Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hapo ni Ukraine plus NATO!
Upo sahihi. Na Urusi ilishatoa onyo pia NATO kutoingilia lakini naona bado anajikita na kuiharibu Ukraine na kuua watu wake badala ya kukaa chini na giant wenzake.

Urusi Ideal na NATO moja kwa moja, ikae chini na giant mwenzake mwenye nguvu NATO wamalizane bila kuonyeshana umwamba kupitia nchi ndogo kijeshi.
 
Pro NATO mbn mna dhihaka sana. Unamzarau mtu usiyemjua. Pengine ukute huyo mtu kakuzidi kila kitu kielimu sio tu kiingereza.

Jadilini hoja wacheni kujadili watu. Au mmeishiwa hoja!? Mkishindwa kutoa majibu kwenye maswali/Hoja za watu ni akheri mnyamaze na sio kuanza kumdharau mtu na kumdhihaki na ilhali humjui. Ndio maan jf zinatumika anonymous id maana identification ya mtu si muhimu cha muhimu ni alichokuwa nacho kichwani maoni, ujuzi, etc



Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Hwana akili hao watoto asbh nimetoka sema leo hawajaenda chuo na shule huu uzi utavamiwa sana leo na watoto.
 
Wadau kuna kitu najiuliza mpaka sasa labda mtanisaidia majibu.

Inasemekana kwamba URUSI ina ndege za kisasa za kivita, kwanini asingeipiga UKRAINE kwa anga muda mfupi yeye akachagua kwenda kwenye vita na vifaru, magari na wanajeshi wa Ardhini?

Matokeo yake amepoteza idadi kubwa ya Mwanajeshi, vifaru, magari?
Ukraine wana Short range air defense system (MANPADS) tena nyingine ni za kisasa na very sophisticated Kama Starstreak ya Uingereza. Hii Satrstreak ya UK ni noma,Kwanza ndo short range air defense system yenye Kasi zaidi kuliko zote duniani yaani ikifyatuliwa tu inafikia Kasi ya mpaka mara nne ya speed ya sauti (Mach 4),pia haiwezi kua jammed au fooled na countermeasures. Hii ikifyatuliwa maana yake ndege Vita ya adui haina muda wa kureact kutokana na speed yake.
Ndo maana mpaka sasa unaona Urusi ameshindwa kupata air superiority kwenye anga la Ukraine anachofanya ni kurusha tu Cruise missiles kutokea mbali baharini,Belarus au kutokea kwenye ardhi Yake.

Angalia hapa hii Helicopter ilivyokatika vipande viwili baada ya kupigwa na Starstreak
 
US ni mnafiki tena mnafiki kupindukia, hajui fair play katika ushindani, bado ana hila na mbinu za kizamani kwenye ushindani wa kiuchumi na kimadaraka. Anampiga vita kila mshindani wake kwa jina la "Democracy" ilhali anachokifanya hakiendani na kile anachokitoa kwenye kauli.

Jana nilikuwa namskiliza yule Secretary wa Pentagon, anadai China ni Main Threat kwao in term of economy na watahakikisha unification ya Taiwan na Mainland China haitotokea kwa kila hali kadri wawezavyo...

Na ukiangalia katika hizi nchi 3 hasa ndani ya nchi 5 za BRICS, Russia ni so Powerful in term of Military, China nae ni Powerful in term of Economy, India is the Largest market in South and Eastern Asia. Huo muungano ni Threat kubwa kwa sustainability ya US.

Sasa ukiangalia hizo nchi ziko thousands of mile kutoka kwenye mipaka yake... Ye anajiona yuko sawa ila yule anayeshughulika na threat mlangoni mwake anamtangaza namna tunavyosikia hivi sasa.

Kama wakumbuka tena kabla ya huu mgogoro kuanza Biden wakati anazungumza na CEOs wa Giants Companies ndani ya US aliwaambia tunaelekea into NWO... Na kwenye hiyo NWO we should take a lead.

