Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Hapo ni Ukraine plus NATO!
Upo sahihi. Na Urusi ilishatoa onyo pia NATO kutoingilia lakini naona bado anajikita na kuiharibu Ukraine na kuua watu wake badala ya kukaa chini na giant wenzake.

Urusi Ideal na NATO moja kwa moja, ikae chini na giant mwenzake mwenye nguvu NATO wamalizane bila kuonyeshana umwamba kupitia nchi ndogo kijeshi.
 

Hwana akili hao watoto asbh nimetoka sema leo hawajaenda chuo na shule huu uzi utavamiwa sana leo na watoto.
 
Ukraine wana Short range air defense system (MANPADS) tena nyingine ni za kisasa na very sophisticated Kama Starstreak ya Uingereza. Hii Satrstreak ya UK ni noma,Kwanza ndo short range air defense system yenye Kasi zaidi kuliko zote duniani yaani ikifyatuliwa tu inafikia Kasi ya mpaka mara nne ya speed ya sauti (Mach 4),pia haiwezi kua jammed au fooled na countermeasures. Hii ikifyatuliwa maana yake ndege Vita ya adui haina muda wa kureact kutokana na speed yake.
Ndo maana mpaka sasa unaona Urusi ameshindwa kupata air superiority kwenye anga la Ukraine anachofanya ni kurusha tu Cruise missiles kutokea mbali baharini,Belarus au kutokea kwenye ardhi Yake.

Angalia hapa hii Helicopter ilivyokatika vipande viwili baada ya kupigwa na Starstreak
 

US hana ushawishi sahvi watu wameshashtuka toka usingizini wanasubiri kukuche. Tukiwaambia unipolar world inakwenda kufa kuna watu humu ndani wanapiga kelele,
 
Ni proRussia yupi ambaye hataki kukubali kwamba hiyo meli kweli imezama!? Mtaje tumcheke na usipomtaja tutakucheka wewe. Muongo!!!

Kwani wewe unakubali meli imezama au imezamishwa!?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Nyie hizo za kuzama mnazitoa wapi? Triga unaniangusha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Catch in fire but afloat... Pentagon hawajui chanzo cha issue hiyo hapa JF mshajua nani kaipiga [emoji847]... Dah kweli wabongo ni konyo...

Hiyo source kutoka western, Ingekuw Sputnik au RT ingesemwa Russia anajitetea.
 
Unahitaji ndege nzuri kivita, mafunzo, uzoefu na adui dhaifu kuweza kushambulia kwa ndege angani bila ndege zako kutungiwa kwa wepesi.
 
Unataka Urusi waiteke Ukraine hata kama wenyewe hawana malengo ya kuiteka Ukraine!?

Lets be objective here!
Unafikiri lengo la Urusi lilikuwa kuiteka Ukraine, ok fine. Hebu tuambie projection yako inakuambia what would be next kama ukraine 'ingetekwa'!?

Yaani With all the facts on the table ingekuwa wewe ndio Putin 'ungeiteka' Ukraine kwa dhumuni lipi. Ni dhumuni lipi ambalo unahisi litafikiwa tu kwa kuiteka ukraine!

Kama kiongozi wa nchi unafkiri ni sahihi kuchimba shimo kubwa ili ufukie shimo dogo!? Kuiteka nchi ni jambo moja kuitawala baada ya kuiteka je!?

Putin kamshindwa Zelensky kivipi!? Au ilitakiwa mpaka amkamate amuue/amnyonge km alivyouliwa Saddam ndio tuseme hajamshindwa!? Jaribu kuwa specific utusaidie. Yaani huko kumshindwa wewe umekupimapimaje!?

Mimi kwa upande wangu ninaweza kusema Putin hajamshindwa Zelensky. Ukiniuliza km nilivyokuuliza nitakujibu pia ni vigezo gani nimetumia na ushahidi nitakuwekea ila mpk uniulize.

Karibu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Alichoandika kwenye uzi kwa lugha ya kiswahili na alichoambatinisha kwa video ya Kingereza ni kulia na kushoto.
 
Ndio leo watu mnagundua hilo?

 
Hiyo Meli imeshazama na Urusi wenyewe wamekiri.
 
Vikwazo havifanyi kazi hivyo na mafuta na gesi ya Russia havijawekwa vikwazo mpaka wakati huu. Nchi nyingi tu za Ulaya bado wananunua gesi Russia.
 
Nafikiri kwa vile wengi wetu ni vijana na wengi wetu ndiyo tunashuhudia kwa kuona military operation ama vita vinakuwaje kwa nukta ya kuwa zao la manufaa ya mitandao ya kijamii inatusaidia kuona kile ambacho mara nyingi kilikuwa cha kufichwa.

Historia ama movie ama kwa kile ambacho tunakishuhudia upande mmoja unapofanya mashambulizi dhidi ya upande mwengine ama kile tunachoonyeshwa baada ya mashambulizi kimetuathiri na tumekuwa na matawi mengi ya fikra kwa kutoa mawazo yetu kwa kuona hapa ni alama A hapa ni F.

Tukubali vita ni sanaa kama sanaa nyengine. Kama sanaa inavyokuwa na ubunifu zaidi vita nazo zina mbinu. Sanaa ya maigizo ipo wazi sanaa ya vita kwa asilimia kubwa ni yenye kufichwa. Muda mwengine nyote mnaweza msielewe, muda mwengine wahusika wenyewe ndiyo wanajua wanachokifanya ni kipi!

Tunaweza tukawa tunajua mwisho wa hiki kinachoendelea baina ya Russia na Ukraine lakini isiwezekane kujua ni njia ipi itakayotumiwa. Pentagon imesema kinachoendelea Ukraine wenyewe hawajui Russia anatumia mbinu gani. Waliyobahatika kufafanua walielezea hivi unachokizungumzia: Russia ilionyesha msafara ule kuelekea makao makuu ya nchi ya Ukraine. Lakini ifahamike makao makuu ya nchi yanalindwa kwa gharama ya namna yoyote.

Kitendo kile sehemu kubwa ya jeshi la Ukraine likatumika kuulinda Kieve. Russia alichokifanya ni kuuzunguka ule mji. Matokeo yake miji mingine ilibakiwa na idadi kiasi cha wanajeshi. Ukumbuke pia lengo ni demilitarize na lengo jengine ni kuondoa Nazi. Demilitarize ikafanyika lakini kukabakiwa na vikundi vidogo vidogo vya jeshi la Ukraine ndivyo hivyo vilivyoleta upinzani wa hapa na pale. Kwa kuwa idadi kubwa ya jeshi la Ukraine lilizungukwa Kieve hawa wanajeshi wa mitaani kupata msaada wa moja kwa moja ikawa ni ngumu. Kuondoa Nazi inahitajika upite mtaa kwa mtaa kwani wahusika hawa walijifícha kwenye makazi ya raia. Hapa utarajie operation itachukua muda mrefu ikiwa utahitaji kupunguza vifo vya raia. Ikiwa haujali unalipua tu!

Ila hakuna mpaka sasa anayejua Russia anatumia mbinu gani! Itakujakufahamika zaidi mchezo utakapo kwisha. Russia siwageni kwenye haya mambo ya kivita. Tujijengee utamaduni wa kuona kwa pande mbili: Ikiwa kitu tukikiangalia kina sintofahamu basi ujue aidha kina makosa mengi au kina mambo ambayoufahamu wetu haujafikia kiwango cha kukielewa kwa wakati huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…