
Msaada wa Uhindi? Inanunua mafuta kidogo kwa sababau putin anapaswa kushusha bei. Soma juu, marafiki wa Putin walileta nukuu Uhindi inanunua kiwango ambacho EU inanunua kwenye nusu siku. (Sikuchungulia, inawezekana).
Msaada wa China? Hadi sasa si mengi. Mfano vipuli vya kompyuta; China yenyewe inategema tekinolojia ya Marekani. Wakiwasaidia Warusi vitu hivi, watapigwa ban wenyewe katika vipuli hivi.
China itaendelea kuchezacheza. Hawapendi Marekani, hawapendi mashambulio ya Putin. Tuangalie dansi yao.
 
Sitaki kushiriki katika ushabiki kupunguza hadhi ya Urusi. Ila wale wanaopoteza sauti hapa kusifu ubora wake hawaoni hali halisi. Tangu kushambuliwa vibaya na Ujerumani wakati wa vita ya pili, Urusi ilitumia sehemu kubwa mno ya uchumi wake kujenga jeshi na kuwekeza katika silaha. Hivyo walikuwa miaka yote ya ukomunisti na uchumi iliyoweza kutengeneza silaha nyingi, silaha kadhaa bora, hawakufaulu kutengeneza gari la kawaida bora, waliwapa wananchi chakula cha kimsingi lakini sehemu kubwa ya watu ilibaki maskini. Walipojitahidi na kukazia nguvu zote walipeleka watu angani (Mwezi walishindwa) na vyomboanga hadi sayari nyingine. Hii waliweza kwa kutuia uchumi wa kiimla, bei yake ilikuwa hali duni ya watu wengi.
Baada ya ukomunisti wanakabiliwa na ufisadi na rushwa kupita kiasi. uchumi unakosa uhakika na hapo watu wenye hela wanajitahidi kuwekeza nje ya nchi, na watu wa nje wanasita kuwekeza katika Urusi kwa sababu ya mashaka. Yaani wawekezaji wako lakini idadi si vile jinsi inavyowezekana...
Viwanda vingi vilivyopo vinategemea tekinolojia ya nje - sasa haina nuhakika kutokana na vikwazo
Urusi kuna wataalamu wazuri, mahandisi wazuri - ila nusudikteta (siku hizi imefikia 3/4 au 5/6) inasababisha wengi wenyi vipaji kuondoka na kutafuta maisha nje.
Hii comment imemaliza kila kitu
 
Back
Top Bottom