Wakati huo huo Putin na Lavrov wamekua wakiirudia sana hii kauli ya kua mwisho wa US hegemony umefika, mwisho wa Unipolar World ndio huu na mwanzo wa Multipolar world ndio huu... Katika dunia ambayo haitakuwa na kiranja mmoja ka ilivokuw tangu vita baridi viishe.

So hapo ndio utapata picha kwanini India na China wamemgomea kwa kila kitu US na wenzao... Utaona kwanini Midle East hasa Gulf region zimetulia tulii kiasi cha Saudia na UAE kuanza kuzichunia Sim za Washington.

US hana ushawishi sahvi watu wameshashtuka toka usingizini wanasubiri kukuche. Tukiwaambia unipolar world inakwenda kufa kuna watu humu ndani wanapiga kelele,
 
Ni proRussia yupi ambaye hataki kukubali kwamba hiyo meli kweli imezama!? Mtaje tumcheke na usipomtaja tutakucheka wewe. Muongo!!!

Kwani wewe unakubali meli imezama au imezamishwa!?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Nyie hizo za kuzama mnazitoa wapi? Triga unaniangusha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Screenshot_20220415-123623-01.jpg
Catch in fire but afloat... Pentagon hawajui chanzo cha issue hiyo hapa JF mshajua nani kaipiga [emoji847]... Dah kweli wabongo ni konyo...

Hiyo source kutoka western, Ingekuw Sputnik au RT ingesemwa Russia anajitetea.
 
Unahitaji ndege nzuri kivita, mafunzo, uzoefu na adui dhaifu kuweza kushambulia kwa ndege angani bila ndege zako kutungiwa kwa wepesi.
Wadau kuna kitu najiuliza mpaka sasa labda mtanisaidia majibu.

Inasemekana kwamba URUSI ina ndege za kisasa za kivita, kwanini asingeipiga UKRAINE kwa anga muda mfupi yeye akachagua kwenda kwenye vita na vifaru, wanajeshi wa Ardhini?

Matokeo yake amepoteza idadi kubwa ya Mwanajeshi, vifaru, magari?
 
Urusi sio kitu cha ajabu kuiteka Ukraine, cha ajabu ni Urusi kushindwa kuiteka. Ukisoma comments zangu za mwanzo uzi huu sikuwa natarajia Urusi akae muda wote huu akiwa hana gains za maana.

Operation imefanyika as if Ukraine ni Al Shabaab kwamba unaleta vifaru unajipigia tu. Watu wana hasira 2014 walichukuliwa Crimea wakaamua isiwe ugomvi watapigwa wakajisalimisha, mara kidogo Donetsk na Luhansk zikachukuliwa kwa false allegations. Leo hii Kremlin na FSB yao eti wakashindwa kujua jinsi Ukraine ilivyofika hatua ya kujikataa itapigana vikali. Wakategemea mserereko wa "neo-nazis" na raia ambao ni friendly kwa Russia, mambo yakaja sio.

Huu uzi ulianza pro-Russians wanamuita Zelenskiy eti Joti hawezi kumkabili Putin ex-spy. Sasa umemshindwa Joti kwa muda wote huu utamuwezaje Nape au Lissu. Yani Zelensky mchekeshaji na unyonge wa Ukraine anafanya hivi je itakuwaje kwa Andrzej Duda wa Poland ambaye ni mwanasheria. Itakuwaje kwa Sauli Niinisto wa Finland na nchi zote hizo zina capabilities kubwa kuliko Ukraine
Unataka Urusi waiteke Ukraine hata kama wenyewe hawana malengo ya kuiteka Ukraine!?

Lets be objective here!
Unafikiri lengo la Urusi lilikuwa kuiteka Ukraine, ok fine. Hebu tuambie projection yako inakuambia what would be next kama ukraine 'ingetekwa'!?

