Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Wewe ndo wasema ila wenyewe wanatumia vizuri tu na tena kampuni kubwa kama Rossiya nusu ya ndege zake ni kutoka Urusi na chache ndo Boeing.kidogo wanatumia Airbus ya France. Kampuni kubwa kama Aeroflot imeachana na kununua Boeing kwa sasa.imeweka Order kwenye ndege mpya ya Kirusi.sasa unasemaje hazitumiki urusi?
 

Misaada yote hiyo Hata chakula,maji hamna mpaka warusi wapeleke hatar sana,,,,nimeona clips kuna jamaa na wenzake walijifisha Kwenye bunker hawakua na chakula wala maji a kasema wengine wamekufa na njaa,hao NATO wanachojua ni weapons tu.
 
Hii nondo inastahili Uzi kivyake, tuchambue uchumi hafifu wa Urussi. Sijui hiki cheo cha Super Power na kawapa sababu hawastahili kabisa.
Sitaki kushiriki katika ushabiki kupunguza hadhi ya Urusi. Ila wale wanaopoteza sauti hapa kusifu ubora wake hawaoni hali halisi. Tangu kushambuliwa vibaya na Ujerumani wakati wa vita ya pili, Urusi ilitumia sehemu kubwa mno ya uchumi wake kujenga jeshi na kuwekeza katika silaha. Hivyo walikuwa miaka yote ya ukomunisti na uchumi iliyoweza kutengeneza silaha nyingi, silaha kadhaa bora, hawakufaulu kutengeneza gari la kawaida bora, waliwapa wananchi chakula cha kimsingi lakini sehemu kubwa ya watu ilibaki maskini. Walipojitahidi na kukazia nguvu zote walipeleka watu angani (Mwezi walishindwa) na vyomboanga hadi sayari nyingine. Hii waliweza kwa kutuia uchumi wa kiimla, bei yake ilikuwa hali duni ya watu wengi.
Baada ya ukomunisti wanakabiliwa na ufisadi na rushwa kupita kiasi. uchumi unakosa uhakika na hapo watu wenye hela wanajitahidi kuwekeza nje ya nchi, na watu wa nje wanasita kuwekeza katika Urusi kwa sababu ya mashaka. Yaani wawekezaji wako lakini idadi si vile jinsi inavyowezekana...
Viwanda vingi vilivyopo vinategemea tekinolojia ya nje - sasa haina nuhakika kutokana na vikwazo
Urusi kuna wataalamu wazuri, mahandisi wazuri - ila nusudikteta (siku hizi imefikia 3/4 au 5/6) inasababisha wengi wenyi vipaji kuondoka na kutafuta maisha nje.
 
Na siku zote ukitumia mabavu utafail tu,Ulimwengu wa sasa ni wa kutumia akili zaidi.Sasa atapigana na wangapi kwa wakati mmoja wakati tu hapo Ukraine bado ndiyo kwanza kumekucha
Ni kweli. Mabavu hayajawahi kuwa na hitimisho sahihi la muda mrefu. Mwisho wa siku lazima uweke silaha chini mzungumze kama binadamu.
 
Mimi ningefuata hapa habari za wikipedia, usipopenda lete vyanzo vyako (WIkipedia inaonyesha vyanzo vyake):
The Aeroflot passenger fleet consists of narrow-body and wide-body aircraft from six aircraft families: the Airbus A320, the Airbus A330, the Airbus A350, the Boeing 737, the Boeing 777, and the Sukhoi Superjet 100. As of March 2020, there are 247 passenger aircraft registered in the Aeroflot fleet

Kati ya hizi ndege 247, 10 zinatajwa kuwa Sukhoi, ndege ya Kirusi ("regional jet", si ya mbali, nikielewa vema ya abiria 100, bado nusu ya thamani yake ni vipuli kutoka magharibi - tafadhali uone kama unapata habari tofauti).

Kwa hiyo - watumie ndege gani wasipotaka kutumia Boeing au Airbus??
 
Umeshauriwa uandike vizuri utaeleweka!
 
ukiwa unatumia app sio rahisi video kufunguka kwaio ukitaka kufungua video iclick hiyo video hlf nenda pale juu kwenye 3 dots itakuja option ya google chrome unatizama hlf unarudi kwenye app kuperuzi
Shukran MKUU imekubali
 
Mara mnasema Urussi inapigana na NATO Ukraine tena mnageuka mnasema NATO iingie Ukraine. Mbona mnarukaruka kama chura juu ya gogo.
 
Kaka tumia akili, usipuuze!
Muda kidogo kwa vikwazo naona nusu mwaka, mengine zaidi. Mwaka 1, 2.
Ukiamua alijua kila kitu - basi.
Msaada wa Uhindi? Inanunua mafuta kidogo kwa sababau putin anapaswa kushusha bei. Soma juu, marafiki wa Putin walileta nukuu Uhindi inanunua kiwango ambacho EU inanunua kwenye nusu siku. (Sikuchungulia, inawezekana).
Msaada wa China? Hadi sasa si mengi. Mfano vipuli vya kompyuta; China yenyewe inategema tekinolojia ya Marekani. Wakiwasaidia Warusi vitu hivi, watapigwa ban wenyewe katika vipuli hivi.
China itaendelea kuchezacheza. Hawapendi Marekani, hawapendi mashambulio ya Putin. Tuangalie dansi yao.
 
Hii comment imemaliza kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…