Yaani With all the facts on the table ingekuwa wewe ndio Putin 'ungeiteka' Ukraine kwa dhumuni lipi. Ni dhumuni lipi ambalo unahisi litafikiwa tu kwa kuiteka ukraine!

Kama kiongozi wa nchi unafkiri ni sahihi kuchimba shimo kubwa ili ufukie shimo dogo!? Kuiteka nchi ni jambo moja kuitawala baada ya kuiteka je!?

Putin kamshindwa Zelensky kivipi!? Au ilitakiwa mpaka amkamate amuue/amnyonge km alivyouliwa Saddam ndio tuseme hajamshindwa!? Jaribu kuwa specific utusaidie. Yaani huko kumshindwa wewe umekupimapimaje!?

Mimi kwa upande wangu ninaweza kusema Putin hajamshindwa Zelensky. Ukiniuliza km nilivyokuuliza nitakujibu pia ni vigezo gani nimetumia na ushahidi nitakuwekea ila mpk uniulize.

Karibu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Alichoandika kwenye uzi kwa lugha ya kiswahili na alichoambatinisha kwa video ya Kingereza ni kulia na kushoto.
Pro NATO mbn mna dhihaka sana. Unamzarau mtu usiyemjua. Pengine ukute huyo mtu kakuzidi kila kitu kielimu sio tu kiingereza.

Jadilini hoja wacheni kujadili watu. Au mmeishiwa hoja!? Mkishindwa kutoa majibu kwenye maswali/Hoja za watu ni akheri mnyamaze na sio kuanza kumdharau mtu na kumdhihaki na ilhali humjui. Ndio maan jf zinatumika anonymous id maana identification ya mtu si muhimu cha muhimu ni alichokuwa nacho kichwani maoni, ujuzi, etc



Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wadau kuna kitu najiuliza mpaka sasa labda mtanisaidia majibu.

Inasemekana kwamba URUSI ina ndege za kisasa za kivita, kwanini asingeipiga UKRAINE kwa anga muda mfupi yeye akachagua kwenda kwenye vita na vifaru, magari na wanajeshi wa Ardhini?

Matokeo yake amepoteza idadi kubwa ya Mwanajeshi, vifaru, magari?

Nadhani sifa za kijeshi anazopewa URUSI haziendani na uhalisia uliopo.

Kwa sifa alizokuwa anapewa asingekubali wanajeshi wake wafariki wengi hivyo na uharibu mkubwa wa zana zake za kijeshi.

Lipo tatizo mahali.
Ndio leo watu mnagundua hilo?

 
Nyie hizo za kuzama mnazitoa wapi? Triga unaniangusha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] View attachment 2188277 Catch in fire but afloat... Pentagon hawajui chanzo cha issue hiyo hapa JF mshajua nani kaipiga [emoji847]... Dah kweli wabongo ni konyo...

Hiyo source kutoka western, Ingekuw Sputnik au RT ingesemwa Russia anajitetea.
Hiyo Meli imeshazama na Urusi wenyewe wamekiri.
 
Vikwazo havifanyi kazi hivyo na mafuta na gesi ya Russia havijawekwa vikwazo mpaka wakati huu. Nchi nyingi tu za Ulaya bado wananunua gesi Russia.
binafsi siamin km marekan anaweza kuiwekea vikwazo india, lazima ujue ht uhusiano wa marekan na india umekuwa sana kpnd cha modi, japokuwa india still ana mahusiano makubwa kisiasa na urusi kuliko marekan but marekan anatambua ht hiki alichoambulia miaka hii ya karibun ni kikubwa sana kwake hawez thubutu kumuwekea vikwazo india, nadhan issue kubwa ni political support ya india kwa russia ndio inawachengua marekan hadi wanapiga kelele hivyo, china na india zimkuwa km mhimili wa kisiasa kwa urusi kpnd hiki kwakweli, imran khan kasumbua sana marekan na masheikh wa gulf yule siku zake zilikuwa zinahesabika tu huwez kuwa na sera huru km huna uchumi huru, uchumi wake unategemea pesa za waarabu halafu sera zake antk ziwe independent how?
 
Mfano,Kulikuwa na haja gani ya kupeleka ule msafara wa magari about 40 km kuelekea Kiev?

Kama mojawapo ya malengo ya hii vita ni demilitarization, na denazification kwanini Urusi asingetumia njia nyingine ambazo ni more effective kama drones, helikopta,na cruise missile,badala ya kutumia Tank nyingi,na magari ambayo kwa kiasi kikubwa ni easy target.
Nafikiri kwa vile wengi wetu ni vijana na wengi wetu ndiyo tunashuhudia kwa kuona military operation ama vita vinakuwaje kwa nukta ya kuwa zao la manufaa ya mitandao ya kijamii inatusaidia kuona kile ambacho mara nyingi kilikuwa cha kufichwa.

Historia ama movie ama kwa kile ambacho tunakishuhudia upande mmoja unapofanya mashambulizi dhidi ya upande mwengine ama kile tunachoonyeshwa baada ya mashambulizi kimetuathiri na tumekuwa na matawi mengi ya fikra kwa kutoa mawazo yetu kwa kuona hapa ni alama A hapa ni F.

Tukubali vita ni sanaa kama sanaa nyengine. Kama sanaa inavyokuwa na ubunifu zaidi vita nazo zina mbinu. Sanaa ya maigizo ipo wazi sanaa ya vita kwa asilimia kubwa ni yenye kufichwa. Muda mwengine nyote mnaweza msielewe, muda mwengine wahusika wenyewe ndiyo wanajua wanachokifanya ni kipi!

Tunaweza tukawa tunajua mwisho wa hiki kinachoendelea baina ya Russia na Ukraine lakini isiwezekane kujua ni njia ipi itakayotumiwa. Pentagon imesema kinachoendelea Ukraine wenyewe hawajui Russia anatumia mbinu gani. Waliyobahatika kufafanua walielezea hivi unachokizungumzia: Russia ilionyesha msafara ule kuelekea makao makuu ya nchi ya Ukraine. Lakini ifahamike makao makuu ya nchi yanalindwa kwa gharama ya namna yoyote.

Kitendo kile sehemu kubwa ya jeshi la Ukraine likatumika kuulinda Kieve. Russia alichokifanya ni kuuzunguka ule mji. Matokeo yake miji mingine ilibakiwa na idadi kiasi cha wanajeshi. Ukumbuke pia lengo ni demilitarize na lengo jengine ni kuondoa Nazi. Demilitarize ikafanyika lakini kukabakiwa na vikundi vidogo vidogo vya jeshi la Ukraine ndivyo hivyo vilivyoleta upinzani wa hapa na pale. Kwa kuwa idadi kubwa ya jeshi la Ukraine lilizungukwa Kieve hawa wanajeshi wa mitaani kupata msaada wa moja kwa moja ikawa ni ngumu. Kuondoa Nazi inahitajika upite mtaa kwa mtaa kwani wahusika hawa walijifícha kwenye makazi ya raia. Hapa utarajie operation itachukua muda mrefu ikiwa utahitaji kupunguza vifo vya raia. Ikiwa haujali unalipua tu!

Ila hakuna mpaka sasa anayejua Russia anatumia mbinu gani! Itakujakufahamika zaidi mchezo utakapo kwisha. Russia siwageni kwenye haya mambo ya kivita. Tujijengee utamaduni wa kuona kwa pande mbili: Ikiwa kitu tukikiangalia kina sintofahamu basi ujue aidha kina makosa mengi au kina mambo ambayoufahamu wetu haujafikia kiwango cha kukielewa kwa wakati huo.
 
Back
Top Bottom